Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Malila,

unajua maeneo ya kwetu ardhi tabu sana nimepata ekari 60 maeneno ya Mbeya, nafikiria iwe nusu alizeti na nusu MITI....niambie Mkuu wangu

kama umepata eneo kubwa hivyo na linakubali mazao,miti usipande,nakuja mbeya mwezi october tutafutane,nitakuonyesha ardhi ya kupanda miti ya mbao bomba zaidi,hiyo ardhi dili mkuu,huko ninakosema kuna ardhi ya kumwaga na ni karibu sana na mbeya mjini. Ktk eneo hilo panda miti ya matunda sio mbao.
 
Malila,

Mimi Ogah, ninaomba kujiunga na kikundi chenu ili tuendeleze libeneke la miti....au unasemaje Mkuu

Timu yetu haibagui mtu,ila tuna kiwango ambacho tunadhani tunaweza kwenda pamoja. Mtu akisema anataka kupanda miti mia moja,hatuwezi kumkataa ila tunamshauri kitaalamu,mara nyingi tunapenda kuanzia eka tano na kuendelea,sio ubaguzi,kwa sababu ni hasara kwako kutoka Dsm kwenda kuangalia miti yako 100 Dodoma. Karibu mkuu.
 
Mkuu Malila tunashukuru sana kwa masomo unayotoa.....please weka vitu hapa hapa mwanangu.........mambo ya pm wengine tutakosa kujua.....please

Poa nitafanya hivyo hapapa uwanjani,kumbe na wewe unapenda sio.
 
Natoa shukrani kwa wachangiaji wote, mawazo mazuri na yamenipa somo zuri. Special thanks to Malila, Mbu asante kwa kuazisha thread hii.
 
thread poa sana hii. shukurani kwa wote wauliza maswali na watoa darasa.
 
Ipitieni na hii thread ina mawazo mazuri sana ya biashara
 
Source ya mtaji wako ni muhimu pia.....naturally kama umeipata kwa mkopo lazima huyo aliyekukopesha ulimuuzia business idea na kama ni hivo hakuna haja ya ushauri......kama ni urithi,zawadi,msaada,hongo,rushwa,10% nk nakusahuri weka kwanza katika fixed deposit for 3 months ukune bongo otherwise utapata zaidi ya 10m confusing ideas....
 
Its a very useful thread ever!
Thanks brother Mbu and Malila.
 
DECI
Panda sasa baada ya miezi minne tuu unavuna
Mkora kweli sijaipenda reply yako, samahani kama nitakukera kama ulivyonikera kwa reply yako mwenzako kaomba ushauri kama huna piga kimya....
 
ushauri wangu ni kusambaza hizo pesa kwenye investment ndogondogo...........mfano
1.BIASHARA YA KUUZA GAS MFANO ORYX AND OTHERS
2.SHARES KIDOGO HASA KWENYE KAMPUNI AMBAZO ZINA FAIDA KAMA SIMBA(TANGA CEMENT)........NA TCC
3.KILIMO KWANZA.........
 
Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;

1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.

Leo niwape item ya tatu tu,mimi nimeajiriwa,najaribu kutumia muda wa mwajiri kwa uangalifu.
Kuna miti mingi ila kwa sisi mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25),
pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda mwakani. Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro,Iringa,Arusha,Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6000/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi,lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 500/ ya chini na 2000/ ya juu pale dar.

Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 18,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao. Mlingoti kilo moja ni Tsh 22,500/ na unapata miche 120,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200.

Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1200,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 15,000/shambani.kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 70,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1200 x 15,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia.

Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi. Nimetoa kwa ufupi sana, ila tutaendelea kuelezana kidogo kidogo, item nyingine kesho.

naomba niibue hii post tena, ili ambao waliimisi waweze kuchangia!!
 
ni kweli kabisa abdul,,,mambo mengi ni kama sarafu yaani yana pande mbili,kwa hiyo ni vyema kuelezea pande zote mbili,ili kuwa salama zaidi.
 
Mie naona Mbu uwekeze kwenye mfumo wa maji safi kule bongo, nenda sehemu ambazo hawana maji ya bomba na ukachimbe visima vya kutumia mota ya umeme ili wapate maji safi badala ya kuchota maji kwenye madimbwi. Hiyo pesa unaweza kuchimba visima 5, hapo utasaidia wananchi wenzako. Unaweza kurudisha pesa yako, iwapo utafanya kila ndoo ya maji ni shs 100.

Maji ya chumvi atamuuzia nani!
Biashara ambazo ni stable na inalipa mda mfupi kanunue mazao vijijini mfano kahawa au mahindi mpunga nk suburi mda ambao bei ime double 3 month uza! Minimum Risk! Ila mwaka huu umeshachelewa!
 
Ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa Bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.
hahaha...naona watu wanaomba feedback hapa
 
...where is MBU? Please lete feedback has been long since you collected the advice from here......!

Mkuu....Marandu...! nakuona hapo chini, hapa ndio mahali sahihi kwa maswali yako meeeeeengiiiii......!
 
kaka ulishawahi kufanya biashara ya kusafiri?kama bado na uko interested kuna biashara ya mbao ngumu toka mozambique inaweza kukulipa kama uko tayari send an email to; akamanyusi@yahoo.com nitakupa contact za watu ambao watakushika mkono kwenda huko.ni biashara inayotakiwa self comitment sio utume mtu uende mwenyewe ununue mzigo na upakie mpaka bongo soko la mbao ngumu hapa si la kuumiza kichwa unaweza uza jumla au ukapanga mahali kijiwe
 
Mkuu Mbu, Malila na wengine waliochangia.,
Ni kweli hii thread naona its the hottest kwenye JF.
Namshukuru Malila kwa kuwa muwazi kinyume na wengi wetu. Na la maana zaidi ni kuwa tayari kuwa mshauri" mentor "wa wana JF wote bila gharama.
Mbu biashara ziko nyingi lakini shidkubwa kwa Tanzania mara nyingi lazima uangalie biashara amabayo usumbufu(wa kweli na uongo) ni mdogo.
Wengi wamezungumzia biashara hii inafaa,ile inafaa lakini hamna ambaye alikuwa anaeleza kuwa mimi nafanya biashara hii kwa hiyo niko tayari kutoa information yote na kujibu matatizo yote.
Wengi hawataki kufanya hivyo kwa sababu biashara wanazofanya wakizisema hapa maswali yatakuwa mengi, utakuta wana maswali ya kuijibu TRA,Police etc.
Biashara ya n'gombe naona kama kuna mambo mengi hayakuzungumziwa especially kwenye matatizo.
Mkuu Malila kwa wenye uwezo chini ya uwezo wa Mbu tuanze na kiasi gani kwa ushauri wako?Kama nina 2.5Million TZSh naweza kuingia ukulima/biashara hii kwa Mafinga na maeneo ya karibu?
 
Back
Top Bottom