Hata ufanye kazi vipi,mwisho wa siku mwili unahitaji burudani. Sasa hapo kwenye burudani kila mtu anayo ya kwake, kama ifuatavyo; kuna wapenda mpira, sinema, vinywaji mbalimbali, ngono, safari, utalii sehemu tofauti zikiwemo mbuga za wanyama, muziki, disco, kuogelea, kula, kulala etc...!! Na burudani hizo zina gharama tofauti tofauti. SASA WEWE UNADHANI STAREHE NI WOTE TUPENDE UNAVYOVIPENDA WEWE..!!
Hata starehe yako ikiwa ni savvanah, bado wenzio watatia pesa uliyonunulia savana mfuko, hata upende kwenda mbugani, bado utalipia kuwaona wanyama, utalipa nauli chakula, kulala etc na hivyobado wenzio watatia pesa mfuko. etc kifupi hakuna cha bure. Hivyo kutuambia kuwa .. nanukukuu.. "Wenzenu wanatia pesa mfukoni kwa kuuza ving'amuzi,nyinyi mnaliwa tu na kupiga makele" .. Mwisho wa kunukuu, ni yale yale tu..!!
BTW, hata kama huangalii au huzungumzii kuhusu mpira, kipo kitakachokupa matokea sawasawa na anayezungumzia mpira. Mtatofautiana namna matokeo hayo yanavyowajia..!!
Hii ni sawa na wale wanaowasema wanaokunywa pombe kwamba wakiacha pombe, kwa mwaka mmoja wanaweza kununua gari, WALIPOULIZWA KAMA WAO WANAKUNYWA, WAKASEMA HAPANA, HAWANYWI, WALIPOAMBIWA WAONYESHE MAGARI WALIYOYANUNUA, WAKABAKI KUTOA MACHO TU..!!