Mtazamo korofi: Mwanamume kufuatilia tamthilia naona kama haijakaa sawa hivi

Mtazamo korofi: Mwanamume kufuatilia tamthilia naona kama haijakaa sawa hivi

Kugombea remote na mtoto au mke wako sio sawa kabisa. Maisha sasa hivi yamekua tofauti sana na zamani, TV imekua kitu kidogo sana na cha kawaida, hivyo baba mwenye kupenda kuangalia tv sio mbaya ukaweka tv yako chumbani kuangalia vipindi vyako unavyotaka kwa muda utakao taka.

Ila pia maisha ni mafupi mno kujinyima kufurahia kile kitu roho yako inapenda as long as haumkosei Mungu au kuvunja shera za nchi. Ingawa kweli kuna zile soap opera unaona kabisa hizi, acha wife, house grl na watoto waziangalie tu. Ila zipo zingine za mission na za kibabe pia. So ni kuchagua, ila pia privacy muhimu, maana siwezi angalia series kama game of thrones na watoto sebuleni.
 
Ukweli mtupu, kuna vitu vipo kike kike Sana! Tamthilia za kiswahili,za kutafsiri za Azam, comedies za kina joti, na upuuzi mwingine,
Mwanaume fatilia siasa, uchumi, au, movie za kibabe, Den of thieves, Night has fallen!
Bora niangalie katuni kuliko tamthilia za bongo na vichekesho vya kinajoti vyenye kuamasisha uchoko wa mwanaume kujigeuza mwanamke
 
Na kweli naishi maisha yangu mkuu....lakini hili ni jukwaa huru kutoa maoni na mtazamo
Raha ya family penda anachopenda mke wako na yeye apende unachopenda. Akiwa anapenda tamthlia na wewe umekaa naye unampa support mnafurahi pamoja ni kitu kizuri sana na yeye akiona unatizama mpira akakaa na wewe na kukuchemsha na ushabiki ni kitu kizuri sana. Haya ndio mapenzi vitu vidogo lakini vinajenga vitu vikubwa.
 
Kama hakuna sheria ya Mungu na ya jamhuri iliyovunjwa hakuna tatizo. Nadhani kuna janga kubwa sana la wanaume kutojiamini kwa miaka hii. Yaani mleta mada unaogopa kutazama tamthlia kwa kudhani utapoteza uanaume wako? Hapo kimoyomoyo unataka kutazama ila unachotaka hapa ni kupata approval ya wanaJF. Hii sio sawa. Mwanaume jiamini.
 
Wazee as long as unaenjoy we endelea usikubali boya flani mtandaoni akupangie maisha yako . Haya maisha NI mafupi Sana
 
Humu JF kuna tamthilia kibao. Kwa hiyo unataka kusema jinsia ya kiume iachane na hizi arosto?!! 🤔
 
Kweli Wanaume wa DSM tunaonewa

~Tunapigwa vita kula Chipsi

~Tumepigwa vita kuoshwa miguu na Kucha tukienda Saluni

~Sasa hadi Kuangalia Tamthiliya tumeanza kukatazwa

Kwani hatuwezi kumlipa Kibatala atutetee 😜🙌
NImeipenda hii mzee wa hovyo

Wasituchagulie mambo katika maisha yetu

Mimi naangalia Evermore azam two na Alparsalan,kama kuna mwenye shida na hilo pm iko wazi
 
Habari za muda huu waungwana.

Hili jambo limekuwa likitatizo sana fikra zangu kila nikiona mtoto wa kiume ameketi na kufuatilia tamthilia moja kwa moja na kila episode huwa namuwazia vibaya sana.

Mimi naona kama vile hili jambo halipo ki-musculine hivi. Kwa mwanaume limekaa sana kidada na kimama mama hivi.

Hebu fikria Baba wa familia unagombea rimoti na watoto au mkeo kwa ajili ya tamthilia.

Mimi naona kama haijakaa sawa. Sijui nyinyi wenzangu maana kila mtu na mtazamo wake.
Judgemental behaviour
 
Ni umri na wakati humuelekeza mwanaume mambo anayopaswa kufanya.Haiwezekani mwanaume akae na wanawake wanatazama tamthilia/series za visa vya mapenzi na visasi hadi ikifikia sehemu ya huzuni wote wanakuwa emotional hadi kububujikwa machozi.Noo!Man,that's not how we do and live it!Na ni vema nyumba/familia akawepo father-figure wa kutoa miongozo sahihi kwa vijana wa kiume.
 
Habari za muda huu waungwana.

Hili jambo limekuwa likitatizo sana fikra zangu kila nikiona mtoto wa kiume ameketi na kufuatilia tamthilia moja kwa moja na kila episode huwa namuwazia vibaya sana.

Mimi naona kama vile hili jambo halipo ki-musculine hivi. Kwa mwanaume limekaa sana kidada na kimama mama hivi.

Hebu fikria Baba wa familia unagombea rimoti na watoto au mkeo kwa ajili ya tamthilia.

Mimi naona kama haijakaa sawa. Sijui nyinyi wenzangu maana kila mtu na mtazamo wake.
Mimi Tamthilia sitizami, ila Movie natizama.
 
Back
Top Bottom