Mtoto wa kaka yangu wa kwanza (First born) amebamiza 'A' za kutosha za darasa la nne mpaka nimeogopa sana, tutafute pesa Elimu nzuri ni gharama

How old are u?
 
Kwa nini usiwachukue wewe hao div 3,4,0 halafu uwafundishe waje kupata div 1?
Shule gani makini inataka failures? Uliona wapi mtoto wa div 3, 4 anapelekwa kibaha, mzumbe, ilboru?
Uzuri nimesoma nao chuo hao wa hizo shule nzuri na walikuwa vizuri tu na hata makazini nimekuwa nao tena kwenye MNCs na INGOs na wapo wanafanya vizuri
Hivyo hayo uliyoandika hapo ni chuki binafsi na maneno ya mkosaji
Usiwe hasi na kuwa na chuki zisizo na msingi
 
Ni aibu kwakweli
 
Umejuaje kama atakwenda UDSM? Mzazi wake anaweza kumpeleka chuo kingine nje ya nchi.
Hawa wengi waokitutumua na EM za 1,2,3m ambao muda wa ada ukifika wanapata stress hawawezi kupeleka mtoto akasone nje baada ya A level. Hawa wanaishia kugombea hela ya HESLB kama waliotoka Kayumba tu. Tena kwasababu walisota kusomesha wanakuwa wakali kweli wakipata boom asilimia ndogo.
 
Kusema ukweli ambao Huwa wanasifia shule za serikali Huwa nawaona kama matahira na mazezeta.Mtu yeyote mwenye uwezo huwezi kumkuta mtoto wake kwenye hizo shule.Mfano mtoto wa mfanyabiashara mkubwa kama mo dewj,gsm,mkurugenzi,afisa elimu,mkuu wa wilaya na mkoa ,waziri na rais huwezi kumkuta mtoto wake anasoma hizo shule japo kuwa wewe kapuku anakuhamasisha upeleke mtoto wake huko.Umasikini tu ndiyo huwafanya wajinga wajifariji kuwa shule za kayumba ni nzuri.
 
Siye tunapamba watoto wapate D mbili tu kidato cha pili waende kidato cha tatu na wakifika kidato cha tatu tunawambia unataka kuwa nani wakisema ndoto zao tunawambia kazana sasa masomo haya upate D nne, wakilata hizo D nne animaliza tunampeleka VETA uko sasa baada ya miaka mitano hao watoto wenye A nyingi wanaanza tubembeleza kufanya kazi kwenye makapuni yao tena mpaka tickets ya ndege wanatuma njoo bwana mtambo umegoma uku
 
Tangu lini mfanya biashara wakajua thamani ya shule mzee, watoto wanasoma nakutoboa ni watoto hawa wakimaskini IQ kubwq shule hizi hizi za kata tunapambana kibishi tunakutana nao kwenye makorido ya vyuo vikuu na badae kwenye maofisi tunagonga nao cheers
 
Yaani mfanyabiashara hajui thamani ya elimu?labda kama unaongelea wachuuzi ambao Bado mitaji Yao haijawa mikubwa.mfanyabiashara anayejitambua anamsomesha mwanawe ili aje kuendeleza zaidi biashara ili kufikia kiwango cha kimataifa na siyo kuajiriwa ili ulipwe ujira wa milioni Moja au mbili.wanaotafuta ajira hizi za laki saba ,milioni au milioni mbili ndiyo hao Sasa wanaotokea kayumba schools
 
kujiliwaza tu
m
 
Mkuu umeelezea vizuri sana, hapa LIKUD amepigwa KO
 
Ndo maana ya kuletwa hela sasa, it's capitalism bro
Tukubali dunia imebadilika sio kila kitu utafanya wewe mzazi na haushindi 24hr na mtoto wako, toa hela watafill gape ambayo kwa namna fulani hutaifill
Ni sawa lakin huo sio mfumo sahihi wa malezi
 
Wadogo zako primary wanasoma English medium, baada ya hapo ni Serikalini.
Mpango wako kama wa kwangu tu.
Primary pekee ndio watasoma e.medium

Nina rafiki yangu primary alisoma Alpha sekondari akasomeshwa Benjamin ilinishangaza sana.
 
Mpango wako kama wa kwangu tu.
Primary pekee ndio watasoma e.medium

Nina rafiki yangu primary alisoma Alpha sekondari akasomeshwa Benjamin ilinishangaza sana.
Usishangae, huwa tunakua na sababu zetu wazazi kama ambavyo na wewe utakua na sababu zako. Mfano mpango wangu ni kama wako ila sababu zetu zinaweza kuwa tofauti kabisaa
 
Mm pia Binti yangu kang'oa div 1 point 10 matokeo ya form 2 na yupo kayumba secondary school
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…