Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Asante kwa ushauri mzuri kumbe hata kazi unataka [emoji3][emoji3]
 
Fanya utafiti mazingira unayoishi, angalia uhitaji wa wakazi wa hapo au chagua biashara iliyopo unayodhani itakulipo then ifanye kwa ubora zaidi. Achana na wanaokuuliza umetoa wap hiyo pesa je kama ulikua mwizi na unataka kufanya legal business, puuza hao wala usiwajibu.
 
Asante kwa ushauri mzuri mkuu
 
Shinyanga siyo mbali fika hapo lyamidati maeneo ya sindo. Kuna Uhaba mkubwa wa maji sijui kwa sas hali ipoje(nlikuw hapo mwaka juzi) ni almost 5 -8 km kutoka lyabukande. Fursa hiyo mkuu
 
Njoo hapa fays resort na hako kamtaji tuanzishe biashara ya kunywa bia
 
Nunua bodaboda 4
Boxer BM150 toleo jipya 2,400,000/=
x4 = 9,600,000/=
10M - 9.6M unabakiwa na 400k kwa ajili ya bima, sumatra usajili and everything

Kabidhi vijana wanne kila mmoja atakupa hesabu ya 10,000/= kwa siku
10,000 x 4 = 40,000

kwa week utaingiza 280,000
kwa mwezi 1,200,000

baada ya miezi 6 unaongeza bodaboda nyingine 3 zinakuwa 6
therefore kwa mwezi utakuwa unaingiza tsh. 1,800,000/= huo mshahara hata mbunge hakufikii, na ni stress free, umelala pesa inaingia tuu!
All the best, akili za kushauriwa changanya na za kwako...

 
Naunga mkono.

Ila bei ya boda boda inaweza kuwa chini ya hiyo bei pia
 
Mimi ni muumini wa uwekezaji wa muda mrefu, kwa mfano ungeenda iringa njombe ukanunua shamba la miti ukapanda kisha ukafanya mambo mengine. Kwa miaka 15 ijayo naamini utakua unazungumza lugha nyingine.

Au biashara ya mbao haswa mbao ngumu. Huwa hazishuki thamani kamwe, ila utafiti juu ya biashara hii ni muhimu na taratibu zote vibali nk.

Hardware nayo inalipa sana nayo pia inahitaji utafiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani mkuu
 
Asante sana mkuu hata Mimi kwenye hardware nilikuwa nafikiria
 
kwa mwezi si 1120000 mkuu au mahesabu yangu cjayapatia 280000×4 week
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…