Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Jesika atolewe na wale wa UDOM ambao wako kihalali ila wakafanyiwa figisu za kisiasa warudi
 
Nimesoma comments kadhaa nikaona nirudi kujibu hoja hizi...
Mosi: Jessica sio miongoni mwa wale wa program maalumu ya Ualimu bali ni mwanafunzi anayesomea degree hivyo kwa muda wa miaka miwili ameweza vipi kujisafisha na kudahiliwa???
Pili: wale wanafunzi wa program maalumu sio kweli kwamba hawakuwa na vigezo hapo ndio wengi mnachanganya, wale wanafunzi walikuwa wanasoma diploma kwa miaka mitatu na sio degree kama wengi mnavyopotosha. Ni halali kabisa ukiwa na ufaulu mzuri basi unasoma certificate 1year kisha diploma 2years hivyo jumla 3years jambo ambalo ni sahihi kabisa hata vyuo vya afya wanatumia mfumo wa miaka mitatu...wanafunzi waliochaguliwa program ile walikuwa na ufaulu mkubwa wa A na B katika masomo ya science na walikuwa wenye division 1 hadi 3, je hao ni vilaza??? Hapana...
Ifike mahali muweze kutofautisha issue ya Jessica kudahiliwa degree na wanafunzi wa program maalumu UDOM
mkiweza kuja kwenye mstari basi issue ya wanafunzi wa program maalumu utaiacha pembeni na kujadili mada husika Jessica amefika vipi chuo kikuu ndani ya miaka miwili??? Sote tunatambua mfumo na mtaala wa elimu ya nchi yetu, hivyo tujadili kwa hoja madhubuti
 
 
Tuanapoteza muda kujadili vitu visivyokuwa na maana. Ukweli ni kwamba nchi ilikuwa imeingiliwa na Mdudu Dili.Nampogeza Rais na waziri wake kutuondoa huko kwenye uchafu. Watu fake walikuwa wanazalishwa kila siku. Reference ya mtu haisaidii. All we want is to uproot this cancer. Haiwezekani tukawa na wahitimu wa makaratasi, ambao hawana sifa kwa jamii. Useless people.
Picha tunaiona kwenye matusi. Ukiona mtu anatukana kama makuli wa zamani kule Bandalini ujue huyo mtu hawezi kuhimili hoja za tafakuli.
 
Jesika awe uprooted sasa...sio unajaza ugoro wako humu w
 
Well said Mr, kuondoa elimu ya makaratasi ...kauli nzuri sana hiyo na turudi kwenye mstari je sio halali kwa mwanafunzi aliyemaliza form four na ufaulu wake akaenda kusoma certificate mwaka mmoja kisha diploma miaka miwili jumla ikawa miaka mitatu??? Ni mfumo ulio wazi kabisa na vyuo vingi sana wanatumia mfumo huo kama DIT, MIST n.k ambapo wanafunzi wanaojaza form wanaruhusiwa kuchagua vyuo vya ufundi, na kipindi nasoma nilipoingia A'level kulikuwa na baadhi ya rafiki zangu waliochaguliwa college diploma for three years even health institutes wanachukua three years means 1 year + 2 years total 3 years, Sasa hapo utasema vipi wale wanafunzi waliokuwa UDOM wakisoma diploma hawakuwa na vigezo?! Hujioni mpaka kuwaza hivyo utakuwa na itilafu kidogo ya ubongo?? Okay kama unavyojinasibu mkulu anafanya kazi nzuri kusafisha nchi (i don't believe) kwanini asianze kusafisha kwa mwanae ambae amehujumu system ya elimu ya juu kuingia degree???
 
afrika hamna over 18.
 
Hivyo vingine vilishagonga mwamba na kwa vile hili limeibuka ghafla, watu walikuwa hawajajipanga. Hiki kitu usikiunderestimate, kinatupa picha halisi jinsi elimu ilivyo duni. Amini usiamini kila atakapogusa atakuta anaowaita 'vilaza' wamejazana. Mtanzania hajafeli, ni system ndiyo iliyofeli.
 
Wanafunzi zaidi ya 400 wamefukuzwa chuo kwa kashfa kubwa kwa wanafunzi hao, wazazi wao na chuo chao. Hapa hawakutajwa majina lakini bila shaka kwenye communities zao wanadharaulika wao na hata wazazi wao waliokuwa wanatambia 'usomi' wa watoto wao. Kweli hiki kitu ni maumivu.

Wengine 7800 wamefukuzwa chuo. Hawa walikuwa wanasoma kwa kutumia facilities za Udom na walikuwa wanapata mikopo kwa asilimia 100 na waliahidiwa ajira. Hawa kusema kweli wengi tuliwalilia. Waswahili wanasema 'mtoto kwa mama hakui'! Na hawa waliofukuzwa inawezekana wengi walikuwa na umri wa miaka 20. Sidhani kama kuna mzazi ambaye aliweza kulala usiku huo ilhali hajui mtoto wake kalala wapi. Walioonyesha sympathy wameitwa vilaza. Ingawaje sababu za kufukuzwa hawa hazijawekwa bayana.

Kinachozungumziwa hapa ni justice bila upendeleo. Bila shaka huu uzi unaumiza roho za watu, cha ajabu hapo ni nini? Si kuna machozi ya zaidi ya watu 8200 yaliyomwagwa wiki iliyopita?

Kutukana au kutokutukana ni ustaarabu wa mtu na siyo kipimo cha elimu yake. Kama wakuu wetu wa nchi wanaweza kututukana hadharani, wananchi wa kawaida unategemea watasemaje? Tangu nakua mpaka hivi leo kuna maneno ambayo sintoweza kumwita mtu: lofa, kilaza, mshenzi, bwege. Kwa wengine haya ni maneno ya kawaida na utaambiwa msamiati unakuwa.

Nakubaliana na wewe kwamba elimu ni cancer au janga la kitaifa. Watanzania tumenyimwa elimu bora na badala ya kuonekana sisi ni victims wa mfumo mbaya sasa tunakuwa victimized. Lazima kuwe na mikakati thabiti ya kuwanyanyua watanzania kielimu. Na sio tu darasa la kwanza bali hawa waliozaliwa miaka ya 80 mpaka ya 2000.

Karibu JF kama kweli ni mara ya kwanza. (Kuna kubadilisha ID).
 
Lu-mimba wako kimya kama watoto wanaoshwa kwenye beseni
Lumumba wajibu nini walikuja spidi kujaribu kuzima hili kumbe ndio wakawa wanachochea zaidi wakawa wanaondoka mmoja mpaka sasa wamepoteana na nasikia Dau lilipanda kuzima moto huu lakini wameshindwa.
 
Hii nchi ya ajabu sana....mpaka sasa bajeti ya nchi imewasilishwa karibia nusu....tunachojivunia ni bomba la mafuta toka Uganda ambalo hatuambiwi tutafaidi nini! Hakuna mpango wowote wa kimaendeleo hotuba za bajeti ni kukopi na kupesti
 
Baada ya kumpa kisa hiki mzee wangu ambaye ni mwalimu mstaafu,aliniuliza hivi hao watoto kama hawana sifa za kufundisha sekondari,je wangemalizia huo mwaka wa tatu wangekosa sifa za kufundisha primary?nikamjibu waalim wa sayansi primary wametosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…