Mtazamo wangu: Yanga ndiye bingwa wa CAFCC 2023

Mkuu,kama mashabiki wa Yanga waliwapania mashabiki wa Simba endapo wangechukua kombe wangewadhihaki sana,sasa hapo unataka mashabiki wa Simba waiombee mema Yanga? halafu team pinzani ndio zilivyo,huwezi kukuta shabiki wa Barcelona akaiombea mema Madrid,au shabiki wa Real madrid aiombee ushindi Barcelona,

Relax,ndio ushabiki ulivyo,Anyway Yanga imejitahidi sana,hope next time watachukua kombe.
Sina shida na mashabiki wa Yanga kuwadhihaki mashabiki wa Simba endapo Yanga ingeshinda na ningewapongeza kwa hilo maana lingeleta changamoto kwa Simba kukazana ili na wao walete kombe!

Binafsi kama ningekuwa rais wa nchi hii ningewasweka rumande wote wanaoshabikia timu pinzani kwenye mechi za kimataifa! Haiwezekani wimbo wa taifa uimbwe kabla ya mechi halafu litokee dude fulani jinga kusapoti timu pinzani! Kwangu huo ungekuwa uhujumu uchumi!

Wimbo wa taifa huimbwa katika mazingira machache muhimu kama vile rais anapotaka kuhutubia taifa na timu za mpira zinaposhiriki mechi za kimataifa! Bila shaka, kwa wakati ule, wachezaji wanaliwakilisha taifa! Wapo kwa niaba ya wananchi na kwa niaba mh rais! Kushindwa ni kumuaibisha rais na ni kuliaibisha taifa! Kama ningekukuta unashabikia rais kuaibishwa lazima ungetafuta nchi ya kwenda!
 
Kwa hiyo sisi tuamini hisia zako au tuwaamini CAF?

Yaani tuwe wazalendo wakati ka premature kama ali kamwe amesema uzalendo ni kwa taifa stars?

JItahidi kaa karibu na wale watu wawili pale utopoloni
 
Tatizo lililopo hapa kwetu, ni hili la mashabiki wengi wa simba kuwa mbumbumbu. Kwa hiyo hata serikali ifanye nini, bado hawawezi kuondoa roho za kichawi na husuda mioyoni mwao.
 
Naanza kwa kuipongeza timu ya Yanga kwa hatua kubwa waliyoifikia kimpira!

Japo hawakushinda kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na CAF binafsi naamini Yanga ndiye bingwa wa michuano ya CAFCC 2023. Wamecheza soka safi na la kisomi, hongera kwako Nabi na timu yako ya benchi la ufundi, uongozi wa Yanga na mashabiki wote wa Yanga!

Binafsi naamini kushindwa kwa Yanga kuleta kombe nyumbani ni kutokana na stile ya ushabiki wa mpira hapa nchini almaarufu Kama utani wa jadi unaofanywa na Simba na Yanga! Nafikiri umefikia pabaya na kama serikali haitaingilia kati sioni tukifanikiwa kimichezo! Aina hii ya ushabiki imehusisha mpaka wivu wa "kike", uchawi na inaua uzalendo wetu! Hapana lazima viongozi ngazi ya taifa waingilie kati!

Kama si Simba kuisaidia USM kwa namna ilivyoisaidia (sina ushahidi, ni mawazo yangu) hakuna namna yoyote USM angesinda mechi ya fainali ya kwanza iliyochezwa Dar achilia mbali kuchukua kombe hili!

Nilipokuwa natazama mechi ya mchezo wa fainali ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, mashabiki wa Simba walifurahi kuliko hata USM wenyewe Yanga walipofungwa goli la kwanza! Lakini Kama haitoshi, mashabiki hao hao wa Simba waliumia kiasi cha kutokwa machozi pale Yanga ilipofunga goli na huwezi amini walifurahi furaha kuu ajabu pale USM walipofunga goli la pili! Haipaswi kuwa hivi! Chonde sana serikali, ingilieni kati suala hili!

Natamani sana kuona michezo ikileta na kukuza umoja, uzalendo, amani, upendo, furaha nk.

Tusipoangalia, tutashindwa kuishangilia timu yetu ya taifa vizuri kwa kuwa tu mfungaji ni wa Simba au Yanga!

Ni jambo la kushangaza watu wa Kenya, Rwanda na mataifa ya jirani walikuwa wakiishangilia Yanga jana kwa kigezo cha timu yetu inayoiwakilisha Afrika Mashariki eti kuna mitanzania ilikuwa inaiombea mabaya!!! Huu ni ushabiki wa kilofa!

Nimemaliza!
Wewe ni mwehu kwani jana hukapata matokeo! Au unajitoa ufahamu
 
Mfungwe Yanga,muilaumu Simba...pumbav kabisa
 
Huu ulikuwa mwaka wa Yanga kuupata ubingwa huu ila ndo hivo imeisha hiyo na bahati haiji mara mbili.Inaweza kutuchukua miaka mingi kufikia hatua hii.Fikiria tangu 1993 ndo kidogo watz tumeonja tena fainali.
 
Tena nimeumia sn vyura kushinda 1 jana,anyway hii ndo maana halisi ya kufa kiume sasa.

Hongereni kombe mmebeba
Haipaswi kuwa mtani! Tufanyiane yote mechi za ndani lakini kimataifa tuwe wamoja!

Binafsi naamini kimataifa akishinda Simba ni taifa limeshinda! Vivyo hivyo hivyo akishinda Yanga ni taifa limeshinda!

Faida ya ushindi ni yetu wote! Kama Yanga ikishinda soko letu la mpira kimataifa linaongezeka! Mataifa ya ughaibuni yakija kutafuta wachezaji wa kuzichezea timu zao pengine wakanunua wachezaji toka Simba pia sababu tu ya soka safi lililotandazwa na Yanga!

Mpira ni ajira! Mnapohujumu timu inayoshiriki kimataifa mnauhujumu uchumi wa nchi na mmatakiwa kushitakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi!
 
Huu ulikuwa mwaka wa Yanga kuupata ubingwa huu ila ndo hivo imeisha hiyo na bahati haiji mara mbili.Inaweza kutuchukua miaka mingi kufikia hatua hii.Fikiria tangu 1993 ndo kidogo watz tumeonja tena fainali.
Mwakani tunachukua! Tumejifunza mengi na tunajipanga na mbinu mpya!
 
Back
Top Bottom