Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usije kujitetea kuwa sikukuambia, narudia tena, nikikata moto nizikwe hapa hapa mjini. Sitapendezwa kabisa kuwa mbali na ile mitaa yetu pendwa.Siyo kosa kusafirisha mwili wa mpendwa wako, lakini siyo suala la kufa na kupona.
Maana hilo si jambo la kiibada kwa hizi dini zetu kubwa.
Kusafirisha mwili ili kumzika alikozaliwa kuna kiasi furani cha upagani.
Maana baadhi ya mira za kiafrika makaburini ni sehemu ya kufanyia IBADA (Maombi).
Kwahiyo baadhi ya makabila yetu hupenda ukaribu na wafu wao ili wasipate usumbufu wakati wa matambiko.
Hahaha, nitazingatia Wosia wako mkuu.Mkuu usije kujitetea kuwa sikukuambia, narudia tena, nikikata moto nizikwe hapa hapa mjini. Sitapendezwa kabisa kuwa mbali na ile mitaa yetu pendwa.
Nakutunuku shahada ya heshima ya udaktari katika nyanja ya ushauri,honorary causa .sasa wewe ni Dk Sky EclatKuwapeleka watoto vijijini kuna faida nyingi tusizozielewa. Licha ya kujua maneno ya kilugha, watajua ndugu, mila na desturi.
Pia watakwenda shambani na kuona kilimo cha mazao kinavyofanyika. Hili linapanua upeo wao ki elimu. Watoto wa mijini hawajawahi kuona nanasi likiwa shambani.
Watoto wa mijini wengine hawajawahi kuona milima. Ukipita Uruguru pale unawaonyesha watoto milima ya Uruguru na kuwaambia kuwa hii ni mfano ya milima meza kama ya Usambara.
Tutafika mahali tutakua tunachoma na kupeana majivuWatoto ambao hawajazoea kwenda kijijini wanakomaa wazazi wazikwe Dar.. sabab wanaona usumbufu kwenda mkoani kusafisha kaburi ama kuombea wazazi wao makaburini kila baada ya muda..
Pongezi nyingi kwa wachaga.. kwa kuzoesha watoto kwenda moshi mara kwa mara
Hao wazazi wambie wawe wanaacha na nauli ya kusafirishia!Je, kuna umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo? Unawapelekaga watoto wako?
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania;
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikishuhudia matukio mengi sana zaidi ya mara 4 katika misiba niliyopata kuhudhuria ambapo watoto waliozaliwa mijini (1980's - 1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kusababisha mpasuko wa mahusiano ndani ya ukoo.
Kwa hapa Tanzania, makabila yetu yamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kuna makabila ambayo kuzika mtu kwao sio jambo la maana sana kiasi kwamba hata ukifia Magomeni wao kukuzika makaburi ya Kinondoni ni kawaida tu.
Kundi la pili ni yale makabila mbayo ni mwiko kabisa kuzika mwili wa ndugu yao nje ya kijiji. Yaaani kama mtu alifia Dar, basi ni lazima asafirishwe mpaka mkoa wa Mara, tena akazikwe katika makaburi ya ukoo.
Hata kama mtu amekufa tuseme huko Ulaya, basi ni lazima aletwe kutoka huko New York mpaka Rorya hukoooo Shirati au Utegi. Juzi hapa nilienda katika msiba mmoja hapa jirani na nilipopanga wa watu wa kabila moja la huko Mkoa wa Kigoma.
Katika msiba huu ndio ninakutana na hiki kisanga cha watoto 3, ambao financially wapo njema sana na mmoja wao ni Country Manager wa kampuni moja ya wazungu huku Dar tena ni mtoto wa kiume.
Sasa wakuu ninaomba kujua chanzo kikuu ni nini? Je, ni wazazi wenyewe kutopenda kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo ya mwaka ili wajuane na mazingira pamoja na ndugu zao wa huko au shida ipo wapi hapa wakuu?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wengine wazazi wamezaliwa mkoa A wakafanyia kazi Mkoa B+C tukazaliwa+kukulia mkoa C ambapo wazazi wanaishi mpaka leo then sisi tunafanya kazi+kuishi mkoa D na tumezalia huku ...hao watoto tutawapeleka wapi hiyo likizo ?wakati kijijini kwa wazee ni mkoa A ambapo dingi mwenyewe haendagi ila Mara chache sanaJe, kuna umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo? Unawapelekaga watoto wako?
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania;
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikishuhudia matukio mengi sana zaidi ya mara 4 katika misiba niliyopata kuhudhuria ambapo watoto waliozaliwa mijini (1980's - 1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kusababisha mpasuko wa mahusiano ndani ya ukoo.
Kwa hapa Tanzania, makabila yetu yamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kuna makabila ambayo kuzika mtu kwao sio jambo la maana sana kiasi kwamba hata ukifia Magomeni wao kukuzika makaburi ya Kinondoni ni kawaida tu.
Kundi la pili ni yale makabila mbayo ni mwiko kabisa kuzika mwili wa ndugu yao nje ya kijiji. Yaaani kama mtu alifia Dar, basi ni lazima asafirishwe mpaka mkoa wa Mara, tena akazikwe katika makaburi ya ukoo.
Hata kama mtu amekufa tuseme huko Ulaya, basi ni lazima aletwe kutoka huko New York mpaka Rorya hukoooo Shirati au Utegi. Juzi hapa nilienda katika msiba mmoja hapa jirani na nilipopanga wa watu wa kabila moja la huko Mkoa wa Kigoma.
Katika msiba huu ndio ninakutana na hiki kisanga cha watoto 3, ambao financially wapo njema sana na mmoja wao ni Country Manager wa kampuni moja ya wazungu huku Dar tena ni mtoto wa kiume.
Sasa wakuu ninaomba kujua chanzo kikuu ni nini? Je, ni wazazi wenyewe kutopenda kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo ya mwaka ili wajuane na mazingira pamoja na ndugu zao wa huko au shida ipo wapi hapa wakuu?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Sawa mkuu...Tatizo watu huko baadhi ya vijiji wamekua walozi sana hasa kwa ndugu
Very complicatedWengine wazazi wamezaliwa mkoa A wakafanyia kazi Mkoa B+C tukazaliwa+kukulia mkoa C ambapo wazazi wanaishi mpaka leo then sisi tunafanya kazi+kuishi mkoa D na tumezalia huku ...hao watoto tutawapeleka wapi hiyo likizo ?wakati kijijini kwa wazee ni mkoa A ambapo dingi mwenyewe haendagi ila Mara chache sana
aisee noma...watu wanafanya zao mishe huko mijini wameligundua na kuanza kuzitenga familia zao na vijiji vyao....
Kuna rafiki yangu naye yuko njema kifedha, katokea hukohuko Kigoma. Aliwahi kuniambia amemaliza miaka 15 hajawahi rudi huko. Nilibaki kumshangaa tu.Kigoma hao in spesho case. Wanaogopa kupigwa 'mitama' na majirani was huko kwao. Kipapai
Kuna baadhi ya watu bado wanaamini mambo ya kurogana?...Wengi wa watu huko vijijini wanaamini kuwa watu wa mjini wameyapatia maisha lakini hawawasaidii,hivyo kuamua kuwaloga na kuleta usumbufu na matatizo kwenye hizo familia