YOU ARE MISSING THE POINT..!!
Kwanza nikupinge, kuwa mke na mume wanafanya ngono..!! Jambo ni moja, lakini utaratibu unafanya jambo hilo hilo liitwe haramu au halali. Mke na mume, kwa sababu wamepitia taratibu zote za ndoa, wanafanya tendo la ndoa. Hao hao kama hawajaoana, basi wanafanya ngono, tena wakati mwingine ngono zembe. Na ndiyo maana hakunaga tendo la ndoa zembe..!!
Kuhusu kuangalia mpira na kwenda mbuga za wanyama, the point is, wote mnatoa hela, na wote mnaishia kuburudika. Mind you, hatuendi mpirani kuangalia viduku, bali kile kinachofanywa na hao walionyoa viduku. Hivyo basi tunapokwenda uwanjani kuangalia vijana hatuendi kwa ajili ya viduku na kusuka nywele kwao, bali boli wanalolisambaza uwanjani. kama ni nywele au viduku hata wanaoongoza watalii huko mbugani nao wanavyo hivyo viduku. Hata wauza bar au wahudumu wa mabaa nao wapo wenye viduku na kusuka nywele. Huendi baa kwa ajili ya viduku vyao, bali bia au vinywaji wanavyoukuuzia.