Mtazamo wangu kuhusu majini (mashetani/ mapepo). Uliza swali lolote nitakujibu

.....
 
Hallucination hufanyika Sana Na Kila mtu anaweza kupata..

Hivi hallucination ni kigezi cha Kuwepo kwa Majini?
Okei habu nieleweshe zaidi hapo
 
Sasa nikisema majini ni gesi ambayo haijagunduliwa tuiite gas X ntakuwa nakosea?

Yapo ila hayaonekani wala hayashikiki ila yanaweza kumfanya mtu aone vitu ambavyo havipo (hallucination) kwa kuvuruga physiology ya mwili



Je nitakuwa nakosea?
Nimependa ulivyothubutu kutoka nje ya box.

I’m interested in your thinking & observation patterns, tuendelee…
 
Hizo emoji za kujichekesha za nini?


Umesoma context ya niliyem-quote?
Emoji za Kucheka Zimeingis Vbaya Tusamehe wazee wako simu za Kupangusa zinatushinda Lengo nilikuwa Nimeweka semicolon na alama ya Kujumlisha naona Imekuja Emoji za Kucheka
 
Carbon monoxide ikishikina na haemoglobin ni ngumu sana kuachiana.

Ningetegemea kama ni kweli majini ni gas ya carbon monoxide basi wenye majini wangekuwa wanakufa Kwa suffocation.

All in all hii kitu nimeipenda kwasabab Ina ukweli ndani yake ukirelate
 
1)Majini ni sehemu ya 1/3 malaika waliofukuzwa mbinguni baada ya kumuasi Mungu wakafukuzwa mbinguni baada ya kuasi.Majinj ni wengi.

2)Shetani-ni aliyekuwa malaika mkuu wa sifa mbinguni lucifer akaasi na kuwashawishi 1/3 ya malaika wamuasi Mungu wakafukuzwa mbinguni baada ya kuasi kwao.SHETANI ni mmoja tu hakuna mashetani.

UASI WAO
Ulianzia moyoni mwa lucifer aliwaza moyoni mwake,alitamaninna yeye aabudiwe kama Mungu,awe na malaika wafuasi wake wa kumuabudu kama Mungu anavyoabudiwa.
Kwa vike alikuwa malaika mwenye kusifiwa na kuheshimika na mwenye cheo na kiongozi wa sifa aliongoza malaika wengine kwa muziki wake mzuri katika ibada za kumuabudu Mungu.
Aliwaza kwa ushawishi aliokuwa nao ashawishi 2/3 ya malaika ili wamuasi Mungu na wawe followers wake ,then aanzishe enzi yake mbingu ya juu kuliko ile ya Mungu aweke koti chake huko na enzi yake huko ili aanze kuabudiwa aanzishe mbingu yake na utawala wake.Pia aliwaza kuwa hata malaika 1/3 watakaobaki loyal kwa Mungu hawataweza kumshinda hata wakifanya vita.Baada ya kushawishi malaika mbinguni alifanikiwa kupata malaika wafiasi 1/3 bada ya 2/3 aliyoikusudia ndio hao MAJINI malaika waasi .

KUFUKUZWA KWAO MBINGUNI.
Baada ya lucifer na 1/3 ya malaika kuasi.Mungu alimuinua juu zaidi malaika mmoja akampa ukuu ,mkuu akampa nguvu anaitwa malaika MIKAELI akamshusha chini walipokuwa lucifer na ile 1/3 ya malaika waasi.Alipotua tu malaika waasi 1/3 na lucifer wote wakaanguka chini ya dunia kuzimu ya chini kabisa.hata ukisema chini ya bahari kama egbermuda triangle n.k sawa ila mwisho wa siku ni UNDERWORLD chini chini kabisa.

MIZIMU -ni majini yanayowapata wana familia wana ukoo..yanapenda kuwapata wana ukoo kizazi hadi kizazi ndani ya ukoo.

MISUKULE -Ni watu ambao duniani walishakufa na kuzikwa au walipotea lakini kiuhalisi hawajafa ila wamefichwa mahali duniani au kuzimu ya duniani.Misukule inaweza na mara nyingi ndio inavokuwa inapandikizwa roho za majini na kutumika katika shighuli za kishirikina.inaondolewa ufahamu.mara nyingi inachukukiwa na wachawi walozi waliomloga kuonekana amekufa kumbe ni mazingaombwe hajafa kafichwa na wachawi,wanamtumikisha katika shighuli zao.

