Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Wewe na aliyekutuma wote vilaza tu.
Wala sikatai kwani mimi ni mwanadamu kuna baadhi ya mambo mimi ni kilaza kama vile kwenye kumywa kangala,mapuya,dengerua, dadii, na kumpumu. Lakini waliokuleta duniani wao ni vipanga mpaka huitwa waonjaji.
Kiakili sina shaka leo karibu siku ya tatu unachota madini ya kutosha na ayakauki.
 
Nenda kanye west...naona umechafukwa tumbo
 
Ungemjibu hoja yake hivi mtoto anaweza kujaza fomu bila kuwashirikisha wazazi wake hivi unataka kusema yule binti babake hajui yupo wapi?
Wewe ukiwa Mtu mzima ni vingapi unavyo fanya tofauti namatarajio au ushauri wa wazazi wako au marafiki zako? Mzazi anaweza kuwa hapendi matokeo ya mtoto wake na anachofanya au alicho fanya ni juu ya mamlaka husika kuchukua hatua . Kuna maneno yanayo semwa mtaani kwamba Raisi wa awamu ya nne hakutaka kuchukua nyumba ya serikali Maana alijua itakuwa chanzo cha kuonekana ni Mtu wa kuchukua advantage ya position yake , kinyume chake ilikuwa ni reasons ya kumuona Kama si miongoni wao, hivyo kutaka ku mchuja katika kumpa madaraka. Victoria hivyo hii sera ya 2014 inaweza kuwa ukipita baraza la mawaziri bila wengine kuridhia, na kutumia kigezo hicho.
Na mwisho kwenye Hiyo form kuna sehemu ya ku refer kwa wazazi kujaza
 
Inasikitisha sana vijana kutumika kuzima mijadala ya msingi kwa taifa hili, hizi agenda setting zinaletwa ili kuzima mambo ya msingi kwa nchi hii. Leo hii Division 4 ya Jesca imewafanya wengi wasahau swala la Lugumu. Jesca pia amekua maarufu hadi kuzima issue ya uhaba wa sukari. Vijana tutatumika hadi lini? Hongera Magu kwa kuzima issue ya Lugumi na Kitwanger wake.
 
Usisahau kuwa hili taifa linaishi kwa matukio

Baada ya jesca litakuja tukio jingine tenaa

Mungu bariki Tanzania
 
Wakati mbuge fulani aliposema Bangi ihalalishwe bungeni maana kuna watumiaji wapo kati yao, kuna uwezekano mkubwa baba jesca alikua mmoja wapo

Wewee sheria ya mtandao asijekuitumia baba Jesca! Ila umenimalizaa hadi mbavu sina.
 
Akina jesca wapo wengi, ili unufaike tunaangalia we no jesca nano? Mfumo wa elimu unaweza kukubeba kwa manufaa yako. Matabaka yapo na yataendelea kuwepo.
 
Wewe August, face the situation in perspective and accept the truth: WE GOT A WRONG CAPTAIN PILOTING OUR PLANE!
 
Unataka kuniambia mh. Sana hajui mtoto amepitia njia gani kufika pale.
 
Nilimsikia siku ile Magufuli kuhusu vilaza,kinachotokea leo hii naona kama sinema ya Kihindi, siamini amini yan!
 
Ninatambua vyema kuwa watu wameibua hoja ya Jesca (mtoto wa Mkuu wa Kaya) kwa sababu hasa ya kuchukizwa na kauli tata ya Mkuu wa Kaya ya kuwaita watoto wa wenzie "Vilaza", niseme tu hii imetukera wengi

Lakini yote kwa yote nadhani turudi katika kujadili na kutafuta majibu ya hoja nzito za kitaifa zitakazoleta manufaa ya moja kwa moja kwetu sote ikiwemo ya kushinikiza kurudishwa Chuoni kwa vijana hawa waliofukuzwa bila utaratibu.

Nashauri tusihame katika hoja nzito za "Lugumi", mijadala ya Bunge live, huduma za Afya, Sheria kandamizi za makosa ya mitandao, Sukari kuuzwa 4,000/= hadi 7,000/=, Mkwamo wa Uchumi wa Nchi, Biashara haziendi, hakuna Soko la Uhakika kwa Mkulima, Umeme Vijijini, Maji safi, Madawati Mashuleni na mengine mengi

Lakini pia tunapaswa kutambua hadi sasa hatuna "Dira" ya Nchi, tunaenda tu kama Ng'ombe, Taifa halina mwelekeo, hatuna Dira hata ya miaka 20 tu, wazo la Katiba mpya linaelekea kuzikwa kwa kisingizio cha "hakuna hela", ni kwa sababu "watawala" ni wanufaika wa "Mfumo" uliopo, kwa hiyo hawaoni haja ya kuliharakisha hili

Mwisho wa yote niseme, kuna watu wanafurahishwa na ukimya wetu juu ya haya ambayo badala yake tumechukua moja la "Jesca" tukifuata msukumo wa hasira, hasira za kudhalilishwa na Mkuu wa Kaya akiwaita wananchi wake "Vilaza". Tusipo-control hisia zetu tutazika mengi ya msingi kwa upepo usio na faida ya moja kwa moja

"Turudini kwenye hoja za msingi, Jesca isiwe Ajenda kuu ya kitaifa"

Naomba kuwasilisha. Ni ushauri tu
 
Usisahau kuwa hili taifa linaishi kwa matukio

Baada ya jesca litakuja tukio jingine tenaa

Mungu bariki Tanzania
Naona mzee wa matukio kaibukia kanisani kwa mzee wa upako huku vijana wake wakiibua threads za benki kuu kuwapoteza watu....nchi imekaa kitapelitapeli tu
 
Nilimsikia siku ile Magufuli kuhusu vilaza,kinachotokea leo hii naona kama sinema ya Kihindi, siamini amini yan!
Hii nchi ya ajabu sana....mpaka sasa bajeti ya nchi imewasilishwa karibia nusu....tunachojivunia ni bomba la mafuta toka Uganda ambalo hatuambiwi tutafaidi nini! Hakuna mpango wowote wa kimaendeleo hotuba za bajeti ni kukopi na kupesti
 
Unataka kuniambia mh. Sana hajui mtoto amepitia njia gani kufika pale.
Unajua kuna mtoto anaweza kuwa an out cast , baba au wazazi wasi take kujua mambo ya mtoto kutokana na tabia yake na pia kuna wazazi ambao Wanapenda kutokujua mambo ya watoto ili asijiumize kichwa na kumpa changamoto ya mtoto kuwa self reliant na kujua kwamba akifanya vitu vinavyo kwenda kinyume , basi kuna matatizo utapata. Na infact ikishakuwa over 18 mfano police hawaruhusiwe kutoa taarifa zako kwa wazazi wako mpaka wewe mwenyewe uridhie. Au mpaka hapo mashtaka yakoyanapokuwa ni ya wazi .
 
Iparamasa na Wambandwa.
Kuna vitu viwili ambavyo ningependa kuviongelea kimoja Kama Jesca haja fikia vigezo Kama wale 7000, basi mamlaka husika wamtoe hapo chuoni na pili tukumbushane kurudi kwenye mstari na ni kufuata vigezo yaani standards , tunapofanya mambo yetu , hivi vitu Ndio vitatu Toa ktk hii thread isiyoisha na inayotutoa kwenye mada muhimu zaidi mfano Lugumi na EPA, escrow , mere meta , tax evasion, money laundering , productivity ,uchafu katika makazi yetu , barabara za makazi yetu na kuendelea.
Mambo mengine katika thread hii ni vikorombwezo au tunaita side show.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…