Ninatambua vyema kuwa watu wameibua hoja ya Jesca (mtoto wa Mkuu wa Kaya) kwa sababu hasa ya kuchukizwa na kauli tata ya Mkuu wa Kaya ya kuwaita watoto wa wenzie "Vilaza", niseme tu hii imetukera wengi
Lakini yote kwa yote nadhani turudi katika kujadili na kutafuta majibu ya hoja nzito za kitaifa zitakazoleta manufaa ya moja kwa moja kwetu sote ikiwemo ya kushinikiza kurudishwa Chuoni kwa vijana hawa waliofukuzwa bila utaratibu.
Nashauri tusihame katika hoja nzito za "Lugumi", mijadala ya Bunge live, huduma za Afya, Sheria kandamizi za makosa ya mitandao, Sukari kuuzwa 4,000/= hadi 7,000/=, Mkwamo wa Uchumi wa Nchi, Biashara haziendi, hakuna Soko la Uhakika kwa Mkulima, Umeme Vijijini, Maji safi, Madawati Mashuleni na mengine mengi
Lakini pia tunapaswa kutambua hadi sasa hatuna "Dira" ya Nchi, tunaenda tu kama Ng'ombe, Taifa halina mwelekeo, hatuna Dira hata ya miaka 20 tu, wazo la Katiba mpya linaelekea kuzikwa kwa kisingizio cha "hakuna hela", ni kwa sababu "watawala" ni wanufaika wa "Mfumo" uliopo, kwa hiyo hawaoni haja ya kuliharakisha hili
Mwisho wa yote niseme, kuna watu wanafurahishwa na ukimya wetu juu ya haya ambayo badala yake tumechukua moja la "Jesca" tukifuata msukumo wa hasira, hasira za kudhalilishwa na Mkuu wa Kaya akiwaita wananchi wake "Vilaza". Tusipo-control hisia zetu tutazika mengi ya msingi kwa upepo usio na faida ya moja kwa moja
"Turudini kwenye hoja za msingi, Jesca isiwe Ajenda kuu ya kitaifa"
Naomba kuwasilisha. Ni ushauri tu