MAJINI WANAOA WANAZALIANA WANA WAZAZI
Wana koo pia wana oa na kuzaa na hufa.
pia wanaweza kuoa mwanadamu wanaweza kuzaa na mwanadamu,wanatumiwa na wachawi.waganga wa kienyeji mizimu ya ukoo,mitume na manabii washirikina ,watu wanaotafuta umaarufu,mafanikio n.k

WANAISHI WAPI SHETANI NA MAJINI
Wanaishi kuzimu na duniani na kwingine isipokuwa mbinguni.
Kuzimu (chini ya ardhi,au chini ya bahari,makaburini,chininya maji,chini ya shimo la choo,yani kicupi chini ya iso wa dunia shimoni kuzimu underworld ndio makazi yao ya asili lakini,hata angani anganla sadiki sio mninguni ila ni angani wakuu wa anga,sehemu zite isipokuwa mbinguni.
kuna wakati shetani anatoka kuzimu anakuja duniani kufanya kazi maalumu ya kudanganya duniani au kazi ovu,majini kadhalika huwa yanakuja duniani.
Na yapenda duniani kwa vilw yanapata makazi mazuri na chakula..damu za watu

MILANGO YA KUINGIA NA KUTOKA KUZIMU
Vyanzo vya maji vishima vya maji,mabwawa,mito,maziwa,bahari,madimbwi
CHOO CHOONI
MAKABURINI N.K

MAUMBO
Yanaweza kuvaa au kuja kwa umbo lolote kama mnyama,ndege mdudu ,binadamu
Kama akija kwa umbo la binadamu sura yake itakuwa haitulii au macho yake yatakuwa hayatulii yanacheza cheza yatakuwa yatofauti na wanadamu wa kawaida.

MAJINI WOTE NI WABAYA
Hakuna jini mzuri ..hata kama anakupa pesa mvuto anakusaidia lakini sio mwema kwa binadamu,wao no aduibwa mwanadamu kwa sababu mwanadamu anapendwa na Mungu na wao walishafukuzwa mbinguni hawawezi kurudi mbinguni mana na mbinguni wanapajua ni pazuri wana wivu hawapendi binadamu twende mbinguni wanataka binafamu waende motoni pamoja nao ili kumkomoa Mungu akose watu kule mbinguni na wao wapate watu wa kwenda nao motoni.

ZIWA LA MOTO SEHEMU WALIYOANDALIWA SHETANI NA MAJINI
Baada ya shetani /lucifer kuasi na 1/3 ya malaika waasi kufukuzwa mbinguni.Walihukumiwa mana walitenda uasi kwa makusudi wakijua na walishakuwa mbinguni tayari...Wameandaliwa ziwa liwakalo moto ..MOTO WA JEHANAMU ni kwa ajili ya shetani na majini au malaika waasi .Mwanadamu yeyete ameandaliwa pepo lakini iki uweze kuingia peponi inakubidi 1)UWE MTAKATIFU -uache uovu ,umpende na kumoendeza Mungu na kushika na kuzifuata sheria zake 2)UTENDE MEMA 3)YESU KRISTO PEKEE NDIO NJIA YA KWENDA MBINGUNI..umkubali huyu Yesu aliyekuja kutoka mbinguni akafa msalabani ili kukomboa ulimwengu mzima Yesu ni mkombozi mwakozi wa watu wa ulimwengu wote dunia nzima hana dini ni wa watu wote aliowaumba yeye Yesu akishirikiana na Mungu baba na Mungu Roho mtakatifu.

