Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Huwa nashangaa unakita familia wasomi kabisa complain ya kwamba marehemu alisema kwamba akazikwe kijijini, hizi zote ni tamaduni kwa mtu mwenye exposure anafahamu kabisa kwamba hakuna tatizo lolote hata akizikwa wapi! Ni Imani potofu ndio zitakwambia kwamba eti msipomzika mahali aliposema kuna mambo yatatokea, ukiamini hivyo basi ndio upeo wako upo hapo etc
Sawa mkuu
 
Sio kuwapeleka watoto nyumbani likizo. Kama bado una wazazi wako baba, mama, mashangazi, wajomba, n.k unaowaamini au ambao walikulea na wewe na bado wapo kijijini, peleka wanao wakasomee huko angalau elimu ya msingi tu alafu watoe waendelee na elimu zingine huku mjini. Hii itawafanya sio kujua nyumbani bali kuwa sehem ya jamii ya kwenu. Pili watapapenda sana kwa moyo wao na watakuwa wanataka wenyewe kwenda na sio kuwalazimisha kwenda kwa sababu wana moments nyingi sana za kukumbuka huko nyumbani, wana marafiki waliokua nao huko tangu utotoni, n.k. Lakini pia unawafungulia nafasi ya fursa nyingine nyingi kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kurudi kijijini kutumia fursa zilizopo ukizingatia mijini kumeshakuwa congested na fursa nyingi ziko occupied. Mfano mtu anaweza kurudi kijijini kugombea hata nafasi za kisiasa kama udiwani, ubunge, n.k na bado akafanikiwa maana anatambulika na jamii yenyewe.

Lakini pia watoto wakikulia kijijini wanakuwa warithi wa boma na mashamba yenu na kuyaendeleza. Mfano mzuri mimi niliacha kazi Standard Chartered Bank mwaka 2015 nikarudi kijijini nikapewa mashamba na babu nikaanza kilimo na sasa nimepiga hatua na nimefungua kampuni ya masuala ya kilimo. Babu alinipa mashamba nikalime kwa kuwa nimekulia kwake na anaona kabisa baba yangu na baba wadogo wameshalowea mjini hawawezi kurudi kukaa tena kijijini. Sasa babu ameshafariki mimi ndio jicho la ukoo mzima maana baba na baba wadogo wote na familia zao wakija wanafikia kwangu na hata wao kama Mungu akiwachukua wana uhakika familia yetu ina mtu wa kuendeleza heshima yake pale kijijini japokuwa watoto wao wengine hawataki kukaa kijijini ila wanapendaga kuja kwa ajili yangu.

Watoto wakifanikiwa kurudi kijijini hata nyie wazazi mnakuwa na hamu ya kwenda kijijini.

N.B: Japokuwa kila jambo lina faida na hasara zake na ndo maana wengi hamko tayari kupeleka watoto wenu wakalelewe na wazazi au ndugu zenu kwa kufikiria ndo kuwapenda sana, ila pia ina faida sana kwa upande mwingine na kwa baadae.
 
Mimi nikifa wanizike popote , yanini kusumbuana eti nisafirishwe na gharama zote nikazikwe sijui kwetu, nini italeta tofauti? Je nitafufuka. Nikifa nizike tu hapo hapo.
 
Mimi nikifa wanizike popote , yanini kusumbuana eti nisafirishwe na gharama zote nikazikwe sijui kwetu, nini italeta tofauti? Je nitafufuka. Nikifa nizike tu hapo hapo.
Wazazi wako nao walizikwa popote? Haufurahii kuona makaburi yao?
 
Wazazi wako nao walizikwa popote? Haufurahii kuona makaburi yao?
Wazazi wangu wako hai kwa uwezo wa Mola. Hakuna uhusiano kati ya walio hai na waliokufa unless kama wewe unaabudu kwenye dini zetu za asili.
 
Wazazi wangu wako hai kwa uwezo wa Mola. Hakuna uhusiano kati ya walio hai na waliokufa unless kama wewe unaabudu kwenye dini zetu za asili.
Mi naamini katika dini zetu za asili of course, ila hata kikawaida kuona mahali walipopumzika ancestors wako ni jambo jema sana, na kuhudumia makaburi yao ni baraka pia mkuu
 
Mi naamini katika dini zetu za asili of course, ila hata kikawaida kuona mahali walipopumzika ancestors wako ni jambo jema sana, na kuhudumia makaburi yao ni baraka pia mkuu
Mimi nikifa nimeufa tu wanizike na wasahau tu labda kama nimeacha kampuni kubwa na huduma za kama hospital na mashule yata keep my legacy and my name living.
Ukifa umekufa tu kwanini wahangaike na mimi sijui kujengea kaburi sijui kunilimia what for?
 
Wazazi wako wakifa hauoni umuhimu wa kuwasitiri mahala pa usalama kuliko kuwazika makaburini huko ambapo baada ya mwaka watafukuliwa wakazike wengine??

Je wewe hautafurahi kuwa utakuwa unaona makaburi yao na kuwa ukumbusho kwa maisha uliyoishi nao na yote waliyokutendea??
 
Wakifa tutawazika walikozaliwa sehemu ya makaburi ya familia. Ila kuna zuri lipi kwa kutazama makaburi? Kama kumbukumbu ninazo picha na taswira za mema waliyonitendea kwa kipindi chote.
 
Ukweli utabaki pale pale, hakuna mtu atajenga makaazi ya kuridhisha na kuweka mazingira safi kijijini kwao alafu asiwe na tabia ya kuwapeleka watoto wake au yeye kwenda kijijini walau mara moja kwa mwaka, wasiokuwa na tabia ya kwenda kijijini mara nyingi hata mazingira hawajandaa vizuri. Nimejifunza kwa Wachaga na Wahaya, ukweli hawa watu utamaduni wao unaendana wote wanajitahid sana kutengeneza makwao vijijini ndiyo maana walio wengi wanazikwa kwao na pia wanatabia za kuwapeleka watoto kwao. Hapa wengine wanasingizia mara vijijini watu wachawi nk kumbe mtu kashindwa kupaendeleza kijijini kwao
 
Back
Top Bottom