Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Wakubwa, hoja zetu ni nzito kweli.

Ila kwa namna CCM Rais ndiye mkiti wa Chama, katibu mkuu wa chama ni mteule wa Rais bila shaka inafahamika Rais akiamua kurea term ya pili kwa utamaduni wa CCM wataotoa form moja tu, na mchezo mzima unaisha.

Ambacho kinafahamika, Spika Job hana nia ya 2025 labda kama alikuwa mshenga wa mwingine? Je, Job ni mshenga wa nani mpaka hii "homa ya 2025" imempata mapema kiasi hiki?

Nikikumbuka Bunge la Spika Samuel Sitta au Big Sam, likikuwa na joto sana na kama ingekuwa ni enzi ya Big Sam, basi Madam SSH angeteseka sana; maana mzee yule sio tu angetoa kauli ila angeunda Kamati Teule kujua kulikoni chunguni?

Nakubaliana kabisa na ushauri wako, kuwa politics na diplomacy vinaendana, ni kama vile US na Russia wanakaa meza moja ila kila mmoja anakuwa na interest zake.

Ikitokea Executive branch akai-pin down Legislative branch kwa sababu ya "argument" na homa za 2025, bila shaka kama nchi tutakuwa tuna-set precedence ambao sio nzuri.

By the way, Mhe. SSH alitaka watu wafunguke na wapumue, na hoja ya Job mpaka sasa bado haina majibu, kwa kuwa tozo zilipitishwa ili tujenge mashule, mkopo wa 1.3 Tril mbona unafanya kazi za tozo?

So far, tunampongeza mama SSH kwa kukopa ili ku-push madarasa yajengwa haraka ili wanetu wasome, japo nadhani kuna haja ya kuongeza wanalimu na learning materials ili kujifunza kuwe na uwiano mzuri darasani na access ya learning materials ikiwepo.

Mijadala ni afya hasa kama ni mjadala wa wazi, na mikopo ni mizuri kama imelenga kujenga nchi kama ule wa 1.3Tril, suala ambalo ni vema wasaidizi wa madam SSH wakaja mbele, ni kuweka wazi fedha za tozo zimekuwa allocated kufanya nini maana tulipata mkopo usio na riba na tume-solve tatizo ili wanetu wakute kuna vyumba vya madarasa.

Mwisho, wizara ya fedha ndio inakopa kwa niaba ya serikali na Waziri wa kisekta asitake "kutuzuga" kuwa mwananchi hatalipa, ifahamike tu, hatakuja mtu kugonga mlango wa nyumba ila wananchi tutalipa kwa namna moja au nyingine, hivyo basi kwenye threshold ya fursa ya kukopa, tusifikirie tu kuwekeza kwenye majenzi, tukopo ili kukuza uzalishaji ambao return on Investment ni ya haraka, na multiplier effect yake inapimika na inaongeza cash flow.

Tukope ili kuongeza ukwasi TIB, TADB ili tusibaki tuna-import basics kama mafuta ya kula, sukari, mashuka ya hospitali, surgical cotton and bandages ila tuzifanye bank hizi zitukopeshe Watanzania kwa dhamana ya serikali, tuzalishe finished consumable goods snd service za kuuza sokoni, kwa namna hiyo tunaongeza tax base na watu wenye misuli ya ku-service mikopo pale inapo-mature.

Siku njema, tuendelee kujadiliana kwa staha, tusiraruane.
 

Kuna nchi ushawahi kuona imepigwa mnada?..

Suala la Tozo wananchi walipiga sana kelele na kuilaumu sana serikali mpaka Rais kuitwa BI TOZO....sasa bila shaka wataelewa mhusika ni nani..

Kukopa sio dhambi, ila tu uwe na unakopa kwa mipango au ukijua namna sahihi ya kulipa either kupitia kodi hizo hizo unazotoza raia au kupitia uzarishaji mali ndani ya rasilimari zilizopo..

Kumbe kuna mtu alikuwa anakopakopa sana na Ndugai alikuwepo kwanini hakuwahi kuyasema haya bali anakuja kusema wengine hapa utaona naye ni muoga na mnafiki tu..
 
Kwanini amebugi? Au kwasababu Rais ambae ni mwenyekiti wa chama ndie alipendekeza jina la job kugombea uspika? Hivi hatuoni haja ya kuwa na spika asiye na chama
Haja ya kuwa na spika asiye na Chama ipo na haikwepeki.

Lakini tatizo kubwa sana sana ni kitu hiki TABAKA LA WATAWALA

Tuiondoe hiyo kwanza
 
Ambayo aliyakataa Samia yana msingi wa kikatiba km ukopaji kinyemela na kupelekwa fedha nyingi Zanzibar kinyume na katiba,agree to disagree ni kwenye mambo yasiyovunja katiba tu na siyo haya ya upendeleo
Weka vifungu vilivyovunjwa, weka data hapa sio empty words.
 
