#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hivi sasa watu wengi wameacha kuvaa barakoa, wanashikana miili na wachache wanaweka maji ya kuosha mikono. Harakati za jiji zimerudi kama ilivyokuwa mwaka jana na hii ni baada ya kusikia kauli za viongozi zikiashiria hakuna maambukizi mapya wala vifo. Tanzania tumefanikiwa kuishinda Corona ndani ya muda mfupi sana, hii ni rekodi nzuri na inabidi tuwapongeze viongozi wetu. Nikiangalia mitaani kwangu watu wameisahau Corona ndani ya siku chache na maisha yamerudi kama zamani.
Swali, nani ametangaza kuwa Corona imekwisha?
Africa hakuna wazee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watawala wapo kwa sababu yao,sio wewe mtanzania juzi tuliambiwa kipimo ni fake,leo msemaji wa serikali anasema hakuna vifo Wala maambukizi huku wakificha idadi ya wagonjwa lakini mtu kutoka mafichoni anasema hali ni nzuri ,yaani ni shida juu shida
Wewe umezika wangapi?
 
Haki ya maeneo mengi Dar yameanza kurudi kama ilivyokuwa mwezi wa 12 (Desemba) mwaka jana, watu wengi wamevua barakoa na walioweka ndoo za maji ya kuosha mikono nao wameziondoa au kama zipo hazina maji.

Biashara ya barakoa nayo Haina wateja kwa sasa baada ya watu kupata taarifa nzuri toka kwa viongozi, hapa naomba niwapongeze kwa kuimaliza Corona haraka sana kukiwa na vivo 16 tu, pongezi kwenu.
Mkuu unajua kucheza na lugha. Werevu amekuelewa. Corona sio tishio haps Tz. Imeua watu 16 tu nchi nzima ndio maana maisha yamerudi kama kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi kama Kenya tumuamrisha Mpaka wa Tz ufungwe juu hatutaki kutangamana na wajinga watuletee maradhi. .. atangaye sana na mjinga ujingaa. Kaa kwenu
 
Kwahiyo na ule uzi wako wa update za corona umechangia sana kueneza corona Tanzania
 
Fikiria nje ya box, critically and objectively without bias
Wenye kuelewa wameelewa. Mimi sitaandika chochote kuhusu COVID-19 kesho.
Wewe ndiyo umenifikishia ujumbe vizuri sana.

Nitakuwa ndugu msomaji tu kesho na siku kadhaa zijazo. Ujumbe muhimu na mzito sana huu.
 
Back
Top Bottom