Kama unajua concept ya
universal jurisdiction, usingeweza kuandika hapa mambo ya
"vicalicious liability"- acha kuchanganya madesa, ndio maana tunapigwa huko nje na habari za mikataba kwa kuchanganya mambo.
Yafaa ujue ni nini maana ya
Universal jurisdiction: The principle of universal jurisdiction provides for a state’s jurisdiction over crimes against international law even when the crimes did not occur on that state's territory, and neither the victim nor perpetrator is a national of that state. The principle allows national courts in third countries to address international crimes occurring abroad, to hold perpetrators criminally liable, and to prevent impunity.
Kama mahakama zetu zimeshindwa, kesi hii ya Lissu yaweza kutumia hiyo principle na mambo yakaendelea kama walivyo mfanyia Milocevic na Charles taylor.
Na kuhusu Vicarious liability: is a legal principle that holds one party responsible for the actions of another party. It's often used in the context of employer-employee relationships, but can also apply to other contractual relationships.
Bilateral investment treaty (BIT): Hizi zinasaidia sana katika ku- enforce awards katika ISDS cases- Hakuna hata moja (ya hizi BiT -popote pale duniani humu) inayosema kwamba makampuni ya nje yatakingiwa kifua na serikali za nchi zao kwa kwa kufanya
illegal acts- rejea kesi ya Tuna Bond - Msumbiji- ambapo kampuni moja lilikuwa linatoa mikopo kwa serikali na wananchi wanalipa mikopo hiyo, baada tu ya serikali kubadirika , kesi ikaaenda mahakamani huko huko London na kampuni likaamuliwa kuilipa serikali billions, ( Soma hapa:
Mozambique wins court claim over corrupt Tuna Bonds - Spotlight on Corruption) Pia Rejea ni kwa nini serikali ya uingereza haikuikingia kifua BAE systens kuhusu yale mambo ya rada wakati Chenge...BAE Systems ilishitakiwa kwa kukiuka sheria na Tanzania ikarudishwa change ya rada, soma hapa:
BAE criticised by UK MPs over Tanzania corruption . Kwa maana nyingine faini waliyopigwa ilizidi bei ya ra radar, Tanzania ni kama ilipewa bule hiyo kitu.
Nacho taka kusema nini? kama Tigo amehusika kwa namna yeyote ile - doctrine ya
occupiers liability inamuhusu na huyo
Tigo- hawezi kuchomoka... parent company ni la UK, mtoto wake yuko Tanzania, kafanya majambozi ya kutapanya data za watu bila idhini yao- lazima baba/mama yake ahenyeshwe...Sheria za UK zina yang'ata sana makampuni yao ndio maana huyo bwana kakimbilia kwao kuwashitaki kwa kutumia kinga ya whistleblowers-
Ujinga walioufanya Tigo sasa utamfanya Lissu kuwa Billionea kwa masihara yao ya kugawa metadata za mtumiaji wa simu ( Lissu- Bila idhini yake). They should have known better.