Mtoto wangu yupo kidato Cha 3 lakini hata dirishani hafiki; atarefuka kweli au ndo basi?

Dirisha linaanza kozi ya nne tu.....na kozi nne maana yake ni tofali nne. Pamoja na hayo lakini mwanangu huyu aliye kidato Cha tatu hawezi kufika. Ni mfupi kweli. Vipi jamani, atarefuka baadae?!!! Ana miaka 17.
Atarefuka huyo mkuu.. miaka 17 nilikuwa kidato cha tatu kama mwanao na nilikuwa mdogo haswa kwa miaka ile nilionekana kama sinto kuwa mrefu ila asaiv ni miaka 17 imepita urefu wangu ni 5.7 inch.

Usimkatie tamaa hata kidogo. Muhimu endelea kumpa matumaini na hakikisha athiriwi kisaikolojia hata kidogo.

Nakumbuka sisi tulikuwa tunabaguliwa mno na wanafunzi wenzetu ambao asaivi wengi wao kwangu ni wafupi sana.
 
Balaa yanii... 😀 😀 😀 halafu wana short temper kama miili yao
Kuna kijamaa hapa kitaa kina 4.7 feet kimekomaa halafu kibishi ile mbaya na kina mihasira kidogo tu eti kitanichapa makofi mtu mwenye 5.9 feet.

Kimakonde halafu ni kishabiki cha Uto, kina mikawara wakati nikiamua kukichezesha mtama mmoja na kukizimisha kabisa inawezekana ndani ya 30 secs tu
 
Dirisha linaanza kozi ya nne tu.....na kozi nne maana yake ni tofali nne. Pamoja na hayo lakini mwanangu huyu aliye kidato Cha tatu hawezi kufika. Ni mfupi kweli. Vipi jamani, atarefuka baadae?!!! Ana miaka 17.
Sasa kama we mwenyewe Andunje, inawezekanaje upate mtoto ngongoti mkuu?
 
Kuna kijamaa hapa kitaa kina 4.7 feet kimekomaa halafu kibishi ile mbaya na kina mihasira kidogo tu eti kitanichapa makofi mtu mwenye 5.9 feet.

Kimakonde halafu ni kishabiki cha Uto, kina mikawara wakati nikiamua kukichezesha mtama mmoja na kukizimisha kabisa inawezekana ndani ya 30 secs tu
Kama nakiona...hahahah huku anatafuna meno...ahahah
 
Back
Top Bottom