KWANINI WATU HUWAONA MAJINI NI WAZURI
Kwa sababu majini yalipofika duniani yaliwafundisha watu waliokuwepo duniani ELIMU ZA SAYANSI,TEKNOLOJIA ,PIA UCHAWI na mabo mengi maovu,silaha vita n.k..pia yalizaa na wanadamu yakazakiwa majitu marefu yaliyokuwa makatili sana na yenye akili sana.
Hata leo majini yanashirikiana na wachawi,na waganga wa kienyeji ,na binadamu..binadamu kama binadamu pasipo msaada wa majini hawezi kufanya uchawi wala ushirikina au uganga wa kienyeji bila MIZIMU/MAJINI.
sasa yanawapatia watu pesa umaarufu,mafanikio ,uchawi ..ndio mana watu wanayaona ni mazuri wengine wanayaita mizimu yetu mizuri inatusaidia,wengine wanataita WALIMU WAZURI..n.k

ATHARI ZA KUSHIRIKIANA NA MAJINI/MIZIMU
Masharti yanakupa mafanikio yenye masharti na kafara
ukifa unaendan motoni kuzimu ya motoni
Unakosa ishirika na Mungu,unakosa matunda ya Roho mtakatifu FURAHA ,AMANI,UPENDO,UVUMILIVU,UPOLE,UTU WEMA,FADHILA ,UAMINIFU ,N.K matunda kama 9 hivi.
Maisha ya watu wanaoshirikiana na majini ni ya chuki,wivu visasi hasira ,hayana amani,yanawaza mabaya tu..hayana mema..ni ya kuigiza,pia yana uchungu mwingi.
na masharti magumu,na kafara sadaka nyingi washirikina wanatoa sadaka kafara kubwa kuliko wacha Mungu tena kafara zao ni za lazima
 
Mkuu,umeandika vitu vikubwa na vya maana sana;binafsi nimekuelewa vzr sana sema wengi hawawezi kukuelewa kwa kuwa elimu ya darasani imewawekea uzio na ukomo wa kufikiri.Unayo elimu kubwa sana ambayo haifundishwi Darasani lkn,ipo na inafanya kazi!
 
SHETANI NA MAJINI+WASHIRIKINA KUZIMU YOTE WANAOGOPA NINI??
shetani majini na washirikina(waganga wa kienyeji na wachawi,KUZIMU YOTE) yanamuogopa JINA LA YESU KRISTO. likitajwa na mtu yeyote hasa aliyemuamini Yesu na kumkiri kuwa ni mwokozi wake.
Mtu anayesali kwa kutaja jina la Yesu hasa akiwa ni mtu wa haki mtu mwema asiye jichanganya na madhambi...AISEE HILI JINA LA YESU huwa linawasababisha uharibifu mkubwa sana kuzimu na kwenye vilinge vya wachawi na waganga wa kienyeji.
Makanisa machache sana yenye nguvu za Mungu makanisa mengi yamekuwa hayana nguvu ya Mungu kwa sababu hata wachungaji wengi wwngine ni washirikina wanashirikiana na kuzimu na majini na hata mafuta yao ya upako yanatoka huko kuzimi hivyo ni huzuni .wanaosali kwa mitume na manabii...pole sana kwao mana wapo njia ya kuzimu..
 
MIZIMU INA NGUVU KUBWA YA KUKAA NDANI YA BINADAMU
Mizimu ina uhalali wa kukaa ndani ya mtu kwa sababu imetokewa sadaka kafara na mababu na ikapewa hati milliki ya ukoo umilikiwa kumiliki ukoo na kizazi chote cha mtu babu wa kwanza hata. kabla ya watoto hawajazaliwa.

Yale matambiko na makafara kama wanayofanya watu wa kaskazini wanapoenda kuhesabiwa ile mizimu ya mgombani inapata uhalali wa kukatama kizazi chote hata ambao bado watakuja kuzaliwa baadae mizimu itawasumbia kwa sababu ya makosa ya baba zao na babu zao.Dawa ni YESU PEKEE ndio kiboko ya haya maroho machafu.
 
DALILI ZA MTU MWENYE MAJINI
Haziko specific zinatofautiana kadiri ya kusudi la huyo jini aliyekuingua amelenga nini kwako kukuua ,kupiga afya yako,uchumi wako,ndoa yako,uzazi,ufukuzwe kazi,usikubalike udharaulike,ukataliwe usipendwe,upate ajali,uingie kwenye kadiri ulivyologwa dalili zipo nyingi na nintofauti kati ya mtu na mtu kadiri alivyologwa hakuna dalili common.

NDOTO UNAZOOTA USIKU UKIWA UMELALA
Zinaweza kukupa picha kama una majini umelogwa unaweza kujua ukifafanuliwa ndoto unazoota ndio njia rahisi na dalili nzuri ni kupitia ndoto.
 