Rais aambiwe anaipeleka nchi yake mnadani anyamaze? Kweli? Huyo atakuwa siyo Rais wa nchi.
Hili sidhani kwamba litaishia kwa Ndugai tu, lazima itakuwepo safisha safisha.
 
Ubuyu wa Babu Issa.

Wazee wa taharuki mnajifanya kuyajua mengi sana kana kwamba nyie ndo wazee wa protocals za hao viongozi.

Tulieni, subirini meza kupinduka
 
Kwa kasi ya ukopoji ya mama na akili yake ilivyo ya kukosa kiasi kwenye hesabu za kukopa basi kufikia 2025 mama atakuwa kakopa kuliko maraisi wote toka raisi wa kwanza hadi wa tano combine maana mama kakopa til11 ndani ya miezi 9 tu tena inaonekana hiyo ndiyo aliyo bahatika kupata maana yake kama angepata zaidi hata til40 kwa mwaka angekopa ndiyo nikasema mama anaongoza nchi kwa kupractise upumbavu kukopa kuna mahesabu
 
My opinion anyway, there could be something fishy sported a far from presidentia advisory committee kumisslead Rais kwa manufaa yao, unajua hata mikopo inaweza kutumika kupata pesa za kupambania vita ya Urais 2025? Ni mtazamo wa kichokozi tu
Mikopo haikwepeki kwa sababu walioishika dunia wanalazimishia hilo.

Msipokopa leo, mnaua uchumi wa ulaya na majinamizi yanayotukamua.

Kikubwa mikopo itumike kwa usahihi na tuwe na open forums za kujadili mwenendo wa uchumi wetu.

Sasa Job alikuwa anatafuta milleage na tunajua kabisaa hana viwango hata vya kuwa mbunge.

Mtu anatoa boko kisha akimulikwa anakimbilia kichaka cha ukabila. Ni kufilisika kisiasa na kiakili
 
Acha chuki za wazi kwa Rais, je meko aliruhusu wengine kujipanga?nini kilimtokea Benard membe?Hili ni kwa viongozi wote wa Africa, ni dhuruma ngapi Ndugai alishiriki kuwatendea wengine awamu ya 5?, eti wabunge wachague moja kumpigia rais au spika kura ya kutokuwa na imani, kwa rais hicho ni kitu kigumu sana.Ila kama mama akitaka spika atoke anaweza, kwa siasa zetu hizi, ni dakika tu, kwani watu wanaangalia tu upepo!!huo sio mgogoro wa bunge na serikali bali ni Ndugai na serikali.
 
Hivi umesikiliza hatua kwa hatua alichoongea Ndugai?! Yaani badala ya yeye kuilaumu serikali lakini ametupa makonde yake kwa Samia personally, na wala sio kama taasisi!!
Upo sahihi.

Dhambi ya kupitisha tozo kandamizi inaanza na Job.

Wengine watafuatia
 
Mawaziri ni wasaidizi wake anahamua yeye nan hamteue nan hamuache
 
hili ni suala muhimu sana kama Taifa kulizingatia..Taifa limekuwa la siasa kila siku..Watu wanawaza urais muda wote..
Mkuu kwa vast of resources available on our motherland, tungekuwa na mijadala ya namna gani tukope kwa kuongezea uwezo bank za maendeleo ili Tz iwe major exporter basics consumable kwa Mozamboque, Malawi, Congo, Burundi, Rwannda, Uganda, Kenya, Madagascar ili kusisimua uchumu, kukuza ajira ili hata hao wanaosoma kwenye hayo madarasa wakitoka shule kuwe na avenue ya wao kuja kuwa producers.

Ila sana, mhhh.

Mungu tusaidie sana, kuna pahala akili yetu hatujaishughulisha vya kutosha.
 
Kwa katiba ya ccm ni ngumu kumpinga Mwenyekiti ana nguvu kuliko chama
 
Ndugai alipokuwa anasema watu watachagua Kati ya mikopo na kujibana bana kwenye uchaguzi wa 2025 alikuwa na maana gani?
 
Now you are back.
We missed you bro.

Hoja hii makini sana.

Samia ameshatishwa na tetesi zinazoenea kwa kasi hivyo ameona wacha aoneshe makali kidogo..
Wazee wakiondoka jukwaa linamiss hekima kubwa sana.....
Alilolifanya linaonyesha wepesi wa kihisia , sasa angeambiwa Idd Amini ame amevamia taifa ndio angeweza hiyo vita ya moto kama vita ya propaganda tu anashindwa kuhema?
 
Huna akili ndyg mnapenda kuwa na matumaini hewa yan mtu anaepokea report za ushushu toka tiss na mi ashindwe na huyo ndugai serious kabisa
 
Umeandika vizuri iwe musigazi (wewe mvulana).Nimeshakupa like
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…