Mtazamo wangu kuhusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli

Mkuu labda nikuulize kitu, kwanini umebezi kwenye Chuki ya Lisu dhidi ya Jiwe na siyo Chuki ya Jiwe dhidi ya Lisu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kuna mchangiaji amedai Tz haijawahi kujenga reli tangu tupate uhuru. Kuwa Jpm ndiyo Raisi wa kwanza kujenga reli ktk Tanganyika / Tanzania huru.

..nilichofanya mimi ni kumkumbusha kuhusu ujenzi wa TAZARA ambao ulikuwa ktk miaka ya 70.
Financier wa TAZARA (interest free loan kwa maneno mengine ni reli ya msaada co kwmb tulijenga) [emoji116][emoji116]
"The TAZARA Railway" The TAZARA Railway

Sent using Jamii Forums mobile app
 

..Je, Jpm aliyewapokea walawiti watoto ikulu unamuelezeaje? How do you defend that?

..Je, hudhani kwamba kitendo hicho kinaichafua Tz?

..hao tunawaomba misaada ingawa baadhi yao wanaunga mkono ushoga lakini wote wanapinga ulawiti watoto. Lakini hapa Tz tumeona walawiti watoto ndiyo watu wa maana wa kupokewa Ikulu na taarifa zake kusambazwa na vyombo vya habari vya serikali.

..Nchi hii itawekewa vikwazo kwasababu ya UKATILI wa serikali ya awamu ya 5, siyo kwasababu TL amependekeza tuwekewe vikwazo. Mabeberu wana wawakilishi wao hapa nchini na wanaona kinachoendelea.
 

Ati wasema Tumeshaamka zamani sana, lakini wakati mtakapovuta blanketi kutakuwa kumekucha.

Hoja yako kuwa asipoteze muda wake kwa kujenga baadhi ya miundombinu, akidhani watu wa kizazi hiki watamkubali yeye au chama chake ni hoja ya kitoto kabisa. Mpiga kura, hasa wa vijijini, anahitaji huduma bora ya afya, elimu, maji na miundo mbinu ya usafirishaji itakayomwezesha aweze kufanya shughuli zake za kijamii, kisiasa na hasa kiuchumi kwa majira na misimu yote ya mwaka.

Unadai ati Kama alidhani akitekeleza baadhi mambo na kuondoa uhuru wa vyombo vya habari, tutamsujudia na kumkubali yeye au chama chake basi amechemsha, ni fikra za mfa maji kisiasa. Siasa za majukwaani zimepitwa na wakati. Na siasa za kwenye vyombo vya habari au/na mitandao ya kijamii ni za udaku tu.

Sijui kwa nini viongozi wa upinzani wanaamini kuwa Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo itawaingiza madarakani!! Wakumbuke tu kuwa wahenga walinena Mkono mtupu haulambwi.
 
Mistari ya mwanzo tu umeshafeli.
Hopeless!

Sina sababu ya kusoma hadi huko mwisho.
 
“Siasa sio Matusi au Chuki, Hoja Hupingwa Kwa Hoja”
Mtu anaye vaa nguo iliyo andikwa pray for Lissu kwanini aswekwe ndani?. Udikteta wa Magu ulikuwa bayana kabisa kwenye swala la Lissu. Alafu wewe unaita ni tofauti za kisia , be serious bwana!.

Mtu anapigwa risasi nyingi hadharani namna Ile afu no uchunguzi, unamnyima matibabu, unamnyima mshahara, unazuia hata marafiki kumpa pole, unazuia hata wanaotaka kumwombea!

Unakamata hata wenye kuvaa nguo tu iloandikwa tumwombee unawaweka, unamvua ubunge, unaweka mbunge mwengine kisha unarudi kuwatangazia kuwa utawashushia neema kwani "Lissu si mbunge wao!."
Ndugu yangu wewe kama hayo yote unayaita tofauti ndogo za kisiasa basi na wewe ni dikteta tena mwandamizi kabsaaa.
 
Acha upuuzi.

Weka tume huru ya uchaguzi, achana na hizo porojo ndefu.

Bei ya haki yako ni barabara? Unayo akili timamu kweli?
Kwako wewe bei yako ni Mbowe na genge lake la wanasiasa waongo na wenye uchu wa madaraka, ambao wako tayari kwa lolote, ikiwa ni pamoja na kuwaingiza WaTz wasio na hatia mitaani, kwa kile wanachodai "demokrasia" ili waingie Ikulu kutimiza ndoto zao binafsi!

