Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Ndugai kafanya ujinga kuomba msamaha, speaker ni mtu mzito sana

Kitendo chake cha kuomba msamaha kimempa loop hole Bi. Tozo kumdhalilisha
2025 sio mbali, kwaalichoropoka spika ilikua nikumsagia kunguni mama then akaomba msamaha huku akijua lengo lake limetimia akiwa nauhakika mama hatakua nalakufanya kutokana naukubwa wake.

Hesabu zimepigwa vizuri sna kma ndugui atapotezwa mchezoni means Kuna timu imepoteza mchezeshaji muhimu sana

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Je ujunbe wa Ndugai una ukweli au hauna ukweli?
 
AH nirudi zangu kwetu Comoro naona mambo hapa kizungu mkuti
 
Unyoka wa Ndugai uko wapi?

Ule ujumbe wake?
Ni kama ujumbe a Assad tuu, uliomfanya aambiwe mjengo hauwezi kufanya kazi naye sababu aliuuita mjengo ni dhaifu, ni wakati sasa umefika naye ajitathimini kwa kauli yake no matter ilikuwa nzuri au mbaya kiasi gani.
 
Dalili mojawapo ya anguko la babiloni ni kuanza kupishana lugha wakati wa ujenzi wa mnara kwaiyo hii inaweza kuwa ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa chama kwa kuanza kuona dalili za kuwepo mgawanyo wa kweli wa madaraka miongoni mwa mihimili mikuu ya serikali. Mimi binafsi naichukulia ni afya kuelekea maendeleo ya kweli kwa taifa la Tanzania nikiona mgawanyiko miongoni mwa viongozi wakuu wa chama na serikali maana kwa miaka yote chama kinafaidika kwa gharama ya maendeleo ya taifa.
 
Hii misuguano inajenga loopholes kwa bakabaka kuingilia mtanange kama ilivyotokea zimbabwe, wawe makini sana.........wacha tusubiri hiyo cabinet reshuffle na jinsi ishu ya spika itakavyokuwa handled..........otherwise wanasiasa wanaweza kujikuta out of the game na tukaanza yale ya sudan.
 
Ni kama ujumbe a Assad tuu, uliomfanya aambiwe mjengo hauwezi kufanya kazi naye sababu aliuuita mjengo ni dhaifu, ni wakati sasa umefika naye ajitathimini kwa kauli yake no matter ilikuwa nzuri au mbaya kiasi gani.
Kama raia tuliungana na Asadi kumshambulia Ndugai kwa kitendo kile kwa nini isiwe sasa?
 
Kama raia tuliungana na Asadi kumshambulia Ndugai kwa kitendo kile kwa nini isiwe sasa?

Toa ushahidi wa ulipokemea Mkuu, na sasa acha iwe kama vile, Assad wa sakata hili naye akabidhi ofisi tubakie tunaugulia moyoni, au wewe unaonaje Mkuu?
 
Kwa nini iwe sasa na hakufanya hivyo wakati nchi inakopa 29 t ndani ya miaka 5?.Miradi imeachwa bila kukamilika na tayari imekula matirion ya mkopo,je,itelekezwe hapo ilipo au tukope tuikamilishe ili iweze kuzalisha pesa za kulipa?.
 
Hiyo siyo nguvu ya sukuma gang huo ni upumbavu wenu wenyewe nguvu ya sukuma gang ipo kwa wananchi na wazalendo waliopo serikalini huyo zuzu ndungai sisi atumtambui hata kidogo ,
usirudie tena kuhusisha wananchi na hayo maugoro ya push gang.
 
Ubuyu wa Babu Issa.

Wazee wa taharuki mnajifanya kuyajua mengi sana kana kwamba nyie ndo wazee wa protocals za hao viongozi.

Tulieni, subirini meza kupinduka
Imani kubwa aliyonayo ndugai ni kwamba uma wa watanganyika unamkubali sana, nitakupa mfano kipindi yamependekezwa Majina kwaajili ya umakamu wa Rais, na lakwake lilikuwemo yaani mbali na Dr Phillip Mpango na Komredi AbdulRahman kinana, yeye akaamini ataupata umakamu kwasababu anakubalika zaidi kwa jamii kuliko hawa wengine

Hivyo hata huyo ndugu uliyembeza sijaona kosa lake madhali kaisimamisha hoja yake vyema, Ndugai hakukurupuka kuzungumza hadharani tena kupitia lile jukwaa alilochagua, na kwa aina ya chama alichopo, sikumbuki lini kiongozi wa Muhimili alimnyooshea kidole kiongozi wa muhimili mwingine basi Rais kwamba Uongozi wake unaweza kuipeleka nchi kupigwa mnada, labda wewe unikumbushe, ni wazi Ndugai alikwisha Sema na nafsi yake, jamaa zake na wasiri wake kabla ya kuwasilisha maoni yake kwa uma


Haja ya kuwa na spika asiye na Chama ipo na haikwepeki.

