Usimwigize mwenzio Jehannam... RIBA ya aina yoyote ni haram soma hapa... nimeweka hii maana sijui wewe ni dini gani ila kama wewe ni muislam kama mimi basi huu ndio usia wangu kwako... Ya Allah nimewasilisha
RIBA NI DHAMBI KUBWA; YAINGIZA MOTONI
Katika Qur'ani Mola amesema :
( الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لاَ يَقُومُونَ إِلاَّ كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُواْ إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىَ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ😉
"Wale wanaokula riba hawasimami ila kama anavyosimama aliye pandwa na Shet'ani kwa wazimu. Hayo ni kwa kuwa wamesema: ‘Biashara ni kama riba tu', wakati Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. Hivyo aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake akaacha [kula riba], basi ni chake kilichotangulia, na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Ama wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu" (Albaqara, aya-275)
Wenye ilmu wanasema aya inatupa taswira ya wanaokula riba watapokuwa wanatoka makaburini mwao siku ya kiyama ya kwamba watakuwa wakitapatapa, wanasimama wakianguka kama mtu aliyeingiwa na shetani.
MLA RIBA HAWI MUUMINI :
Mwenyezi Mungu amebainisha kuwa kula riba na imani hayakubaliani:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ😉
"Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni kilichobaki katika riba, ikiwa nyinyi ni Waumini" (Albaqara, aya-278)
Kwa hivyo ikiwa sisi ni waumini kweli basi tumche¹ Mwenyezi Mungu na tuache riba.
SIYEACHA RIBA KATANGAZIWA VITA NA MWENYEZI MUNGU :
Mwenyezi Mungu amesema baada ya aya iliyotangulia:
.( فَإِن لَّمْ تَفْعَلُواْ فَأْذَنُواْ بِحَرْبٍ مِّنَ اللّهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُؤُوسُ أَمْوَالِكُمْ لاَ تَظْلِمُونَ وَلاَ تُظْلَمُونَ😉
"Na kama hamtafanya [hivyo], basi jueni kwamba mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe" (Albaqara, aya-279)
Vita vya Mwenyezi Mungu si vya risasi au mabomu, lakini vita vya Mwenyezi Mungu hapana mtu ambaye anaweza kuvikimbia. Miongoni mwa vita vya Mwenyezi Mungu ni kupatwa na maafa mengi kama vile dhiki au mtu kutokuwa na raha katika maisha yake hata akiwa na mali nyingi. Kwani Mwenyezi Mungu huondoa baraka katika mali ya riba::
(يَمْحَقُ اللّهُ الْرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ😉…
"Mwenyezi Mungu huifutia baraka [mali ya] riba, na huzibariki [mali zinazotolewa] sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukana [amri Zake], mtenda dhambi" (Albaqara, aya-276)
Huwenda ukamuona mtu masikini lakini akawa yumo katika furaha kuliko huyo anayekula riba. Sababu ya huyu kuwemo katika furaha ni ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyoahidi ya kuwa Mu'umini yeyote atakaetenda mema (mke au mume) basi atamhuisha maisha mazuri na atamlipa malipo mazuri akhera:
(مَنْ عَمِلَ صَالِحاً مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ😉
"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda" (An Nah'l, aya-97)
Lakini atakae pinga amri za Mwenyezi Mungu basi atakuwa na dhiki hapa duniani na siku ya kiyama atafufuliwa kipofu:
(وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُه يَوْمَ الْقِيَامَةِأَعْمَى😉
"Na atakayeacha kufuata mawaidha yangu, basi kwa yakini atakuwa na maisha ya dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu" (Ta'ha, aya-124).
Bila ya shaka hapana mtu aliye tayari kufufuliwa kipofu, kisha aingizwe motoni. Kwa hivyo hapana budi ila tuyapokee mawaidha ya Mola wetu.