Unachosema ni Kweli Mkuu binafsi niliingia m3 kwenu kilimo mwishowe nkapata m2.174 na ikataka kuniachanisha na wife coz ilinikataza kabisa hizo mambo.
Hiki ndio kizazi cha watanzani cha Sasa,yaani we mkeo ndio ana ku remote?
Huu utani sasa
Naendelea kusema kama umeamua Kufanya kiliomo kwa Kuiga hapo ndio utapotea,ila kama umefanya Kilimo kama maisha hapo utatoka.Tatizo watu wanataka kwamba akiingia kwenye kilimo basi mwaka huohuo atusue.
Kuna watu wanapoteza robo tatu ya mtaji waote,ila wanarudi tena na kiasi kilichobakia kufunika maeneow alioteleza.
Wewe mfano una 7m au 5m,hivi unashidwaje kutena 1m kwa ajili ya Consultation kutoka wa Mtaalam wa kilimo?
Tatizo letu tunabahitisha kulima wa kuulizana wewe unafanyaje,inakuwaje mtaani kwako kuna mama alima matembele na bamia uwani kwake na anapiga bao mtaani watu mnapangana foleni,halafu wewe mwenye mtaji wa kuanzisha kilimo cha kati unaganda kwa kukimbia changamoto.
Lazima kwanza mjue kutofautisha mkulima aliekulia kijijini na mkulima alietokea mjini.Sasa Mkulima alietokea mjini yeye anasimama kama mkulima na mfanyabiashara,ila yule mkulima wakijijini wengi bado wana mentality kwamba lazima wasubirie watu watoke mjini ndio wanunue bidhaa zao.
Naendelea kusema kwamba Kilimo kinalipa sana,na lazima ukubali kwamba pia ni gharama na hakuna kiti kisicho na gharama.
Mie nalima Hoho huku Zanzibar maeneo ya Bweleo na Fuoni,mwaka wa mwanzo zilinipiga kweli,ikabidi nimtafute Mtaalam Dar nimlete Zanzibar afikie home ili anipe ushauri,alichofanya ni kuchukua Sample ya udongo na kurudi Dar kwenye Maabara kisha akaka kuniambia namna ya kuendesha kilimo kulingana na aina ya matokeo yake na aina ya mbolea kubalance hali ilivyo.
Ili ni cost sana hii proccess,lakini kwa vile nilikuwa na dhamira ya kweli na nilijipanga kwa changamoto zoote hizo,ndani ya miaka miwili habari imekuwa nyingine kabisaa.Na kwa vile nipo kwenye Utalii nimetafuta vihotel vyangu kadhaa na supply vizuri sana tu.
Ukiweka kipindi cha mpito cha miaka mitano basi utatoka,ila ukitaka kilimo kikulipe kwa miaka miwili au mitatu hapo utafeli na utakuwa unajidanganya sana.Na wengi tunakimbia changamoto.
Hivi unajua kwamba kuna wafugaji wa kuku wanapoteza mtaji woote?kwa kufa kuku kwa wakati mmoja?Lakini bado wanakomaa mpaka leo ukiwaona nashangaa.
Jitathmini