Mtoto wa Magige Nyerere afariki katika ajali ya gari Shinyanga

Mtoto wa Magige Nyerere afariki katika ajali ya gari Shinyanga

Labda nikuulize maana wewe ni bwege sana! Wakati wa vita na Nduli Idd Amin jeshi la wananchi wa Tanzania tulikuwa hatufuki hata 5000 mimi nikiwa mmojawapo wa wanajeshi. Na kule kwenye vita yaani mstari sa mbele hatujufika hata 3000 tulioenda kupigana hadi kumng’oa na kumkimbiza Nduli toka ardhi ya Tanzania na Uganda! Hao watu elfu 20 walitokea wapi? Nijibu hapa maana wewe inaonekana unakunywa pombe aina ya ‘pingu’ ambayo kabla hujaanza kunywa lazima ufunge pingu suruali juu kidogo ya magoti ili kuzuia mzigo!
Ana msongo wa mawazo mkuu,mpotezee.
 
Nyerere analipwa .
Kusababisha Watanzania zaidi ya elfu 20 kufa kule Uganda pasi na sababu za msingi unadhani MUNGU atafurahia uzao wako?
ACHA chuki mkuu,Ina maana mwalimu angetuacha sisi wa mkoa wa Kagera chini ya Idd Amin! Najua utasema Nyerere alimprovoke Amin Sababu ya urafiki wa mwalimu na Obote,lakini sasa Amin alishavamia (Actus reus) na mens Rea ilikuwepo kwamba alitaka kuipora Kagera.Kama mwalimu angemuappease Amin bado Amin angetaka zaidi.Je,kosa la mwalimu liko wai hadi alipiziwe kisasi? Mautii ni mauti na hakuna kisasi
 
Pole nyingi kwa familia ya ya mwalimu nyerere, pamoja nao tuna sikitika sana!

Kwa vile uhai na umauti ni nje ya uwezo na matakwa ya kibinadamu , hatuna la zaidi ila kushukuru na kumuombea pumziko lenye amani .
 
Chief Nyerere amefariki katika ajali ya gari usinu wa kuamkia leo Jumamosi.
Amefariki hospitali baada ya juhudi za kuokoa maisha yake kushindikana.
Ajali imetokea Shinyanga ambako Chief alikuwa anafanya kazi.
Hii ni fatal crash nyingine kabisa.
Ijimaa iliyopita tumemzika Daudi Nyerere,mtoto wa Makongoro Nyerere na sasa,siku saba baadaye,Ijumaa usiku,Chief amefariki katika car crash. Magige Nyerere ni kaka yake Makongoro Nyerere.
Kwa hiyo sasa ni wajukuu wa Mwalimu Julius Nyerere wawili ambao wamefariki katika car crash.
Again,hii ni ajali tofauti. Siyo ile ya Daudi Makongoro Nyerere.
Makongoro Nyerere na Magige Nyerere wote ni watoto wa Mwalimu Nyerere.
We will update this.
chief ni jina lake au cheo
 
Nyerere analipwa .
Kusababisha Watanzania zaidi ya elfu 20 kufa kule Uganda pasi na sababu za msingi unadhani MUNGU atafurahia uzao wako?
😭😭😭😭😭 Jaman vita ile Bora ingekua ikifikaga maadhimisho yake wasiituonyeshe kumbukumbu ya kilichotokea maana ni maumivu tu wanatups inamaana wazee walikufa kivile.
 
Chief Nyerere amefariki katika ajali ya boda Bora,alikuwa abiria kwenye boda boda usiku wa kuamkia leo Jumamosi.
Ajali imetokea jana,amefariki leo.
Amefariki hospitali baada ya juhudi za kuokoa maisha yake kushindikana.
Ajali imetokea Shinyanga ambako Chief alikuwa anafanya kazi.
Hii ni fatal crash nyingine kabisa.
Ijumaa iliyopita tumemzika Daudi Nyerere,mtoto wa Makongoro Nyerere na sasa,siku saba baadaye,Ijumaa usiku,Chief amefariki katika ajali ya boda boda.
Magige Nyerere ni kaka yake Makongoro Nyerere.
Kwa hiyo sasa ni wajukuu wa Mwalimu Julius Nyerere wawili ambao wamefariki katika car crash.
Again,hii ni ajali tofauti. Siyo ile ya Daudi Makongoro Nyerere.
Makongoro Nyerere na Magige Nyerere wote ni watoto wa Mwalimu Nyerere.
Kwa hiyo,ilikuwa ni ajali ya piki piki,siyo ajali ya gari.
usiku na boda bodaa kweli mchumi rip kamanda
 
Nyerere analipwa .
Kusababisha Watanzania zaidi ya elfu 20 kufa kule Uganda pasi na sababu za msingi unadhani MUNGU atafurahia uzao wako?

Bila vita vya Kagera ungekuta Tanga ni bandari ya Uganda. Awali ya yote ulikuwa hujazaliwa unaandika vitu usivyojua tuachie sisi tuliokwenda mstari wa mbele.
 
Back
Top Bottom