Ukweli ni kuwa kama ndani ya uongozi wa CCM, kungekuwa na watu wenye uzalendo kama kule Singapore, wangefika mahali na kutamka kuwa, miongoni kwetu hakuna mwenye uwezo wa kuifikisha nchi pale tunapotaka. Wangesema, tumtafute mtu mwenye uwezo, nje ya chama, tumshawishi akubali kuongoza nchi. Ndani ya CCM, watu wamefikia uwezo wa mwisho. Hakuna jipya litakalopatikana.
Kule Singapore wananchi hawachagui mtu bali wanachagua chama. Halafu chama kilichoshinda kinaenda kumteua waziri mkuu. Siku za huko nyuma, chama ambacho kilishinda, walikaa miezi miwili bila ya kumpata waziri mkuu. Baadaye, walifikia uamuzi kuwa ndani ya chama chao hakukuwa na mtu wa kuiongoza Singapore ifike mahali wanapotaka. Wakaenda kumshawishi mfanyabiashara aliyekuwa na mafanikio makubwa ajiunge na chama chao, halafu awe waziri mkuu. Naye aliwapa masharti, mkitaka niwe waziri mkuu mkubali niiongoze nchi kama kampuni yenye kutengeneza faida na siyo kama taasisi ya ukiritimba wa serikali. Wakakubali. Huyo ndiye aliyeleta mafanikio makubwa ya nchi kwa kiasi cha kushangaza.
Hakika, hawa waliopo sasa, tutabakia hivi hivi. Tutabakia na hizi siasa za kishabiki lakini nchi itaendelea kuning'inia kama ilivyo sasa. Na sisi sote tutahukumiwa. Muumba atasema, niliwapeni kila kitu kwa nini mliishi maisha ya jehanamu. Hakutakuwa na la kujitetea. Kusema oh ilikuwa CCM, Samia au Magufuli, haitasaidia. Swali la msingi ni, wewe ulifanya nini?
Nchi maskini zinahitaji super intelligent and visionary leaders, kuliko mataifa yaliyoendelea, ambayo mifumo ya kiutawala ipo imara.