Mbowe na genge lake, tangu wamepata hayo madaraka wamewafanyia nini walio wapa kura ya KULA, zaidi ya kutumia ruzuku kwa maslahi yao binafsi!

Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura kuathiri matokeo.

Endelea na kuwa NYUMBU lakini kumbuka hata mamba wamo kwenye kundi lenu.
 
Kama unatambua hata Trump anakosolewa ushawahi kuona anawaua wakosoaji wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali kadhalika si dhani kama unaweza kuleta maendeleo yaliyomazuri kwa kudhulumu maisha ya watu. Binafsi sikubaliani na siasa za kuuana. Ila kama mtazihalalisha hata ninyi ni vyema mkaandaa shingo zenu ili mzionje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kumung'unya maneno, kiongozi wetu anaonyesha wazi kuwa ana matatizo. Kiuongozi, kiafya ya akili na amekosa kabisa hata hekima kidogo tu ya kiuongozi.

Mnaandika maneno mengi, lkn huyu Rais hafai hata kabisa kuongoza taifa hili.

Kuhusu Lissu, mnataka afanyaje wakati ni wazi pia kuwa waliotaka kumuua kwa kumrushia risasi 38 wanakingiwa kifua na serikali?
Si hilo tu, anafanyiwa Dhihaka na rais eti alikuwa mbunge anaezurura tu huko nje ilhali alipigwa risasi na watu ambao wanakingiwa kifua na serikali ya Magufuli?

Huyu mtu wenu mwambieni ukweli, kwamba ameharibu sana nchi hii! Na hata kama anatutisha tusiseme haya wazi lkn watanzania wengi wanamnafikia, hawampendi na wanamlaani!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na tatizo lako na wengine nikumpa uMungu kwamba hajakosea, hakosei, ana nia nzuri na kumruhusu asifuate taratibu tulizojiwekea kwa kisingizio cha kazi.

Hii nchi haijawahi simama kabla ya uhuru na baada ya uhuru.
Tuliwahi fikia literacy rate zaidi ya 90 na sasa si hivyo. Zimewahi kujengwa shule nyingi sana kabla yake.
Tumewahi kuwa na viwanda vingi na kusafirisha bidhaa nyingi nje.
Kuna watu nchi hii (pengine na yeye) wamesoma bure mpaka chuo kikuu.
Barabara na madaraja mengi makubwa yamejengwa kabla hajawa yeye raisi.
Zilikuwepo ndege nyingi kuliko zilizopo sasa.

Kutwa watu wanatukaririsha humu kuwa uncle ndo kila kitu. Nina uhakika kwa unyoofu wa mwenendo wako watanzania wengi tu wakumzidi. Kwenye milioni 55 hatukosi wachapa kazi hata CCM wapo na
hakuwaweka yeye wala uwepo wao CCM sio sababu yake.

Kwa nini tupoteze nguvu nyingi kumpamba mtu ambaye anafanya wajibu wake na tayari kuna waliomzidi kabla yake yote kwa gharama ya kuumiza na kuwanyanyasa wengine?
Kwa nini tuwazuie wengine wasifanye wanayotakiwa kwa misingi ya nchi kisa mapenzi ya mtu mmoja?
Kwa nini tusherekee wengine kuumizwa kisa madaraja?
Kwa nini tumuache akiharibu mifumo ya haki na utawala ambayo tulikuwa tunaiboresha?
Kwa nini tusiwaze wengine kutuongoza ati kuna mmoja kafanya vizuri wakati yeye angali si maarufu alipata fursa hiyo akafika hapo? Je angezuiliwa afanyavyo maana yake angejengea wapi hizo ndoto zake?

Kwa nini turuhusu watendaji malaki walio nchi hii kuishi kama digidigi wakiwindwa wakose ubunifu watende kama maroboti wakati wanatumia rasilimali za nchi?

Nasisitiza huyu ni mtu na atakufa. Muda hausimami. Kama falme ambao ndugu huhakishiwa maisha bora na bado wapo wanaopinduliwa hakuna namna watu milioni wakataka udumu. Na kuwakandamiza siku zote hutengeneza roho za kupinga. Ni heri tuziruhusu katika amani kuliko kuacha zikue zilete hatari.
Samahani Mfiaukweli mataga ni nini?
Mimi sijasema Magu hana mapungufu yake mbona mnanipiga mawe, Magu sio Mungu
Tubishane kwa Hoja tu ila sio kelele

Nifundishe na mie nielewe ambacho unadhani sikielewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani huduma bora kwa hao watu wa vijijini zinaletwa na ccm au ni kutokana na kodi za wananchi? Siasa za majukwaani hazijawahi kupitwa na wakati maana ndio siasa zenyewe. Labda kama hujui siasa ni nini. Siasa za kwenye vyombo vya habari na mitandaoni ni kutokana na nyakati, hizi ni nyakati digital, taarifa nyingi hupatikana mitandaoni.