Ndio lakini inabidi utafute msaada nenda kwenye maduka ya kisuna yanakuwaga karibu na misikiti huko utapata dawa nzuri zipo nyingi tu
Pia nasikia kuwa jini huwa haondoki mwilini mwa binadamu hata kama ukifanikiwa kulifukuza baadae hurudi tena mwilini mwako, hii imekaaje?
 
Sasa tu assume gas X ina sifa kama za carbonmonoxide zilizoboreshwa

Yaani ina bind na haemoglobin kisha ikikuachia inakaa kwenye serum kusikilizia i bind tena

Hapo unaonaje mkuu?

Majini yanaweza kumuua mtu kwa ku suffocate (kumkaba) je unajua hicho kitu mkuu?


Tukimuuliza DR Mambo Jambo atuelezee kitaalam hii scenario ataweza? Tumsubiri


Kama watu hawana mawazo tofauti watagunduaje vitu vipya au kufanya thesis?

Hivi unajua mtu akija amekabwa ana suffocate wakati huo ana hallucinate na kuongea kiarabu akivukizwa moshi wa majani flani au moshi wa karunguyeye hiyo hali inaisha hapo hapo


Najua tukimuuliza DR Mambo Jambo atatuambia ni asthmatic attack lakini ukimuuliza mtu mwenye asthma huwa ana halkucinate? Au anaweza kukaa hata lisaa akiwa kakabwa na kuchanganyikiwa ? Tusubiri jibu?
 
Pia nasikia kuwa jini huwa haondoki mwilini mwa binadamu hata kama ukifanikiwa kulifukuza baadae hurudi tena mwilini mwako, hii imekaaje?
Yanaweza kufukuzwa

Kuhusu kurudi endapo yatakuwa yametulizwa tu
 
Unamaanisha Majini au Majinamizi? au ni kitu kimoja?
 
Hallucination hufanyika Sana Na Kila mtu anaweza kupata..

Hivi hallucination ni kigezi cha Kuwepo kwa Majini?
Okei habu nieleweshe zaidi hapo
Ki medical majini hayatambuliki, akija mtu mwenye majini hapo ofisini kwako utamterm kama mgonjwa wa akili ,(psychosis) utamsukuma wodi ya vichaa

Ila kabla hujafanya hivyo uta request vipimo ikiwemo cha Malaria

Sasa kikawaida mtu akiwa na supply ndogo ya oxygen au glucose ktk ubobgo kupitia mzunguko wa damu hupata hallucination (japokuwa sio watu wote)

Sasa mtu mwenye afya njema mfano mganga wa jadi au yeyote mwenye majini akivukizwa ubani au kupigiwa mdundo (dufu) anaanza kupitia pattern zote za mtu anaye hallucinate


Ataanza kuona vitu ambavyo mlio pembeni hamvioni, ataanza kukuambia matatizo yako kwa usahihi (mganga) ataanza kuongea lugha mbali mbali, kucheza au anakuwa kama anatembelewa na kitu ktk mwili wake utamuona kupitia body language na movement zake


Yote hayo yatatokea akiwa hajitambui (disioriented), je utasema ubani au mdundo ni triger au precipitating factor?


Sasa turudi kwa mtu mwenye malaria kali ambaye RBC zake zinapasuka pasuka na plasmodium wanakula glucose sasa supply ya oxygen na glucose si itakuwa chini?
Akianza kuhallucinate si ndio?


Nikirudi nyuma nkasema kukiwa na gas X ambayo ina combine na haemoglobin ili kupunguza oxygen kwenye circulation na kusababisha hypoxemia kwenye tissue za ubongo na mtu kuhallucinate ntakuwa nakosea?
 
Nasikia ukianza kufatilia sana haya madude basi lazima yatakua part ya maisha yako
 
Mimi Nakuelewa Sana ila Tu sitaku Kurelay kwenye Thesis zako kwa Sababu bado hujaelezea Vya Kutosha Hujatoa Sababu za Kichemikali wala Hujatoa sababu za KIbaologia..

Though Point zako Zina matter sana Na Kuna Kiukweli kidogo japp bado hujaeleza Vizuri na Kwa kina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…