Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Watoto hawana mazoea ya kwenda kijijini, msiba upelekwe kijijini, nani akaratibu hizo shughuli za mazishi??

Anayeacha maelekezo akifa akazikwe kijijini aache na nauli kabisa ya kumpeleka huko.

Besides, wakishamzika, wao na vizazi vyao hawarudi huko tena, yaani ndiyo nitolee. Bora azikwe mjini, manispaa itasafisha mazingira ya nyumba yake ya milele.

Everyday is Saturday................................😎
 
Mkuu usije kujitetea kuwa sikukuambia, narudia tena, nikikata moto nizikwe hapa hapa mjini. Sitapendezwa kabisa kuwa mbali na ile mitaa yetu pendwa.
 
Mkuu usije kujitetea kuwa sikukuambia, narudia tena, nikikata moto nizikwe hapa hapa mjini. Sitapendezwa kabisa kuwa mbali na ile mitaa yetu pendwa.
Hahaha, nitazingatia Wosia wako mkuu.
Nadhani makaburi yale Chang'ombe (Wailes) au ya Unubini yanatufaa.
Ikishindikana basi tupelekwe Kisutu au Kinondoni.[emoji120][emoji120]
 
Nakutunuku shahada ya heshima ya udaktari katika nyanja ya ushauri,honorary causa .sasa wewe ni Dk Sky Eclat
 
Infantry Solder mdogo wangu pamoja na umri wako mdogo lakini unatoaga mada fikirishi za kujadili.
Mtu asikudanganye kupenda kwenu ni maendeleo. Chunguza makabila yasiyopenda kwao hata maendeleo yao yanakuwa hafifu sana. Wazungu ndio maana hata akija Tanzania akifa anapelekwa kwao mwili ukishindikana hata akichomwa moto majivu yanapelekwa kwao.

Mila za kabila flani mtoto akizaliwa hata azaliwe Marekani kitovu kikikatika kitapelekwa hadi kijijini kinachimbiwa ndani ya nyumba hizi ni mila siwezi kujadili.Utakuja kuona makabila yasiyopenda kwao kunakuwa na sababu moja wapo kwa vile kwao hakuna hata nyumba mtu anaona aibu kumpeleka mzazi wake maana atachekwa jinsi kulivyo na hali mbaya.

Maendeleo ya wachaga sio bure ni shauri ya mila hizi za kupenda kwao mkataa kwao ni mtumwa.Ukipata watoto usipowapeleka kwao wanapoteza identity ya kujua asili yao na kujua mila zao ni kweli nakiri tumebadilika lakini nyumbani ni nyumbani tu.Makabila mengine ushirikina unawarudisha nyuma mno kiasi cha kuogopa hata kuzikwa kwao

Moja ya kuzika nyumbani ni alama kwa mfano mkoa wa Kilimanjaro ardhi ni haba sana mtu anapozikwa kwenye shamba lake hata vizazi vya nne vinapopatwa na matatizo ya ardhi kudhulumiana makaburi yanatumika kama beacon ya utambulisho kuwa hapa palikuwa kwa nani.

Hata vitabu vya dini Yakobo alivyofariki mwanaye Yusuph alimpeleka kumzika kwao nchi ya ahadi.
 
Tutafika mahali tutakua tunachoma na kupeana majivu

Hizi abudu za makaburi na mashirikina mengine zinauwawa na muendelezo wa evolution na globalization
 
Hao wazazi wambie wawe wanaacha na nauli ya kusafirishia!
 
Kwtu ni muhimu nasisitiza kuzikwa nje ya makaburi mababu ni sawa na kutupwa porini. Wazungu ndio kielelezo cha kuzikwa makwao hata kwa kuchomwa na kulekwa majivu.naona wajumbe wengi wanashauri watu wajiwekee kabisa pesa za kugaramia usafiri wa kupeleka miili yao pindi watakavyokufa ili waliobakia wasisumbuke. Wazungu hufanya hivyo kabla ya umauti wao
 
Wengine wazazi wamezaliwa mkoa A wakafanyia kazi Mkoa B+C tukazaliwa+kukulia mkoa C ambapo wazazi wanaishi mpaka leo then sisi tunafanya kazi+kuishi mkoa D na tumezalia huku ...hao watoto tutawapeleka wapi hiyo likizo ?wakati kijijini kwa wazee ni mkoa A ambapo dingi mwenyewe haendagi ila Mara chache sana
 
Kwa mujibu Wa Dini ya kiislam mtu atazikwa alikofia.Hao wamefuata Sunna hakuna haja ya kuingia gharama ya kusafirisha maiti.
 
Tatizo watu huko baadhi ya vijiji wamekua walozi sana hasa kwa ndugu,na watu wanafanya zao mishe huko mijini wameligundua na kuanza kuzitenga familia zao na vijiji vyao....

Wengi wa watu huko vijijini wanaamini kuwa watu wa mjini wameyapatia maisha lakini hawawasaidii,hivyo kuamua kuwaloga na kuleta usumbufu na matatizo kwenye hizo familia... na mbaya Zaidi hata ukitokea msiba na watoto wakapeleka vijijini basi hao ndugu walozi kwenye hasira nao hutumia nafasi hiyo kuwaangamiza.

Sababu nyingine in uwepo wa dini umefanya hizi mila zionekane hazina umuhimu pia uwepo wa elimu umeonyesha kuwa kusafirisha in gharama zisizo na msingi...hivyo tunazika tu Kinondoni.

Hizo sababu nilipewa na bàadhi ya watu kwa kujaribu kuuliza swali kama lako.
 
Very complicated

Uzuri mkoa A kuliko nyumbani unakujua, ni wewe kusuka ama kunyoa
 
Mtu amekaa Mkoa A miaka na miaka. Watu "wote" wanaomfahamu wako mkoa A. Kule kwao mkoa B "hakuna" anayemfahamu. Akifa kwa nini apelekwe kijiji cha mkoa "B"? Hata babu yake hakuzaliwa kijiji cha mkoa "B", utakuta na yeye alihamia.
 
Wengi wa watu huko vijijini wanaamini kuwa watu wa mjini wameyapatia maisha lakini hawawasaidii,hivyo kuamua kuwaloga na kuleta usumbufu na matatizo kwenye hizo familia
Kuna baadhi ya watu bado wanaamini mambo ya kurogana?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…