Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Huo mtaji wako ni Mzuri Kama ukiamua kufanya biashara ya duka la chakula au nafaka, mm nlianza na 4m na naendelea vyema, cha msingi ni kuwa makini pia uwe na heshima na pesa
unaweza kunisaidia mchanganuo wa biashara kwa 4m
 
Ndugu zangu naomba ushauri wenu nimekopeshwa ml 3.5 kwa miezi 6 naomba mnambie biashara gani nifanye kwa kipindi iki kigumu cha mzee wa kazi tu niweze pata Marejesho ya kla mwezi pamoja na riba ya asilimia 10
 
Ndugu zangu naomba ushauri wenu nimekopeshwa ml 3.5 kwa miezi 6 naomba mnambie biashara gani nifanye kwa kipindi iki kigumu cha mzee wa kazi tu niweze pata Marejesho ya kla mwezi pamoja na riba ya asilimia 10
Hongera kwa kupata Mkopo mi Niko tofauti na Mawazo ya Graduates wengi wa Humu ambao wangekushauri Ulime Matikiti bila kujua utatakiwa ulinde Ngedere/Nyani

Mkuu kwa Kua unafanya return kila mwezi biashara ya Mazao ni nzuri Kwako ila madali wanakera sana.
 
Hongera mkuu uko mkoa gani? ushaur wangu kwa sasa biashara chakula inalipa .
 


Kila kitu kinawezekana, Hizo picha ni huko kahama napochukua mchele na nlianza na mtaji mdogo tuu Kama wako lakini naona mambo yanaenda safi, cha msingi uwe kwenye location nzuri na mengine yatafuata ndugu yangu.
mkuu waweza niunganisha na mnunuz wa jumla wa mchele
 
Habari za leo,
Nahitaji ushauri zaidi. Nimepata 6m. Naam
Nikapata wazo LA kununua kirikuu used,
But suddenly nikawaza vitu vingi Sana kuhusu biashara ya kirikuu katika mahali nilipo but Inaweza leta faida but nakuwa kama nimesita.

Wazo 2,
Nipo na ufugaji wa nguruwe nipo nao 20.nawaza pia kuongeza mabanda na kuongeza mtaji wangu .
Note : pesa Nimepewa nitumie within 6 months na kurejesha Bila Riba.

Naomba tushauriane mawazo zaidi upande wa biashara kwa lengo LA kuwekewa hii fedha ili kaleta matokeo mazuri kwa Muda huu wa 6months.


Asante :nawakilisha.
 
Ningelikupa ushauri mzuri hakika ungelikufaa, lakini nimestuka kusoma unafuga nguruwe... Ngoja nikae pembeni.
 
Nunua mahindi makavu,mpunga au alizeti,weka godauni.After six months,, 6m itaweza leta hata Mara dufu.
 
achana na mambo ya kirikuu,tena used ndo hatari kabisa.kwa huo muda mfupi hivo wa miezi 6 biashara itakayokufanya upate faida ni ya kununua na kuuza bidhaa(trading),nadir uumize kichwa ujue bidhaa ipi itakutoa.
 
Nunua Bodaboda MPE mkataba after 12 months itakuwa ya kwake,but within a week akuletee hebsabu kiasi,Fulani ulizia huko ulipo kwa madreva wa mabodaboda.
Kwann umuingize mkataba?
1.ataitunza pikipiki akijua akimaliza miezi,mliyokubaliana itakuwa ya kwake,so hatoitumia vibaya.
2. Utakuwa umejiwekea mazingira bora bcoz Huo mkataba mtakuwa na terms zenu.
3. Itakupa faida ya haraka.
Take it or leave it,neno langu si sheria. But that's all I can advice for tonite.
 
Habari za leo,

Nahitaji ushauri zaidi. Nimepata 6m. Naam
Nikapata wazo LA kununua kirikuu used,
Nilikuwa mmoja wa wamiliki wakubwa wa virikuu, nilikuwa navyo virikuu vingi tu. Ila sasa sina hata kimoja. Hii ni biashara kichaa.
Mfano una virikuu vitatu, kimoja kitaleta hela leo, kingine dereva anakwambia kuwa anapeleka gari service, mwingine atakwambia tairi imeisha. Kwa hiyo baada ya wiki badala ya kupata hela ya virikuu vitatu, unaishia kupata kimoja. Wiki ijayo yule aliyeleta hela anakwambia anaenda service, huyu mwingine atakwambia mapato au bima inatakiwa kulipia.
So far, unaingojea hiyo laki moja kwa wiki alafu unaitumia ndani ya siku mbili imeisha unangoja tena kwa wiki.
Pia virikuu havidumu, vinawahi kufa engine. Ni bora uendelee na wazo la kufuga kiti moto... Hiyo biashara itakutoa maana soko la kiti moto ni kubwa mno...
 
Ni biashara nzuri ila faida yake ni ndogo mnooo!
 
Fungua mobile kitchen mkuu ambayo inaweza kua kwenye kirikuu kama upo dar lakini.Uwe unauza vitafunwa kama chapati, maandazi, vitumbua,bagia na mihogo ya kukaanga. Asubuhi inatega posta ,jioni inakua fire/kariakoo au sehemu yoyote yenye watu wengi. Hutakosa laki na hamsini kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…