Mtazamo wa Rais Samia kuhusu Mashirika ya Umma si sahihi

Ila Kwa hiyo hapa wewe unaona ni.sawa si ndio? Nyie wajamaa ni mzigo Kwa Taifa

View: https://www.instagram.com/p/CyOd4lEtXKf/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Haya unayoyasema yapo pale tu kwa nia njema tu ya Marais waliopita na huyu aliyepo. Siku ikitokea akaja Rais mwingine mwenye msimamo kama ule wa awamu ya nne, utayasikia hewani tu
Utasubiri sana, kwa mazingira ya sasa hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya unavyotamani iwe.

Mwendazake aliweza kufanya yale kwa sababu kwa kauli yake mwenyewe alisema alikuwa na kichaa na ndugu Antony Dialo alituthibitisha kuwa Mwendazake alikuwa na cheti cha mirembe!

Hatuhitaji Rais kichaa!
 
Ahsante mkuu!
 
Kinachopingwa ni uwekezaji wa DP world au ni vipengele ndani ya mkataba wa uwekezaji? , mkataba walioingia na India na huu waliongia na sisi ni sawa?
 
Mkuu, umenikumbusha. Nilisikia shirika la umeme la Afrika Kusini limefilisika ilhali tuliletewa hapa wakusanye madeni kwa TANESCO!!!!
 
Uchumi umeusomea wapi? Nawasiwasi umwsoma soviology ndo mana we ni mweupe kichwani. Au umesoma engineering. Kumbuka mwiguli ni first macroeconomist hata imf inamjua
Ndokaweka kodi ya sh 100/= kwenye mafuta akituambia bei yake huko yanakouzwa inashuka. Ajabu bei inapanda tokea August na hakuna tamko lolote la kuiondoa hiyo kodi wala uwajibikaji kwa uongo.
 
Ni awamu ya tatu tafadhali, siyo ya nne. Tuliuza kila kitu kwenye awamu ya tatu na si ya nne
 
Ni awamu ya tatu tafadhali, siyo ya nne. Tuliuza kila kitu kwenye awamu ya tatu na si ya nne
 
Reactions: Ame
Hakuna sehemu duniani serikali haifanyi biashara Halotel ni shirika la serikali huko duniani, huu ni mfano mdogo

KCB ni serikali ni mfano mwingine mdogo

Endelea kuwa masikini wa fikra... serikali I natakiwa ifanye biashara
 
Reactions: Ame
Mimi naona serikali iruhusu ushindani kwenye hayo mashirika kama ilivyo kwenye simu, benki, mafuta, elimu, afya, usafirishaji na kadhalika.
Hilo likirushiwa Kuna namna nchi itatekwa na wache kisha wengi watabaki kama watwana.

Mwandishi ameweka vizuri, mashirika yote ya umma yaliyobaki ni ya kimkakati wa maendeleo ya taifa na yanahusu usalama wa nchi na watu wake. Kama wanataka waende kufufua Yale yali binafsishwa enzi za Mkapa yafanye kazi, kwanini hawataki kwenda kuwekeza huko wanataka haya mashirika ya kimkakati? Huo ni ujambazi na uporaji wa Mali ya umma watanzania katu tusikubali kurubuniwa. Mkapa mwenyewe amekufa akijutia ubinafsishaji, Leo Yale Bado hayajarudia kama enzi yalivyokuwa wanataka kutuletea mambo ya state capture kwakua consolidate wealth and power Ili wao wawe ndiyo kama wafalme? No and no thank you!
 
Hakuna sehemu duniani serikali haifanyi biashara Halotel ni shirika la serikali huko duniani, huu ni mfano mdogo

KCB ni serikali ni mfano mwingine mdogo

Endelea kuwa masikini wa fikra... serikali I natakiwa ifanye biashara
Watu wetu hawana exposure ya kutosha na wale wenye exposure wengi wameamua kuungana na ma kabaila wa Dunia kunyonya raia wa kawaida
 
Ulitakaje?
 

Ulishawahi fika India ukaona umasikini uliopo Kwa mtu wa kawaida au unaongea tu kinadharia?

India ambako mtu Hana hata sehemu ya kuweka nyumba yake huko rural ndiyo ulinganishe na Tanzania ambayo Kila household Ina access kwenye land? Acha utani wewe!
 
Kinachopingwa ni uwekezaji wa DP world au ni vipengele ndani ya mkataba wa uwekezaji? , mkataba walioingia na India na huu waliongia na sisi ni sawa?
Wanaolalamika mkataba hawana uelewa wa hiyo mikataba. Wanasema kuwa DP World atakuwa na utawala mzima wa masuala ya bandari. Vipi kuhusu hizi barua za TPA zilizopo mtandaoni zinazotangaza zabuni ya uendeshaji kwa makampuni mbalimbali?.

Kama DP World wanatufunga kwa vipengele vya mikataba, mamlaka ya TPA inapata wapi nguvu ya kutangaza hizi tender za uendeshaji wa Bandari?.

Hao kina Prof Tibaijuka na wanasheria wengine wengi tulionao kwa makusudi wameamua kupotosha umma kwa malengo wanayoyajua wao wenyewe.

Mkataba hauna tatizo lolote, sisi tunaousoma na kuutafsiri kwa uelewa wetu ndio wenye matatizo.
 
Wingi wa watu ni changamoto dunia nzima.

Sisi wenye maeneo ya wazi bado ndio tunakimbilia kwao kutibiwa sukari na mioyo yetu.

Tazama wahindi wanavyokimbiza kwenye orodha ya matajiri wa dunia nzima.

Tazama wanigeria wanavyofanya vizuri kwenye sekta ya afya huko Marekani na UK.

Wanajielewa kuliko sisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…