Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

Heko dah
 
Katoto hako ni ka ajabu sana miaka 4 kana tabia za uke wenza? Mtoto gani hapendi zawadi? Kama baba yake yupo mwambie huyo mwanamke amrudishe kwa baba yake. Mtoto umekua nae tangu mwaka sasa hiv miaka 4 kakomaa na tabia za kuzila zila? Karudishe kwa baba yake.

Nb.hicho ndo kiwanja chenye mgogoro sasa.😂
 
Kusema ukweli kuoa ma single mother kuna changamoto yeye anataka umpende mwanaye mwanaye hakupendi mama anajaribu kulazimisha ili asimtie aibu maana alimtetea kuja kukaa na ww lakini mtoto hana mood kabisa. ngumu sana
Pole kaka ila usilazimishe kitu. Watoto wana akili kuliko tunavyofikiri. Endelea kuwa baba kwa mtoto huyo, hata kama haonyeshi response nzuri kwako ila nakuhakikishia ipo siku atakutambua. Endelea kuwa baba kwake kuna kitu unajenga ndani yake na majibu utayaona. Usichukulie kuwa ulezi huo ni lazima upate malipo.
Ila pia ongea na mama mtu. Why hataki mtoto wake aonane na baba mzazi? Hayo ni makosa hasa kwa sababu baba mtu yupo na zaidi mtoto anamtambua baba yake. Actually nahisi huyo mtoto anaumia kuliko anavyoonyesha na nyie mnafikiri anaku reject.
Take heart, yupo Mungu atakulipa kwa kikubwa hiki inachofanya
 
Hii ndio point.
Mtoto anamjua baba yake.
Full stop.
Mwingine unaonekana stranger tu.
 
Aisee mna kazi, yote hayo ili tu kumrubuni mtoto wa watu!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna ulazima wa kumwambia mtoto huyu ndiye babako kwani hata watoto wako mwenyewe huwa hawaambiwi kuwa wewe ndiye baba yao bali mtoto ujua automaticaly, mfno, mpokee baba, msalimie baba, baba yuko wapi? hii nguo umenunuliwa na baba, mwishowe mtoto ujua kuwa huyu ndiye baba.
 
Katika saikoloji huwa tunasema kila jambo huwa lina sababu yake

Ukiona mtoto wa singo maza hakupendi ujue kuna sababu nyuma ya paziaa na chanzo cha haya yote Ni MKEO na NDUGU JAMAA wa biological father kuna maneno dogo wameshamjaza na kama unavyojua koo zetu za kiafrica zinavyomuelezea baba wa kambo
 
Maisha yatakuwa magumu kama huyo mtoto wa kambo hakutaki, na pia huwezi lazimisha akutake.
Unajua ni makwazo kuishi na mtoto usiyeelewana naye, maana kumsomesha ni lazima mama yake atamtetea je maisha yatakuwaje na huyo mama kama mtoto hakutaki.
 
Unabishana na mtoa ushauri tena?
 
Michepuko inaaribu familia..michepuko inasababisha Wanaume wanafungwa JELA...
Michepuko Inafanya Wanaume wasijali familia zao inavyotakiwa..

Lakini wengi humu mnaaamini mnauwezo wa kuhandle michepuko yenu..
.Mungu awasaidie
 
Baba mtoto yuko hai mama mtoto hataki kumpa mwanae amkuze na hataki kabisa kuwa na mazoea naye sasa hapa mm nafanyaje nimependa mke, mke hana kazi nimeoa
hahahaha umenichekesha sana.... huyo mtoto anza kumcontrol wewe awe na adabu na akuheshimu...mwambie mama yake kama haiwezekani ampeleke kwa baba yake..... naziona dalili za wewe kushindwana na huyo mkeo kisa mtoto. shika kiboko huyo mtoto ni mdogo lakini ana uwezo wa kufundishika....

kila siku mnapewa humu ushauri kuhusu kuoa watu wa aina hiyo lakini hmsikii kabisa....
Hapo jipange aiseeee...

c Jokajeusi
 
hahahah jf hatari sana .. unajua watu kila leo wanashauriwa kuhusu hili jambo la viwanja vyenye mgogoro lakini ndi kwanza wana nunua...

halafu nkulazimisha mtoto ampende kwa kumnunulia vizawadi mimi bnakataa huyu mtoto si wa kubembeleza ni kuachana nae tuu asimbembeleze kama kumpenda achague yeye na asimlazimishe amuite baba..... shida ya ndugu yetu ana lazimisha mtoto asiye wake ampende
 
Hakika umenena dea, [emoji120][emoji120][emoji120]
Hapo kwenye swali, ndo na mie niliwaza hivyo.
 
Huyo ni mtoto mdogo kujua wewe sio baba yake sio rahisi labda huwa unamtazama tofauti. Unakuta watoto wengine kila mtu anamwita baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…