#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Kama ni elimu wangeanza kupewa waficha maradhi, kwa kunawa mikono na kutoshika [emoji102][emoji103] na [emoji105] dunia nzima leo tungekuwa free na Corona kama kweli hiyo ndiyo suluhu!

Mwana wa mfalme naye alipuuzia haya? Na sasa ni Malkia naye alipuuzia haya? Makamu wa Rais Bukinafaso naye alipuuzia haya?

Kwa nn hamtaki kuchukua hatua dhabiti dhidi ya corona? Nia ni kuokoa au kuangamiza?

Kwa miundo mbinu ya Tanzania kweli madaktari wataweza kuhudumia wagonjwa ma kumi kwa mamia hata angalau robo ya wale walio Italy na Spain?

Maabara yenyewe iko moja kweli serikali iko imara dhidi ya hili?
JIELIMISHE kuhusu homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya CORONA aina ya COVID-19. Piga 199 au 08001100124

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Farao katoka kumsaidia mjusi kwenye mawe! sasa anakunywa kahawa na kuuliza kwa nini haijazwi maana ni kiduchu! Ajabu sana kwa kweli... Ana K wa WHO ameambiwa ajiudhuru kwa kuto kutilia maanani mambo ya msingi!
Eeh mola wetu, moyo wa Farao ulikuwa sawa na wa jiwe (kama jiwe lina moyo).

Ulitenda mwuujiza akatambua uwepo wako naye Farao akaruhusu busara itawale.

Kwa unyenyekevu tunakuomba hebu ukajidhihirishe wewe na uwepo wako ili mioyo ya viongozi wetu ikaione nia njema iliyopo kwetu sisi waja wako, ili hatimaye busara ikaachwe kuchukua nafasi yake.

Ni wazi kuwa taarifa sahihi zitaakisi dharura na mikakati thabiti ya kuchukua kwa wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni elimu wangeanza kupewa waficha maradhi, kwa kunawa mikono na kutoshika [emoji102][emoji103] na [emoji105] dunia nzima leo tungekuwa free na Corona kama kweli hiyo ndiyo suluhu!

Mwana wa mfalme naye alipuuzia haya? Na sasa ni Malkia naye alipuuzia haya? Makamu wa Rais Bukinafaso naye alipuuzia haya?

Kwa nn hamtaki kuchukua hatua dhabiti dhidi ya corona? Nia ni kuokoa au kuangamiza?

Kwa miundo mbinu ya Tanzania kweli madaktari wataweza kuhudumia wagonjwa ma kumi kwa mamia hata angalau robo ya wale walio Italy na Spain?

Maabara yenyewe iko moja kweli serikali iko imara dhidi ya hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuna pesa za kutosha mkuu
 
Corona imebuma bongo, hamkumsikia Gwajima alivyokuwa anaifukuza?
 
Mkuu umeongea kwa machungu sana,ni wakati muafaka sasa wa raia kuiadhibu serikali tukutu ya CCM kwenye box la kura iwe kwa kumwaga damu au lah haiwezekani kuwa na baba wa familia mwenye kujali pesa kuliko afya za wana familia wake ,no,Mimi naumia sana juu ya hii government uchwara,inayoamini real problems huwa zinasolviwa na imagination ideas kama kumwomba Mungu,shwaini mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi sasa waliopima coronavirus nchi nzima hawazidi 300(Hotuba ya Zitto). WHO wanahimiza njia pekee ya kukabiliana na janga hili kupima na quarantine.Je tumezingatia ushauri huu?
 
Hatuna pesa za kutosha mkuu

Mkuu hatuna pesa za kutosha za kufanyia nini? Pesa mbona tunazo nyingi tu. Hii nchi ni tajiri sana kwa kweli:

1. Angalia Harambee ile ya juzi na Majaliwa zimepatikana zaidi ya 1B kwa muda mfupi tu.
2. Vipi pesa ya ruzuku kwa vyama kwa sasa zikielekezwa huku?
3. Vipi bajeti ya uchaguzi mkuu 2020 ikielekezwa huku?
4. Vipi pesa zote za miradi yote mikubwa zikielekezwa huku?
5.vipi zikiitishwa Harambee zaidi?
6. Nk nk

Kweli tulikuwa hatuwezi kupambana na hali yetu na kujiweka katika hali sawa zaidi kupambana na hili gonjwa?