Acha upotoshaji, wapinzani hawataki tume huru ya uchaguzi ili kuwapeleka ikulu, wapinzani wanahitaji tume huru ya uchaguzi ili mshindi apatikane kwa uhalali. Huenda unabishana kuhusu uwepo wa tume huru bila kujua hata wanaoidai wanamaanisha nini. Tatizo lililopo sio kuwa hamshindi baadhi ya sehemu kihalali, bali huwa sehemu kubwa ya ushindi wenu ni kupitia udhaifu wa tume mnayolazimisha iendelee kuwepo.
 

Unaweza kuleta ushahidi kuwa siasa na uhuru wa vyombo vya habari unazuia ujenzi wa reli, unanyima utoaji wa huduma za jamii nk? Kenya hapo wana uhuru wa vyombo vya habari, wanafanya siasa, huduma za jamii zipo, wana reli kama yetu na inafanya kazi sio hata iko kwenye ujenzi. Na isitoshe uchumi wao uko juu kuliko wakwetu. Mbona huko Kenya hayo yamewezekana. Acheni Utetezi wa kipuuzi, kama hamna hoja kaeni kimya.
 
Umetuhadaa kuwa hauna chama ila dalili zote zinaonyesha Wewe ni kada mwaminifu.Ukweli utatuweka huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za wapinzani ni matusi, hakuna mpinzani aliyenijibu hapa bila kutukana
Unashangaa kuwa watu wako influenced na siasa???? serious? unavyotetea hapa upinzani are you not influenced? haijakuathiri? is that not the reason you are arguing?

Am sorry, but am not an idiot you believe everyone must be. Nina uwezo wa kufikiri, nina kumbukumbu na nina exposure kwenye mambo mengi tu. Sina tabia ya kuamini kitu bila kufanya verification.
Sasa tuje upande wako, unadai Tundu Lissu anaichafua Tanzania; kwa kudai hivyo unaashiria kuwa unaamini hao watu wanaomsikiliza Lissu ni wapumbavu sana kiasi kwamba ama hawawezi wenyewe kufanya verification ya kile wanachoambiwa au hakuna chanzo kingine wanakoweza kupata habari husika. By the same token, imani yako ni kuwa Kila anaemkosoa Magufuli ni mpinzani. Sasa huo ndio upumbavu wenyewe niliokuuliza, maana mtu mwenye akili timamu ni lazima atajua kuwa HAIWEZEKANI watu wote wakawa na mawazo yanayofanana hata kama wamezaliwa mapacha achilia mbali kuwa wanachama wa chama kimoja.

Una hiari ya kumuabudu Magufuli, lakini usitake, usilazimishe wala kutarajia Kila mtu afanye hivyo. Not everyone is a nincompoop.
 
Nimeshakwambia kama Magufuli ana nia njema kwanini asiruhusu huo uchunguzi huru? nini kinachoshindikana hapo.

Tena nikakwambia, utaviamini vipi vyombo vya usalama Tz wakati Lissu akipigwa risasi ulinzi uliondolewa nyumbani kwake?

Sijaona majibu uliyotoa kuhusu hilo.

Na ujue tena kwamba, Lissu kupinga baadhi ya mambo yakiyokuwa yakiendelea Tz ulikuwa ni mtazamo wake, wajibu wenu ulikuwa ni kumjibu muonekane jambo mlilofanya mlikuwa sahihi, sio kukimbilia kumuita Lissu msaliti, huo ni uoga.

Halafu unasemaje nakuwekea maneno mdomoni, hujui unachokiandika ndio kina akisi mawazo yako, so either uandike au uongee yote ni yaleyale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli is a country bumpkin.

Sent from my typewriter using Tapatalk
And has turned Tanzania into a laughing stock. Mtu gani mwenye akili anaeweza kumsema vibaya housegirl wake mbele ya wageni (hata kama mtu huyo ana kosa)? Busara ya kawaida kabisa ni kusubiri wageni waondoke ndipo unamkosoa. Sasa Rais anaewafokea subordinates wake hadharani na kuwauliza watu wasiojua hata taratibu "eti wananchi, hawa niwafanye nini" ni Rais au kituko? Hana ofisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…