Lakini tatizo kubwa sana sana ni kitu hiki TABAKA LA WATAWALA

Tuiondoe hiyo kwanza
Kwanini?
 
Swali bado ni lile lile kwenu, Samia yeye hana akili ya kujia hili ni sawa hili si sawa? Kwa hiyo ikitokea siku wakamuandikia Tanzania haina raisi, atasoma tu Kama ilivyo?
 
Toa ushahidi wa ulipokemea Mkuu, na sasa acha iwe kama vile, Assad wa sakata hili naye akabidhi ofisi tubakie tunaugulia moyoni, au wewe unaonaje Mkuu?
Mkuu! Kwani hukuona Asad alivyoitwa majina mazuri mazuri kwa ujumbe wake ule?

Sasa kwanini huu wa Ndugai tunaupiga teke?
 
Tuendelee kupiga magoti na kusali Amaleki anakaribia kuaga umati. Spika alikuwa na mapungufu mengi, ubabe, hata alivyo handle issue ya lissu kupigwa risasi bungeni.

Sikuwahi kujua mungu atampatia stahiki yake kwa style hii. Na gods time is always the best.

Sakata hili la kugongana kwa mihimili linaweka bayana umuhimu wa katiba mpya bila kelele wala vipigo.

However lazima kutakuwa na built in consequences kutoka mhimili wa bunge lazima effect zake zitakuja kujionesha waziwazi.

Mtumishi Alphonce Temba, Marehemu Sheikh Yahya Hussein, walitabiri ujio wa Katiba mpya rasimu ya warioba sio pendekezwa ya makada wa kijani. Hope by 2026 tutakuwa na kitabu mezani maana mazingira au nature imeanza kujiandaa.
 
Mimi naona hadi sasa tatizo ni kati ya watu na sio kati ya taasisi. Wabunge wapo walivyo ... Taasisi ya ccm ipo dhidi ya Ndugai na si against bunge.
 
Simpendi Sana Ndugai.Ni spika wa hovyo Sana tangu tuanze kuwa na bonge la vyama vingi.Anaendesha bunge kibabe na hujaribu kuua au kuzima hoja zote asizozipenda yeye binafsi.Bunge la Ndugai limegeuka kuwa taasisi ya kubariki kila kitu kutoka serikalini na ni vigumu kulitofautisha na caucus ya Chama cha mapinduzi!!

Pamoja na huu mtazamo wangu hasi kwa Ndugai na Bunge lake kwa ujumla lakini nikisoma hii nukuu ya alichokisema naona kwakweli umemtafsiri vibaya.Ukifuatilia mtazamo wa Ndugai huko nyuma kuhusu tozo,utaona kwamba anaunga mkono tozo moja kwa moja na anaona ikiwepo tozo nchi itaondokana na kukopa na hivyo kujiendesha yenyewe.Ukimsoma hapa anakazia mtazamo wake huo kuhusu tozo na mikopo.Anawaambia hao 'wasomi' umuhimu wa tozo na kwamba baada ya kupunguza tozo kutoka kwenye mafuta na miamala sasa Rais analazimika kukopa Ili mambo yaende.Kwahiyo an
naonya kama mtaamua kuwatoa hawa(kwa sababu ya tozo) na kuweka wengine 2025(ambao watakuwa hawana tozo kabisa ila wataendelea kukopa) basi itafikia mahala nchi itapigwa mnada.

Kwahiyo hajamsema Rais.Anawasema watu wanaopinga tozo na hapohapo wanataka maendeleo na nchi iweze kujitegemea.Anawauliza inawezekanaje?Kwahiyo anamsaidia Rais kuelimisha uma umuhimu wa tozo na kwamba kipi kitatokea endapo zitakuwa hazipo.Kwamba kama wanataka basi wawatoe hawa wa tozo 2025 na waweke wa mikopo,wakope mpaka nchi ipigwe mnada.

Kwakweli ametafsiriwa vibaya na sijajua watu ni chuki tuu kwa Ndugai ndo wanajifanya hawaelewi hoja yake au ni kweli hawaelewi.Ningekuwa mimi ni Ndugai ningejiuzuru baada ya kujua kuwa hata Rais nae hajaelewa hoja yake au labda ameelewa vizuri kabisa ila nae ameamua kutumia mwanya huohuo kumuangusha kisiasa.Ajiuzuru kwakuwa amejua Rais hampendi na amemuweka kwenye kundi la wanaompinga ndani ya Chama chao.Chochote atakachofanya au kusema Rais atakiangalja kwa jicho la uadui.Kwakweli anapaswa kujiuzuru kwakuwa haiwezekani tena kufanya Kazi na Rais mwenye mtazamo huo kwake kama spika wa bunge.

Asimame aufute ule msamaha aliouomba(kwa nia njema kabisa ya kujishusha kwa Rais wake hata kama hakumuelewa) ajiuzuru nafasi yake kwa kueleweka vibaya ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya ....(Ila ni kwa makusudi)!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…