Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Tanzania kuna tatizo kubwa la maarifa,hata miradi inayoanzishwa na vijana wengi wa ndani ni ile ya kutaka kutambiana na watu wa mtaani au tuliosoma nao,hatuanzishi vitu kwa ajili ya kuitawala Afrika Mashariki au Kusini mwa Afrika kibiashara au kiubunifu,

Kenya na sasa Rwanda wanafanya vitu si tu kwa ajili ya kutambiana bali kuifanya Afrika kuwajua wao ni watu wanaotumia akili zao vizuri,

Sisi tumebaki kuzungumzia Mpira masaa 24 km wapumbavu,wale wauza uchi wakina Mobeto na Paula ndio tunaona watu wa kuigwa,katika jukwaa la biashara na fursa kaangalieni nyuzi ngapi za maana huwa hazipati wachangiaji lakini ukiweka nyuzi za kisengerema wabongolala wanavyokulupuka kuchangia,

Tubadilikeni wakuu,tuitazame sekta ya madini na kilimo kwa jicho la pili,sekta hizi zinaweza kuwabidilisha vijana wengi wakaishi ndoto zao hapa hapa Bongo bila ya kwenda kuteseka huko ughaibuni km sisi tulivofanya miaka hiyo
 
Mkuu ulichoandika kina ukweli fulani, ndiomaana mimi kuna post hapo juu nimeandika kuwa watanzania tuna laana fulani hivi ambayo wenyewe hatuijui.
Mwezi uliyopita niliona video flani ya mkuu wa polisi mkoa wa Dodoma akiwaasa wazazi wa mkoa huo kuwalea vizuri watoto wao baada ya vijana wengi kujiingiza katika makundi mabovu ya kihalifu. Kamanda huyo alisema kwamba viwanda na mashamba mengi yaliyopo huko yamejaa warundi na wanyarwanda baada ya wazawa kushindwa kufanya kazi katika mashamba na viwanda hivyo.

Kamanda anasema ikitokea baadhi ya wazawa kujitahidi kufanya kazi basi siku akipokea mshahara wake harudi kazini mpaka siku hela zitapoisha 🤣🤣🤣
 
Watanzania walioko South Africa ni watu walio tofauti Sana ki matabaka, Kuna Ma Professor wanafundisha vyuo vikuu...UWC, UCT nk,Kuna watu wameajiriwa katika makampuni makubwa,Ma Engineer,Kuna watu wataalamu WA kuchimba Mafuta kwenye ma Oil rigs baharini,Kuna ma manager WA SuperMarkets,Na Mameneja was Mahotel Na Restaurants halafu Kuna walio wengi Zaidi hawana ujuzi wowote,wakiulizwa Sasa umekuja kufanya nini,majibu....nasubiri Meli,Kazi yoyote hawawezi kufanya,wanaishia kutafuta opportunities Za kufanya uhalifu wowote wakimbie hapo ndipo matatizo yanapoanza.....Sasa haiwezekani watanzania wote walioko South Africa,wakajumuika pamoja eti wakajadili mambo ya maendeleo,Maprofessional niliowataja hapo wanajumuika pamoja Na kujadili mambo Kadha WA kadhaa ya maendeleo, mikutano mingi ikifanyika University of Western Cape, UCT ni ambapo vijana Walala nje,Ma beach boy wanaogopa Hata kufika....
Sasa Ushauri Tu ni kwamba kabla hujasafiri lazima ujue unakuja kufanya nini....
 
Asante mkuu kwa ushauri. Najua ni vigumu kwa watanzania wengi kutuelewa, lakini sio mbaya tukitoa angalizo kama hili ili wale wenye akili waweze kufuata ushauri wetu kabla ya kuchukua maamuzi.
 
Dunia ya leo ambapo kuna VETA NA SIDO, kijana jnatakiwa uchangamkie fani kwanza upewe kijicheti chako, kwanza ujifunze kupaka rangi magari na ujue kweli, ukajifunze kushona nguo kama una nia miaka miwili ushajua kabisa, ujenzi wa majumba na decoration tena kisasa kabisa, ufundi wa magari hapa nenda garage za mtaani piga spana za kutosha veta katafute cheti tu, ukiwa na fani amini utakakoenda lazima utapata sehemu ya kuanzia, hasa unaenda nchi za watu hauna ujuzi wowote unawaza ukauze drugs mimi nakuona ni mwehu tu hata ukiuliwa naandika RIP napita kushoto
 
Small fish kwenye small pond......
Anataka kuonekana mkubwa baharini.

Kama Bongo hii huwezi kumudu maisha yako ( hujui hata ukiamka kesho unaenda wapi kufanya nini).
Usiende Kwenye Nchi za kibepari, utaishia kula shaba tu.
Waoga wa maisha nyinyi wabongo, mmeshazoea, kesho nitaponea kwa shemeji, kesho kutwa kwa mjomba
Mkishakula mmeshiba tumbo ndiii, mnaridhika na ratiba, saa ngapi utafikiria kujikomboa
Hao wacha wafe, ni mabingwa wamejikomboa kwenye ratiba yako, ya kusarandia ndugu na washkaji upone siku iende
 
Ila ukweli wangu broh siwezi kwenda SA kufanya kibarua cha mashambani au kuvua fish......

I rather be a misheni town ila siyo kuuza ngada na vitu vya wizi....kwani nikiuza nguo na viatu siwezi toboa, jibu ni kuwa nitatoboa chap tu.
Tatizo vijana wa bongo wanataka kuwa mabeach boy na usuper star wa kishamba...wakati kwao bongo mama analia njaa.
 
Elimu huna....
Ujuzi huna.....
Huna ramani yoyote.
Unadhani hivi vyote vitapatikana ukifika south?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…