Mtazamo: Imani ya wananchi kwa Serikali imeshuka tangu Dkt. Magufuli atutoke

Mtazamo: Imani ya wananchi kwa Serikali imeshuka tangu Dkt. Magufuli atutoke

Ukweli ni kuwa kama ndani ya uongozi wa CCM, kungekuwa na watu wenye uzalendo kama kule Singapore, wangefika mahali na kutamka kuwa, miongoni kwetu hakuna mwenye uwezo wa kuifikisha nchi pale tunapotaka. Wangesema, tumtafute mtu mwenye uwezo, nje ya chama, tumshawishi akubali kuongoza nchi. Ndani ya CCM, watu wamefikia uwezo wa mwisho. Hakuna jipya litakalopatikana.

Kule Singapore wananchi hawachagui mtu bali wanachagua chama. Halafu chama kilichoshinda kinaenda kumteua waziri mkuu. Siku za huko nyuma, chama ambacho kilishinda, walikaa miezi miwili bila ya kumpata waziri mkuu. Baadaye, walifikia uamuzi kuwa ndani ya chama chao hakukuwa na mtu wa kuiongoza Singapore ifike mahali wanapotaka. Wakaenda kumshawishi mfanyabiashara aliyekuwa na mafanikio makubwa ajiunge na chama chao, halafu awe waziri mkuu. Naye aliwapa masharti, mkitaka niwe waziri mkuu mkubali niiongoze nchi kama kampuni yenye kutengeneza faida na siyo kama taasisi ya ukiritimba wa serikali. Wakakubali. Huyo ndiye aliyeleta mafanikio makubwa ya nchi kwa kiasi cha kushangaza.

Hakika, hawa waliopo sasa, tutabakia hivi hivi. Tutabakia na hizi siasa za kishabiki lakini nchi itaendelea kuning'inia kama ilivyo sasa. Na sisi sote tutahukumiwa. Muumba atasema, niliwapeni kila kitu kwa nini mliishi maisha ya jehanamu. Hakutakuwa na la kujitetea. Kusema oh ilikuwa CCM, Samia au Magufuli, haitasaidia. Swali la msingi ni, wewe ulifanya nini?

Nchi maskini zinahitaji super intelligent and visionary leaders, kuliko mataifa yaliyoendelea, ambayo mifumo ya kiutawala ipo imara.
 
Wananchi wakisikia kuna Tril 1.3 zimekopwa kwa ajili ya kuchochea mdororo wa uchumi ulioletwa na Uviko -19, wanahisi kupigwa tu. Wanajua kuna kizingumkuti namna zitavyotumika.

Umeme umekuwa ni tatizo la kukatika katika kila mara, wanahisi, kuna mchongo wa kupigwa kama walivypopigwa huko nyuma kupitia Escrow na Richmond

Teuzi za mawaziri zikifanyika, wanajua kuna safu ya mawaziri inapangwa ili kulikamua taifa, maana wanaoteuliwa wananukia ufisadi.

Waziri mwenye dhamana ya Biashara anakanusha hadharani kuwa hakuna mkataba au maelewano juu ya uzinduzi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili hali uzinduzi wa ujenzi ulifanyika.

Ni muda mfupi sana serikali iliyopo madarakani imepoteza imani kwa wananchi.

Kwani hao wananchi walikuwa na imani na serikali ya Magufuli, au walikuwa wanaogopa kusema wasije wakatekwa na kuuwawa?
 
Kabisa, bora umesema, hawa mitume wa Magufuli wanataka kuja kupotosha humu ili ionekane watu walikuwa na imani na mwendakuzimu.
kiujumla wananchi hawajawahi kuwa na imani na serikali ya chama cha mapinduzi msitake kumwangushia jumba bovu huyu mama ili ionekane huyu mwendazake kafanya cha maana
 
Back
Top Bottom