Mtazamo korofi: Mwanamume kufuatilia tamthilia naona kama haijakaa sawa hivi

Mkuu unazungumzia tamthilia gani? Maana kuna tamthilia zenye action ndani yake ila ikiwa ni full drama kwakweli haijakaa sawa
Mwanaume unatakiwa utazame movie za vita mtu anamwagwa utumbo, mwingne anakatwa kichwa afu mkataji analamba damu.
Movie kama escape plan au escape room ndio za wanaume.
 
Naona vijana wamehamaki kweli kweli....ni mtazamo kama unafuatilia freshi Tu...
 
Na vipi kufuatilia maisha na taste za mwingine hio imekaa sawa ? (Sio kwa mwanaume tu hata Mwanamke)...
To each his/her own...; By the way tamthilia ni nini ? Naweza kusema hata hizi siasa za majitaka zinazoendelea ni Tamthilia...

 
Hivi prison break ni tamthilia?
 
Kwanza huo muda wa kuangalia TV Mwanaume anatoa wapi jamani,unatoka kazini unafika sa 1 au 2.Ukiangalia kitarifa cha habari usingizi unaanza hapo hapo kwenye kochi.
 
hizi action series zenye mabunduki na mapanga ni za wanawake pekee kuangalia? Au labda utupe tofauti kati ya series na tamthilia.
Nadhani inaeleweka vitu ambavyo ni MASCULINE.....hasa hzo actions movie...nadhani kuna mdau hapa juu ametanabaisha vyema....
 
Nadhani inaeleweka vitu ambavyo ni MASCULINE.....hasa hzo actions movie...nadhani kuna mdau hapa juu ametanabaisha vyema....
ZIpo tamthilia ambazo ni Masculine pia.
Labda ungespecify aina ya tamthilia ambazo hazifai kwa mwànaume.
MImi najua tamthilia ndo hizo hizo series..ni suala la lugha tu.
 
ZIpo tamthilia ambazo ni Masculine pia.
Labda ungespecify aina ya tamthilia ambazo hazifai kwa mwànaume.
MImi najua tamthilia ndo hizo hizo series..ni suala la lugha tu.
Basi inawezekana..... pengine mimi sio mjuzi wa kuzitofautisha
 
Hii Tamthilia inayojadiliwa hapa ndio nini huko Daslam?

Mtufahamishe na sisi basi tusiojua hivyo vitu.
 
Si ndo burudani, na anafata ratiba kabisa watoto wamepiga katuni yeye anaanza saa 8 na nusu
 
Mwanaume akiangalia tamthilia inakiwaje labda,nguvu za kiume zinapungua au zinamuondolea uanaume wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…