Mtazamo wa Rais Samia kuhusu Mashirika ya Umma si sahihi

Mtazamo wa Rais Samia kuhusu Mashirika ya Umma si sahihi

Sawa, je, Kwenye mkataba wa bandari uliosainiwa na Rais na kupitishwa na bunge, kuna kipengele chenye title ‘UKOMO’?
Elimu yako ni ya darasa la ngapi?, Mkataba wa bandari uliosainiwa na Waziri Mbarawa kwa niaba ya Rais Samia kule Dubai hauna kipengele cha ukomo.

Nimekueleza zaidi ya mara mbili kuwa ukomo unazaliwa baada ya kuwepo kwa mikataba ya kibiashara, hauandikwi kwenye mkataba wa IGA uliopita bungeni.
 
Elimu yako ni ya darasa la ngapi?, Mkataba wa bandari uliosainiwa na Waziri Mbarawa kwa niaba ya Rais Samia kule Dubai hauna kipengele cha ukomo.

Nimekueleza zaidi ya mara mbili kuwa ukomo unazaliwa baada ya kuwepo kwa mikataba ya kibiashara, hauandikwi kwenye mkataba wa IGA uliopita bungeni.
Hakipo?! Kumbe napoteza muda kubishana na mtu ambae hata hajausoma mkataba wenyewe?!
 
Hakipo?! Kumbe napoteza muda kubishana na mtu ambae hata hajausoma mkataba wenyewe?!
Nimekuuliza swali elimu yako ni darasa la ngapi haujanijibu.

Hakiwezi kuwepo kipengele cha ukomo, kwani ukomo unakuwepo kwenye mikataba ya kibiashara.

Mkataba wa jumla unaokwenda bungeni hauwezi kuwekwa ukomo.

Narudia zaidi ya mara tano kukupa elimu ndogo tu hiyo. Novemba mwanzoni nenda pale TPA utakuta mambo yamebadilika kabisa.
 
Kuna tetesi kuwa hoteli zilizokuwa zinamilikiwa au zina hisa za serikali huko kwenye mbuga....
Watakunywa bila shaka. Inaelekea Rostam aziz ndio mshauri mkuu na mama mwanae abdul ndio mfuatiliaji migao ya mama😂🤣🏃🏃
 
Watakunywa bila shaka. Inaelekea Rostam aziz ndio mshauri mkuu na mama mwanae abdul ndio mfuatiliaji migao ya mama😂🤣🏃🏃
hata sijui...yatarudi maana JPM lazima arudi tena kwa haya mazagazaga yanayoendelea
 
Serikali ya Samia eti inatazama mashirika ya umma kama uwekezaji wa kibiashara ambapo serikali haistahili tena kuwekeza ila watu binafsi. Msimamo huo sio sahihi kwa sababu mashirika ya kibiashara ya umma yalikwisha binafsishwa yote tangu awamu ya Mkapa. Yale yaliyobakia ni yale ya kimkakati kwa maendeleo ya nchi hayawezi kupewa watu binafsi.

Mashirika kama TANESCO, TTCL, TRC, Air Tanzania, mashirika ya kuzalisha na kusambaza maji, TPA, etc etc. Ili mashirika ya kimkakati kua na tija na kufikia malengo ya uwepo wake lazima serikali iwe na utashi wa kuyasimamia vema.

Serikali inayoruhusu vigogo wake wale kwa urefu wa kamba zao kwa vyovyote itakua na muelekeo wa kuwaacha vigogo kupora kutoka mashirika ya kimkakati ya umma na hatimae kujidai kuyabinafsisha huku ni uporaji wa mali ya umma.

Hatuna haja kuonesha kwa nini mashirika ya kimkakati kwa maendeleo ya nchi yawepo. Na tukisema maendeleo ya nchi tunamaanisha maendeleo ya umma wa wananchi na sio tabaka fulani.

Tuliwahi kubinafsisha TRC, TTCL, na air tanzania na tulichokiona kama matokeo ilibidi kuyarudisha mashirika hayo mkonono mwa umma kwa maana ya kumilikiwa na serikali.

Reli tuliibiwa na wahindi mali zote zisizohamishika kama majumba na viwanja kwa maana walipiga hela wao na mwisho hadi karibu kuibiwa uwezo wa kujitegemea kwa wao kuanza kupeleka vichwa vya treni india kwa matengenezo ambapo karakana na wafanyakazi wenye ujuzi na uwezo walibakia kinywa wazi.

Kuhusu Air Tanzania vivyo hivyo makaburu wakatuadhibu vibaya.

Kinachotakiwa ni Samia kuwa makini na ajue sera na itikadi za CCM bado ni relevant asituchanganyie ulaji kwa urefu wa kamba wakati ni uporaji wa umma.

Kinachotakiwa ni usimamizi imara wa mashirika ya kimkakata na kuacha kufanya uteuzi kishikaji ambapo wapigaji na watu wasio na weledi na uzalendo kupewa kuendesha mashirika hayo.
Hivi zile magawio ilikuwa inatolewa Enzi ya JPM imekuwaje nyakati hii hatuyasikii tena? Na kama walikuwa wakweli hizo pesa Sasa hivi zinaenda wapi?
Serikali bado inaendelea kuwapa hela??
Mfano wa ATC! TTCL nk!!?
Nchi ni ngumu hasa mchwa wanaendelea kuitafuna!!
 
Back
Top Bottom