Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?


Ramthods,

This is one of the best threads nilizowahikuzipitia kwa kweli. Nakumbuka wakati ile thread ikiwa hot mkuu Malila alifanikiwa kunishiwishi nirudi tena kny project ya misitu!
 

...ulaji huu, bado unaendelea...

jiwe la 1m/= (Tshs), linapatikana kwa 500,000/= mpaka 350,000/= kwa wale 'nyoka' na bei zao za jioni...

Unanunua na kurundika mzigo ndani (hayaozi haya), siku ya siku bei ziki shoot-up tena, aaah 😀

... Demand is always greater than supply kwenye mambo ya urembo.

au?
 
dogo Mbaraka Juma (mshiriki wa faidika na bbc) ameshika nafasi ya pili hivyo kakosa USD 5,000 kama mtaji wa kuanzisha mradi wake wa kufuga panya na vyura kwa ajili ya mafunzo ya upasuaji kwa wanafunzi wa A-level (Biology). Mradi huu una-sound kinoma kwani kupatikana kwa hawa specimen huwa shida sana kupatikana hasa kwa shule za Dar. USD 5,000 ni pesa kidogo sana, ningeshauri Mwana JF mmoja ajitolee kumpatia mtaji huyu dogo ili aendeleze ndoto yake, pia atakuwa ameunga mkono bbc ktk kushindanisha vijana kuibua fikra za kijasiliamali.
 

...cruelity to animals bana, angesema hao panya watasaidia ugunduzi wa TB au landmines kweli...


...a Belgian organization is using rats to alleviate two of Africa's greatest scourges: land mines and tuberculosis.

source; http://www.miller-mccune.com/mice/mine-heir-927
 
...cruelity to animals bana, angesema hao panya watasaidia ugunduzi wa TB au landmines kweli...

Mkuu hawa wanyama wanakuwa na matumizi mengi, kuwatumia kwa mazoezi ya upasuaji ni murua. Kumbuka ndo tunapata madaktari wa kutibia wanadamu na wanyama wengine hasa wa kufugwa majumbani, zoo, game reserves/parks etc. siyo ukatili mzee
 
Next Level, tayari umeshaanza kamili kamili kwenye hii project? Me ningependa sana kupata company nijitutumue misuli mkuu!

Yes mkuu....currently nakamilisha kuchukua ekari 16 kwa mwaka huu na kuwatika miti hapo Ir...then kny mwezi wa pili or tatu nikupanda....tamcheki Malila as well! Karibu mkuu
 
Malila et all

Shukhrani kwa mawazo kede kede ya kujenga...mradi kama hii ya misitu inatufaa sana Watanzania tulioko nje sababu haihitaji uangalizi wa kila siku na pia mitaji yake ni midogo.

Naomba nisaidie uzoefu wako kwenye hili suala la kusimamia

4. Msimu mzuri na maandalizi yake - Hasa eneo la Wami Luhindo, Morogoro.

Majirani zangu kule ni Wamasai wenye ng’ombe wengi (1500+). Ningependa kufahamu ni miti gani nikipanda haitaliwa na ng’ombe na itastahimili magugu kama ulivyogusia hapa chini



Nimeshauriwa nipande Jatropha lakini hili zao nina mashaka nalo kwa sababu tangu limegunduliwa kutoa mafuta ya mitambo miaka mingi haijapiota kuona hasa madhara yake kwenye arthi na mazingira kwa ujumla.



 
 
 

Minimum ni miaka kumi unaanza kuvuna mitiki yako,faida za mitiki ni hizi,kwanza unashika ardhi,fidia kwa mtiki mmoja ni balaa,bei yake ktk soko ni kubwa sana kwa sasa, eka moja inachukua mitiki 576 hivi kwa kipimo cha mita tatu kwa tatu. Ili upate mavuno bora panda 500 tu ktk eka moja.

Mtiki mmoja kwa sasa pale Dar unauzwa tsh 1500/ max na Tsh 500/as minimu. Usafiri sijui kama una gari au la, manpower ni maelewano zaidi.

Kama una eka 3 pale Mapinga nakushauri panda mitiki,wajenzi wa mahoteli watakufuata kununua,miche iko pale Mbezi kabla ya Pemmaco bevi. Msimu ni mwezi wa tatu/nne.
 
Next Level, tayari umeshaanza kamili kamili kwenye hii project? Me ningependa sana kupata company nijitutumue misuli mkuu!

