Mtoto wa Mzee Malecela amtukana Tundu Lissu na kutoa kauli za vitisho na shari dhidi ya mikutano ya CHADEMA

Mtoto wa Mzee Malecela amtukana Tundu Lissu na kutoa kauli za vitisho na shari dhidi ya mikutano ya CHADEMA

Nisiongeze chochote.

Fuatilia ktk video.

Bahati nzuri Tanzania ni Nchi kubwa, sio kama Burundi, au Afrika ya Kati, au South Sudan. Huko kwenye vi Nchi vya hovyo hovyo unaweza kuongea hivyo, lakini Tanzania ni smart zaidi, ni kubwa zaidi na Ina watu mart. Huwezi kufanya fujo.
 
Ukiondoa mahaba yako mleta mada.........jamaa hakuongea Baya ......Ila wewe Una mahaba na mrengwa au mtajwa .........
 
shida iko wapi hapo kwenye maongezi ya jamaa, tuache kudekadeka, maneno hayo hayo kila siku huyo huyo TL na wenzie waliyatumia kwa marehemu JPM.
 
Mzee wao aliharibu alipobadilisha jina na kusilimu uzeeni - Mwalimu akammaliza hapo hapo teh teh teh

..habari kwamba Mzee Malecela alibadili dini sio za kweli.

..pamoja na hayo hakuna ubaya wowote ule kubadili dini.
 
Tatizo halikuwa kubadili jina bali motives behind ya kufanya hivyo.
Mzee aliuza utu wake

..zile zilikuwa propaganda tu.

..Mzee Malecela ana uwezo mkubwa ukilinganisha na wanasiasa uchwara tulionao sasa hivi.
 
inategemea unabadilisha dini katika mazingira yepi? ya huyu mzee yalimtatiza hadi Mwalimu.

..hakubalisha dini Mzee wa watu.

..Mwalimu alimtoa kafara Malecela kutokana na hoja ya Tanganyika.

..Kwa taarifa yenu Mzee Malecela alituletea serikali ya Tanganyika Mwalimu akaipora.

..Wakati Malecela akiwa Waziri Mkuu Bunge lilipitisha azimio la kuunda serikali ya Tanganyika.

..Pia kipindi cha Uwaziri Mkuu wa Malecela Bunge lilitunga sheria ya kurudisha mfumo wa vyama vingi.

..Mwalimu alikuwa anacheza rafu ili apitishe mtu wake kugombea Uraisi.
 
..hakubalisha dini Mzee wa watu.

..Mwalimu alimtoa kafara Malecela kutokana na hoja ya Tanganyika.

..Kwa taarifa yenu Mzee Malecela alituletea serikali ya Tanganyika Mwalimu akaipora.

..Mwalimu alikuwa anacheza rafu ili apitishe mtu wake kugombea Uraisi.
Kwa hiyo yule Mzee Jumanne alikukwa nani mkuu? ni hivi Mwalimu hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujihusisha na Zanzibar kujiunga na OIC. Kwa hiyo kitendo hicho kilimkera sana Mwalimu hadi akafikia kumtaja Malecela kuwa ni muhuni na mroho wa madaraka.
 
..suala la " jumanne " lilikuwa siasa za kuchafuana tu.

..Mwalimu hakufurahishwa na hoja ya Tanganyika, na alitunga mpaka na utenzi na kitabu.

..kuita wenzake wahuni ilikuwa na mapungufu ya Mwalimu Nyerere ktk kutumia lugha za staha ktk kujenga hoja.
 
Back
Top Bottom