Ni nini tafsiri rahisi kama una qualifications had PhD, Mke pia ni mwalimu mbobezi wa kufindisha watoto elimu ya msingi, mnajaliwa watoto saba, na kati ya hao, mmojawapo anatoka na div 4 point 30.. Je ni child neglect? Au ni yale yake aliyosema Bashe ya kwamba taaluma ya waalimu ni chaka la waliofeli?
Inawezekanaje kama baba pia mama wote ni wanataaluma na wanashindwa kuwaelewesha au kuwafundisha watoto wao masomo ya awali hadi wafaulu na kuepukana na hizo div4 pts 30? Je jukumu la baba au mama la kusaidiana na waalimu wa awali linaishia wapi na lini? kama mtot ana utindio wa ubongo au ni mgumu wa kuelewa, au ni mzito kichwani, vipi shule maalum, alipelekwa?Kuwaita wengine vilala ni dalili za frustrations au msongo wa mawazo na kutokuelewa katika familia hadi motto kufikia div 4 points 30.
Jamii itawaelewaje, achilia mbali kama ni first family au la? Kama sio child neglect ni nini? halafu watoto saba...du...mzee alikuwa hachezi mbali na kinyama ugomvi, lakini kuwafundisha ilikuwa mtihani mwingine kwake (Ni kazi ngumu sana ile), yeye ni kufyatua tu watoto na kusonga mbele (elimu ya uzazi wa mpango pia haikueleweka) ama kweli walio mpa jina la Bulldozer hawakukosea... samahanini kama kuna walio udhika na uzi huu...