Ni muda sasa Dunia ikiwa ina pambana na Janga la Corona.
Modelling ya Wanasayansi nchini Kenya inaonesha kufikia mwishoni mwa mwezi April 2020 kuna uwezekano wa Kenya kuwa na Wagonjwa 10,000. US inaonesha by August 2020 marehemu wanaweza kuwa zaidi ya 82,000. Italy kwa sasa vifo ni zaidi ya 12,000.
Nchi zetu za Africa hasa Tanzania zimewekeza sana katika Siasa na kubakia madarakani na siyo Tafiti za kuliendeleza Taifa. Nchi yetu imeshindwa hata kufanya tafiti za kuzuia magonjwa ya Mhogo!
Siyo kwamba wataalam hawapo nchini, laa asha! Wataalum wapo wengi sana.
Tatizo kuu la Tanzania ni vipaumbele. Mbunge wa Tanzania sifa kuu ajue kusoma na kuandika tu, mshahara mnono, Gari zuri, Allowances kibao, mikopo, Ruzuku on spot akistaafu. Na huyu ndie apange sera za Taifa karne ya 21 dhidi ya US, Germany, Russia na China. Kweli au ni mzaha?
Bunge letu ni muda sasa haliidhinishi pesa za Tafiti karibu 90% hata ya Pesa ndogo ilioombwa. Hakuna nchi itaendelea duniani bila Research & Development. Hizi ndizo huzaa Innovation (patent rights) kwa wagunduzi.
Utashangaa Mjinga mmoja ana ropoka ni muda sasa wa Maprofessor, madaktari , Watafiti na Wahadhiri kuja na Tiba ya Corona! Yaani Professa umlipe Tshs 3m. Researchers Tshs 1.5m na Wahadhiri Tshs 1.5M (bila gari, nyumba kapanga, no allowances, nk). Afu Kibaji na Mlinga uwalipe Tshs 15m kwa Mwezi! Tena bila pesa za Tafiti!
Ni muda sasa:
1. Serikali itenge at least 1% ya GDP kwa ajili ya R&D.
2. Serikali ijenge Vyuo/Centers za Utafiti. Ziwepo za Virus, Bacteria, nk. Ziwepo za Mazao, wanyama, nk. Ziwepo Centers za Gunduzi za bidhaa, huduma, maarifa, nk. Siyo kila kukicha CBE New Branch, UDSM New Branch, Chato University, nk.
3. Serikali itume vijana wa Sayansi Takribani 2000 nchi zote duniani kuiba maarifa kila nyanja. Na kuwarudisha baada ya miaka 10. Hatujachelewa tuanze sasa!
Hivi ni nchi gani hii hadi Toothpick tunaagiza China? Hand Sanitizers MSD wanaagiza China? Mask hadi msaada?
Ni muda muafaka sasa kuheshimu wasomi na Sayansi. Ni muda wa wasomi kuongea. Siyo kila Mjinga anaongea kuhusu CORONA.
Tuendelee kujikinga na Corona kwa kufuata ushauri wa Wataalam wa Afya. Corona inaua vibaya!
Sent using
Jamii Forums mobile app