Taasisi yenye kuheshimika duniani ya Bloomberg na hata WHO wanaonya kuwa Africa na ugonjwa huu tuko wiki 2 hadi 3 kufikia katika hatua mbaya kabisa kuliko ile inayopitiwa na ulaya hivi sasa. Wanazidi kuonya na hata ku mobilize pesa kujaribu kuinusuru Afrika.

Tume funga masikio hatusikii ya azana wala mwazini.

Wakati mataifa mengine hata yaliyo maskini kuliko sisi wakichukua hatua, ati sie tumekumbatia tiba mbadala (maombi). Ati walioambukizwa ni siri tokea katika idadi yao hadi pia katika personalities zao.

Looh! Pole yetu sie. Hakika mficha maradhi na mficha uchi lao mbona moja!
 
Nchi za waastarabu fighting to flatten the curve, waswahili wanaandaa mazingira ya exponential growth.

Mkuu ni aibu sana hasa serikali yenyewe inapokuwa imesheheni wasomi wabobezi na wazamivu kama hii.

Siamini kwa hakika kama ma PhD yote yale na ma profesa wote wale kwa njas za matumbo yao tu wameshindwa kumshauri Dr. Magufuli, daktari wa sayansi kuwa tuko njiani kuelekea kwenye anguko kuu.

Nilitabiri kwenye uzi hapa kuwa wanajua fika wanachokifanya. Ni makusudi tu na kuwa kuna kitu wanachokisubiria. Bila shaka come April, mwezi huo hautaisha watachukua hatua stahiki.

Ajabu ni kuwa wanafanya ucheleweshaji wa kuchukua hatua stahiki wakiweka maisha yetu sote rehani bila ya kujali.
 
Habarini Wanajanvi.

Pamoja na kua Corona Virus ndo ipo mkononi kwa sasa, haijanisaulisha balaa la Ugonjwa wa UKIMWI kwani hili nalo limeka juu ya Msimamo wa ligi kwa Muda mrefu sana.

Yaani kama ndo ingekua UKIMWI ni moja ya Football club ya Ulaya basi ingekua na uhakika wa kucheza UEFA Champion kila msimu na ingepiga mpaka Finali na kuchukua kombe kila msimu.

Maana UKIMWI naukubali sana kwa kusajiri wachezaji nyota. Maana ukiwa nao Magonjwa yote nyemelezi ya hatari Ukimwi unawasajiri. Hata hii Corana tayari UKIMWI imeuona na inataka uisajiri kwa Muathirika. Yaan ukimwi siku zote inasajiri mastriker wa hatari.

Naombea sana kama Dawa itapatikana ama kinga itakayotibu na kuzuia corona virus basi ndo hiyohiyo dawa itibu na ama kukinga virus visababishavyo Ukimwi. Waafrika tumeonewa sana na huyu jamaa.

Tunapojikinga na Corona Virus tusijisahau pia kuna huyu UKIMWI bado yupo vizuri kuliko hata hii corana virus na ikitokea wakapiga corabo mziki wake utakua sio wa dunia hii.

Take Care.
 
Corona limao, ndimu, kusukutia na chumvi na chakula bora.Kuishi ukanda wa joto.
 
Daaaah!!! Heading yako inamatiki lakini ulivyokua unaendelea kuandika nadhani dish liliyumba na kuanza kuandika fyongo maana ulichokiandika mstari wa mwisho kinaonyesha umekosa busara.

Kwenye andiko lako fyongo ni hii hapa ' UKIMWI bado yupo vizuri kuliko hata hii corana virus na ikitokea wakapiga corabo mziki wake utakua sio wa dunia hii'. Hapa umekosa Busara.
 
HabariJf!

Toka Corona iingie hapa bongo na ku kiki,kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitake advantage ya Corona kwa kujinufaisha.

Kuna watu wamekuwa hawataki kulipa wenzao kwa kisingizio cha Corona.

Kuna mpangaji wangu ,Jana nimempgia kumdai hela ya kodi maana kodi yake imeisha mwezi uliopita.

Jamaa ananijibu mambo magumu eti si unajua babu Corona,nikimfuata simkuti anatoka saa11 alfajiri anarudi watu wote wamelala.

Jana sasa nimempgia ananijibu eti nipo Karantini babu ,nikamuuliza upo Karantini gani nikufuate unipe changu akakata simu.

Ombi langu watu walipe madeni sio ishu kuleta visingizio vya kijinga.
 
Back
Top Bottom