Kampani gani unataka mkuu,wewe ni-pm uone mambo. Mkuu hapa ni kuanza kila kitu kiko wazi sasa. Nasisitiza tutaendelea kuwalaumu jirani zetu wa-Kenya mpaka lini?
 
Yes mkuu....currently nakamilisha kuchukua ekari 16 kwa mwaka huu na kuwatika miti hapo Ir...then kny mwezi wa pili or tatu nikupanda....tamcheki Malila as well! Karibu mkuu

Mkuu next l,

Kumbe ni wewe,siku moja tulikuwa wote Vingunguti bwana,na siku nyingine tulikuwa wote Mkuranga kule porini na yule jamaa dalali feki. Unakumbuka mimi niliachiwa kuendesha Kia fulani ya mjomba wa rafiki yako,rafiki yako na mjomba wake wakapanda Landcruiser ya jamaa yangu. Mimi nikazunguka nyie mkakatisha na Cruiser. Kule mimi nimeshalamba tayari kipande cha kutosha.
 
 

Ha!Ha!ha!ha!Ha!ha!HA!hah!a!H1hh1haaaaaa...... Malila wewe ni zaidi ya jiniazi mkuuu.....duuh...kumbukumbu zimekurudi haraka sana mkuu............Yes, mkuu tulikuwa na Kia that day, halafu tukawa na yule jamaa Mkinga na LandCruiser mkonga........ngoja nisimalizie.......!

Now network imerudi kabisa...........bwana ASIFIWE.....mkuu! now najua na job wapi upo sio? ngoja tuongelee kule jikoni.........!nakuPM?
 
Wakuu,

Swali jingine: mmeweza vipi kujiunga pamoja na kutimiza haya malengo? Mnajiongoza vipi na mnatatua vipi migogoro yenu?

Mradi wa kuvuna baada ya miaka 5+ mkiwa zaidi ya 10 na wote muwe kwenye mstari mmoja sio kazi ndogo.
 
Wakuu,

Swali jingine: mmeweza vipi kujiunga pamoja na kutimiza haya malengo? Mnajiongoza vipi na mnatatua vipi migogoro yenu?

Mradi wa kuvuna baada ya miaka 5+ mkiwa zaidi ya 10 na wote muwe kwenye mstari mmoja sio kazi ndogo.

Watanzania ni watu wazuri ila wamekosa kiongozi mwaminifu. Ktk hili sisi sote tumeanika uwezo wetu na udhaifu wetu wazi. Taarifa za kazi yetu ni za wazi,hesabu za kazi yetu(project) ni za wazi, kwa hiyo utakuta mwenye uwezo mkubwa anaweza kushirikiana na mnyonge bila taabu na bado hahisi kubebeshwa mzigo. Mnyonge anacho kitu cha kuchangia ktk project na kigogo ana kitu cha kuchangia ktk project zetu mkuu.

Kundi hili ni la watu wanaojua nini cha kufanya.ni mchanganyiko mzuri kweli,injiniasi,b/nessmen,politicians,students,pastors.

Mpaka sasa ni miaka 3,kila mmoja ameridhika na progress yetu. Kiongozi wetu mkuu ni mwaminifu sana na anaijua njia ya kupita na wenzake. Tumeokoa gharama sana kwa kufanya pamoja.
 


Kila la kheri Wakuu, kama mmefanikiwa hapo basi kipingamizi pekee kilichobaki kwenu ni mawingu..!!

Tutawasiliana zaidi.
 
Ni kweli usemayo,mmoja ilibidi tumwache baada ya kuona analeta politiki wakati sisi tuna maanisha. Alipokuja gundua tuko mbali alilia sana ili arudi kundini ikawa/na imekuwa nguma kukubalika tena.
 
Wakuu,

Ule mti wa mbao mwekundu ambao siku hizi unatumika sana badala ya mninga unaitwaje. Nasikia huu mti ni mgugu kuliko mninga...na kwa kweli rangi yake inavutia sana. Kuna mdau hapa anajua jina lake kwa kiswahili au kimombo?
 
kama ni mti wa mbao na sio wa kiasili yaani exotic unaitwa mlingoti mwekundu, kwa kizungu unaitwa Eucalyptus saligna. Eucalyptus grandis ni mlingoti mgumu lakini mweupe.

Kwa sasa eucalyptus saligna una-replace mbao ngumu sokoni kwa sababu wenyewe sio wa kiasili na ni hot cake kwa sasa. Ipo miti mingine migumu zaidi ya mninga lakini kwa sasa haipatikani sana. Labda ni mkongo,nao ni mgumu na rangi yake ni nyekundu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…