Mtazamo korofi: Mwanamume kufuatilia tamthilia naona kama haijakaa sawa hivi

Mtazamo korofi: Mwanamume kufuatilia tamthilia naona kama haijakaa sawa hivi

Mkuu unazungumzia tamthilia gani? Maana kuna tamthilia zenye action ndani yake ila ikiwa ni full drama kwakweli haijakaa sawa
Mwanaume unatakiwa utazame movie za vita mtu anamwagwa utumbo, mwingne anakatwa kichwa afu mkataji analamba damu.
Movie kama escape plan au escape room ndio za wanaume.
 
Naona vijana wamehamaki kweli kweli....ni mtazamo kama unafuatilia freshi Tu...
1002319002.jpg
 
Na vipi kufuatilia maisha na taste za mwingine hio imekaa sawa ? (Sio kwa mwanaume tu hata Mwanamke)...
To each his/her own...; By the way tamthilia ni nini ? Naweza kusema hata hizi siasa za majitaka zinazoendelea ni Tamthilia...

 
Habari za muda huu waungwana.

Hili jambo limekuwa likitatizo sana fikra zangu kila nikiona mtoto wa kiume ameketi na kufuatilia tamthilia moja kwa moja na kila episode huwa namuwazia vibaya sana.

Mimi naona kama vile hili jambo halipo ki-musculine hivi. Kwa mwanaume limekaa sana kidada na kimama mama hivi.

Hebu fikria Baba wa familia unagombea rimoti na watoto au mkeo kwa ajili ya tamthilia.

Mimi naona kama haijakaa sawa. Sijui nyinyi wenzangu maana kila mtu na mtazamo wake.
Hivi prison break ni tamthilia?
 
Kwanza huo muda wa kuangalia TV Mwanaume anatoa wapi jamani,unatoka kazini unafika sa 1 au 2.Ukiangalia kitarifa cha habari usingizi unaanza hapo hapo kwenye kochi.
 
hizi action series zenye mabunduki na mapanga ni za wanawake pekee kuangalia? Au labda utupe tofauti kati ya series na tamthilia.
Nadhani inaeleweka vitu ambavyo ni MASCULINE.....hasa hzo actions movie...nadhani kuna mdau hapa juu ametanabaisha vyema....
 
Nadhani inaeleweka vitu ambavyo ni MASCULINE.....hasa hzo actions movie...nadhani kuna mdau hapa juu ametanabaisha vyema....
ZIpo tamthilia ambazo ni Masculine pia.
Labda ungespecify aina ya tamthilia ambazo hazifai kwa mwànaume.
MImi najua tamthilia ndo hizo hizo series..ni suala la lugha tu.
 
ZIpo tamthilia ambazo ni Masculine pia.
Labda ungespecify aina ya tamthilia ambazo hazifai kwa mwànaume.
MImi najua tamthilia ndo hizo hizo series..ni suala la lugha tu.
Basi inawezekana..... pengine mimi sio mjuzi wa kuzitofautisha
 
Hii Tamthilia inayojadiliwa hapa ndio nini huko Daslam?

Mtufahamishe na sisi basi tusiojua hivyo vitu.
 
Last weekend nilienda kumtembelea jamaa kwake, ilipofika mida nane nusu mchana akanambia tuhamie sebuleni maana kuna marudio ya tamthilia zake anazofuatilia.
Na mwamba aliwabadilishia watoto cartoon ili aangalie tamthilia za kina Gambo😂😂😂.

Japo ni tv yake na nyumba yake ila nilimuona bonge la kituko😂😂😂
Si ndo burudani, na anafata ratiba kabisa watoto wamepiga katuni yeye anaanza saa 8 na nusu
 
Mwanaume akiangalia tamthilia inakiwaje labda,nguvu za kiume zinapungua au zinamuondolea uanaume wake?
 
Back
Top Bottom