Mtoto wa miaka sita anagoma kwenda shule. Nini kifanyike?

Tumieni njia ya kumbembeleza sasa na vizawadi kidogo ataenda tu
 
Maswali ya kujiuliza:
-Hiyo mimba iliingia kawaida au ilitafutwa kupitia mitume na manabii/kwa waganga?
-Kati yenu nyie wote mlisoma vizuri tu na kumaliza elimu zenu bila shida?isijekuwa anapitia njia ya mzazi mmojawapo au kwenye familia zenu mlizotoka kuna mtu wa hivyo aliwahi tokea.

mkipata majibu tafuteni njia ya kumsaidia hata kama Ana uelewa wa vitu vingi basi anahitaji hata elimu ya msingi tu kujua kusoma,kuandika na kuhesabu.
 
Mtoto mdogo anakushindaje ?....mkunje wakati bado mbichi.....huyo aende shule apende asipende.
 
ngoja nitete na ubalozi wa marekani

Dogo achukuliwe apelekwe WTC(war training centre) kituo hicho Cha mafunzo kitamfaa

mjukuu wa mkwawa
nae ilikuwa hivyohivyo alipelekwa na ni noma ndani yajeshi la marekani
 
Dikteta wa baadae huyo. Mungu apishilie mbali akatawale somalia
 
Itakuwa amerithi tabia zako mbaya.kwa kuwa hataki shule inabidi umpeleke Kwa wa hadzabe akaanze kuishi maisha ya kuwinda wanyama na kula wabichi maisha yote.huko hakuna Cha shule Wala kuwaza maendeleo
 
Mpambanieni mtoto apate elimu japo ya msingi, asiposoma kabisa atakuja kuwalaumu wazazi ukubwani kwamba hawakumsomesha na huenda akaja kuwasumbua baadae, msikate tamaa tumieni Kila mbinu angalau ajue kusoma na kuandika bila hivyo ataishi maisha ya ajabu sana
 
Huyu mtoto anatumika chukua hatua za kiroho
 
Toto mmelidekeza halafu mnakuja kutusumbua humu JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…