Mtoto wa Rais Samia (Wanu): Sitamani Kuonekana Mtoto wa Rais Nikiingia Mahali/Naumia Mzazi Akitukanwa

Mtoto wa Rais Samia (Wanu): Sitamani Kuonekana Mtoto wa Rais Nikiingia Mahali/Naumia Mzazi Akitukanwa

"Kuna mahali naingia nafanya kazi zangu naondoka bila Watu kujua kama nilikuwa pale, lakini unapokwenda kwenye shughuli za kijamii hasa harusi kuna Watu lazima wanitambulishe kama mtoto wa Rais, ile huwa inanifanya nisiwe huru katika mazingira yale" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

“Inaumiza kama mtoto kuona mzazi anarushiwa maneno mitandaoni na katika kipindi ambacho muda wake wote amewekeza kwa Taifa, muda mwingi anakuwa mbali na familia, lakini ni Mtu imara sana namfahamu hajawahi kutetereka kwenye hilo” - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

"Moja kati ya changamoto kubwa ninayokutana nayo katika uongozi wangu ni wananchi wangu pamoja na Watu wengine kuhisi naweza kufanya kila kitu kwa kigezo kwamba ni mtoto wa Rais, sio kweli kwamba naweza kufanya kila kitu na kuna wakati nazidiwa" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

View attachment 3075878
So stupid, mtoto wa, rais unaongea pumba, hapo ukute na yeye anavizia ajira, au kapachikwa sehemu,
Aache ujinga Rais kutukanwa ni kitu cha kawaida, atumie nafasi yake kusaidia wenye uhotsji, kama Hana wazo aige anavyofsnya Charlene Ruto, mtoto wa rais wa Kenya,
Huyu wa kwetu unaweza kukuta Hana hata degree moja, kikubwa anachokifsnya ni swala tano na kutunza mume tu, so pathetic
 
Kukosolewa kwa staha ni kukosoa kwa kutumia lugha ya staha na sio lugha ya kuudhi au kutukana. Somo hili la ukosoaji wa staha nililianza toka enzi za JK Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim! alipokuja JPM, pia tulipiga somo hili Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli na sasa Samia Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda kote huko kunatumika lugha za staha.
P
Rais ni taasisi hivyo urais ukiwa ni taasisi natumai muhusika kwa hivi sasa ni Dr. Samia anao wasaidizi wake wanaoandaa hotuba zake na nini cha kutekeleza na cha kutotekeleza hivyo anatakiwa kuwa makini na kikosi chake kuhakikisha kinampa taarifa sahihi na si bora liende, swala la tumpe muda miaka yote mitano halikubaliki, vinginevyo na sisi tukifeli mitihani tulewe muda! Rish aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza alipovurunda hakupewa muda na hakubisha, alipisha njia. Nirudi kwenye matusi! Haya matusi yanatumika kama fimbo ya watawala dhidi ya watawaliwa kwani huwa hatupewi huo ushahidi wa hayo matusi zaidi ya kuambiwa wanatukana huku tukishuhudia bakora za umeme zilizotumika Afrika Kusini wakati wa makaburu zikianza kutumika!
 
Mmwambie Mam,Mwajuma anaiba fedha za miradi ya maendeleo kule Moshi manispaa!
 
Kukosolewa kwa staha ni kukosoa kwa kutumia lugha ya staha na sio lugha ya kuudhi au kutukana. Somo hili la ukosoaji wa staha nililianza toka enzi za JK
P
Ifunguliwe mahakama ya maadili kushughulika mashauri ya kesi za lugha za staha na kuudhi.
 
Muuliza mother, lini atafika Lupa Tingatinga? Wananchi wanahitaji wamuone ili wampe kura
 
Back
Top Bottom