Mtanange wa Klabu Bingwa Afrika: Al Ahly 5 vs Simba SC 0

Mtanange wa Klabu Bingwa Afrika: Al Ahly 5 vs Simba SC 0

Tulia dawa iwaingie mikia nyie mechi mbili goli kumi!!! Mwarabu Jana kajipigia kipindi cha pili akaona acha apige Show game....
Wewe mambo yanayoendelea kwenye michuano ambayo unamiaka 20 unaishia kuyaona kwenye tv yanakuhusu nini...hata tukifungwa mia hayakuhusu..we endelea kujiandaa namechi zenu nasikia leo mnacheza na wakina alikiba
 
.
Hapana siwezi kuwa na mawazo mengi juu ya kupoteza mchezo dhidi ya Al Ahly,, tumefungwa na timu kubwa Afrika
.
Nazani nusu ya wachezaji wangu hapa Simba hawana uwezo wa kucheza soka la kimataifa
.
Ili ufanikiwe katika mashindano haya ya klabu Bingwa Afrika CAF Champions Leagua hatua ya makundi lazima ufanye usajili wa wachezaji wenye uwezo wa kucheza soka la kimataifa sisi tumefeli hapo
.
Huwezi kucheza na timu kama Al Ahly,, huku wachezaji wako nusu nzima ya kikosi hawana uwezo wa kucheza soka la kimataifa na usifungwe lazima Al Ahly,, watakufunga tu.
.
Alisema kocha mkuu wa Simba Sc Patrick Aussems baada ya mchezo wa jana kumalizika. ( Sport BC )
 
ONA MAAJABU HAYA NDANI YA MIAKA 5 ILIYOPITA

Mwaka 2014.
Yanga 1 - 0 Al ahly (Dar)
Al ahly 1 - 0 Yanga (Cairo)
(Al Ahly akashinda 5-4 kwa penati)

Mwaka 2016.
Yanga 0 - 0 Al ahly (Dar)
Al ahly 2 - 1 Yanga (Cairo)

Mechi nne ;-
Al ahly win 2
Yanga win 1
Sare 1

magoli ya kufunga;-
Al ahly 3
Yanga 2

hiyo inamaanisha katika mechi nne Yanga karuhusu goli 3 tu kwa Al Ahly wakati yeye pia akifunga goli mbili.

RECORD YA UNDERDOG.

Al ahly 5 - 0 Mikia SC

yaani magoli aliyofungwa katika mechi yake moja tu ni Sawa na magoli ya timu zote mbili katika mechi NNE walizocheza tena Al Ahly waliwapumzisha Key Players wao 8 , walimaliza mchezo first half hawakutaka kumaliza nguvu zao kwa Mbumbumbu. . Endapo wangeuwasha moto dk 90 basi underdog wangevunja rekodi ya Club African.

TUNAVYOITWA WA KIMATAIFA TAMBUENI SIO KAZI RAHISI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa nadhani mnaanza kuelewa....mtu anawaambia watu na akili zaokuwa Simba ni awa na Barcelona...halafu baadaye anakuja sema alikuwa anahamasisha kwamba ukiwaambia simba ni sawa na Barcelona eti Simba wanahamasika kuja uwanjani...What a shame!!! Yaani viongozi gani wa mpira tunao nchini?? Yaani kiongozi anapiga domo sawa na comedy na Simba eti wanaona kuwa eti huyo anafaa....Na bado huyo Saoura kule Algeria atapiga mtu 7-0 kwahasira...hakutakuwa na magoli ya offsde ya Kagere kule....
Aden Rage hakukosea kuwaita mbumbumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzetu Yanga miaka 5 mfululizo hawajawahi kukanyaga makundi ya klabu bingwa, Simba tumekanyaga sio jambo dogo.
Tukubali makosa yetu, huku tukiwa tumepata fundisho la usajiri bora na sio kuokota wachezaji.
Tupange mikakati ya kupata point home game kundi liko open bado.
 
Nanyie kesho mnacheza na kina alikiba...jiandaeni na mechi zenu hili kombe la africa linawahusu nini wakati mnamiaka 20 mnalisikia tu kwenye radio
Mngelijua hilo basi mwaka jana msingetupigia kelele tulipofungwa ,wakati tukiwa kwenye hatua ya makundi michuano ya shirikisho CAF na bado tarehe 12 feb tena kwa mchina .
 
kwenye dirisha dogo tuliwashauri kumsajiri kakolanya wakafikiri labda tunawapelekea 'jeshi'
 
Simba wachezaji wao professional wana viwango vibovu sana...Bora wangecheza watanzania watupu wapate exposure....
 
Hakuna siku timu yoyote ya Tanzania inaweza ikaidharau timu ya Misri, hii nadharia sio kweli hata kidogo kwani siku zote mpira wetu ni mdogo sana kwa ule wa Egypt.

Waarabu baada ya kupata magoli matano ktk kipindi cha kwanza hawakuwa tena na pressure ktk kipindi cha pili hivyo walichokuwa wakifanya ni kulinda ushindi wao kwani waliishamaliza biashara.

Simba warudi darasani uwezo wao ni mdogo sana kuweza ku-make impact yoyote kwenye mashindano haya.
 
Kila anayeenda anaenda kutia aibu tu,hivi hakuna uwezekano tukaacha kushiriki hata kwa miaka mitatu kisha tukapeleka timu ya ushindani!!.
ila ndo vizuri tupigwe pigwe tukishaacha mpira wa kiingereza/maneno mengi,at least tutafika mbali.Washapigwa 5 na pengine hakuna mpango wowote wa kudhibiti yasijirudie...Japo upande mwingine ni furaha yangu kuona wanapigwa japo wiki tena.
 
Back
Top Bottom