Mtoto wa Jirani amezoea kuniita baba

Mtoto wa Jirani amezoea kuniita baba

Kama ni katoto ka kike acha kabisa mazoea nako.

Siku hizi kuna upuuzi Sana unaibuka kupitia hawa watoto.
 
Kuna Jirani yangu ana mtoto wa miaka mitano ni wa kike.

Ni mtoto muongeaji afu ni mchangamfu Sana, tumezoeana Sana nikirudi kwenye mishe mishe au nikienda dukani lazima nibebe zawadi kwa ajili yake.

Shida mtoto ameanza kuniita baba na akiulizwa na mtu baba Yuko wapi ananionesha mimi.

Je, wakuu sio tatizo kuwa karibu na mtoto huyu nisije kuwa chanzo ndoa za watu kuvunjika

Nb: Baba yake mtoto anafanya kazi nje ya mji anakuja likizo na wikiend Mara mojamoja.
Haujaeleza yote
Tuambie mara ngapi unasneak kwao kumsalimia mama ake?

Sisi watu wazima humu, tutaficha siri.

Au siyo Depal ?
 
Daah, mimi wako watoto wawili, wote mabinti, yaani wakiniona tu kanisani huwa wanakuja mbio kunikumbatia na hawataki kukaa na mama zao, mmoja hadi aliandika jina langu shule kama baba yake, waalimu ilibidi kumpigia mama yake kuuliza! Bahati nzuri mama aliachana na baba ila mawasiliano ya kulea mtoto yapo, hakuna na wala hayatakuwepo mahusiano yoyote na mama mtoto!
 
Hizo habari nishazipata kwa taarifa yako..kwanini unajipendekeza kwa mwanangu?

Nikija hapo mtaani sitokuacha salama..seriously
 
Sisi tuliolelewa na kukulia mazingira ya kota late 80s tulifundishwa kuwa treat wazazi wa watoto majirani kama baba\mama na hadi leo hii na ukubwa wangu huu nikienda pande hizo au kubahatika kukutana na wazee hao huwaita baba/mama kwa moyo mkunjufu kabisa.
Haya mambo ya anko na anti yamekuwa yakitumika miaka hii ya 2000s kutokana na uzungu kutamalaki.

Hivyo kwa mzazi muungwana na mwenye uelewa hawezi kutilia shaka mahusiano ya wewe na huyo mto na hata mama yake pia.
Kingine kosa lipo kwa huyu jirani yako kukaa mbali na uwepo wa mwana imemjengea mtoto kukuthamini kama baba kutokana na vile unavyomjali na kuwa karibu nae.
Mkuu asante sana umenikumbusha mbali sana, zamani mimi nilijua watu wote pale kijijini ni ndugu zetu tuna maana ilikuwa baba(tata),bamdogo,bamkubwa,shangazi,babu na bibi.
Baada ya kuwa mkubwa ndo nikaelewa
Kwa kesi ya mwenzetu kulingana na mazingira ni pagumu kidogo kwakweli,baba angekuwepo sawa
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
Maana kila thread ya mada za kijinga sijui niite hivyo lazima nikute ni yeye. Na kajiunga tu mwaka jana, mpaka huu mwaka uishe servers zitakua zimejaa balaa
1.Kumbe Kuna Wana Jf wananifuatilia sikujua Hilo.😂
2.Npo Jf tokea mwaka 2015 Ila kujiunga nimejiunga mwaka Jana kuwa na ID.
3.Acheni makasiriko tumejuana Jf kwa id fake so relax
 
Daah, mimi wako watoto wawili, wote mabinti, yaani wakiniona tu kanisani huwa wanakuja mbio kunikumbatia na hawataki kukaa na mama zao, mmoja hadi aliandika jina langu shule kama baba yake, waalimu ilibidi kumpigia mama yake kuuliza! Bahati nzuri mama aliachana na baba ila mawasiliano ya kulea mtoto yapo, hakuna na wala hayatakuwepo mahusiano yoyote na mama mtoto!
Kuna time ni nyota tu zinaenda,ata sis tukiwa wadog Kuna mabrother zetu tuliwapenda kuwa nao krb
 
Back
Top Bottom