Mtu akikuomba ushauri kwa jambo kama hili utamjibu nini?

Mtu akikuomba ushauri kwa jambo kama hili utamjibu nini?

KILA NIKIMUONA MTOTO WA MUME WANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA!

Kaka naomba tu unisaidie maana najikuta nashindwa haya maisha. Mimi nimeolewa ndoa yangu ina miezi minne sasa. Wakati nakutana na huyu mchumba wangu aliniambia kabisa kuwa ana mtoto ambaye amezaa na mwanamke mwingine, alishaachana na mwanamke na kaolewa hivyo yeye anaishi na mtoto wake kwani hataki mtoto wake kulelewa na Baba wa kambo.

Basi mimi sikua na shida, nilikua naenda kwake, namuona mtoto lakini wakati huo hata sikuona kuwa ni tatizo kwakua nilikua bado sijaolewa. Lakini Kaka baada ya kuingia kwenye ndoa, kuanza sasa kuishi na yule mtoto ndiyo sijui naonaje, mpaka nahisi kuchanganyikiwa. Katoto ni kakike, lakini ana sura ya Baba yake, yaani sijui nikuambieje Kaka, sio kwaba ni mtoto mabya, siwezi kusema hivyo lakini hatuendani naye kabisa.

Rafiki zangu wakija kunisalimia inabidi niseme tu ni mtoto wa ndugu yake na mume wangu lakini si mtoto wa mume wangu. Mtoto ana miaka mitano, ana akili, kachangamfu anajua kila kazi na ananiheshimu. Yaani kangekua katoto kazuri ningekapenda balaa kwani kana heshima sijui nikuambieje Kaka, lakini shida nashindwa, nikimuangalia wakati mwingine najiikuta na hasira tu nampiga hata bila sababu.

Hali hiyo inaniumiza kwani mwisho kanakuja kuniomba msamaha wakati hata hana kosa. Yaani kuna vitu vingine najikuta nagomba mpaka basi, nakua tu na chuki na mtoto. Wakati mwingine namfanyia visa tu ili kumpiga, mfano juzi nilimuwekea chakula kingi makusudi ili aache kula, basia liacha nikajikuta nampiga kuwa anachezea chakula basi nikamlazimisha kula na kweli alikula lakini alishindwa hata kunyanyuka yaani anapepesukapepesuka ila alimaliza na kuosha vyomboa akaosha.

Nilijisikia vibaya kwani sikupata faida yoyote, hali hii inanifanya nakua na kisirani, nakua mtu wa hasira hata kwa mume wangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, nataka kuongea na mume wangu amuondoe huyu mtoto ampeleke kwa Bibi yake. Mume wangu wazazi wake wamefariki lakini ana ndugu wengine, kuna Baba mdogo wake na wengine tu ambao wana uwezo.

Sio kama si mtaki moja kwa moja lakini aondoke tu ili niwe sawa maana nahisi naweza kumuua huyu mtoto. Shida ni kwamba mume wangu anampenda sana mtoto na kwakua yeye alilelewa na ndugu baada ya wazazi wake kufariki basi anasema kuwa mwanae hawezi kulelea na mtu mwingine yoyote na aliniambia kabla hata hatujaanza mahusiano, nisaidie kaka nifanye nini maana nahisi kuchanganyikiwa.

Je kama ni wewe ndio unaombwa ushauri kama huu, utamjibu nini, utamuacha salama kweli?
YANI NYIE WATOTO MLIOPATIKANA BAAA MNA ROHO MBAYA SAM
 
Kuna technical error huwa zinatokea hadi wazazi wanashindwa kuishi pamoja na kumlea mtoto. Kikubwa ni kuwa mkweli ndani ya nafsi kama umemkubali mwanamme na unajua ana mtoto kwanini baadae umgeukie mbogo mtoto! Si ulikuwa na option ya kukataa kuolewa na uendelee kumsubiri huyo asie na mtoto? Roho mbaya haijengi, ukimchukia mtoto wa mmeo asie na tatizo kitabia am sure hata ndugu zake pia utawachukia sasa utaishije kwenye hiyo ndoa ambayo unataka uwe wewe na mmeo tu?

By the way hivi we dada mbona unaonekana mgomvi sana, mahusiano yako hua unayaendeshaje, maana nikiangalia vichwa vya wanaume tulivo less sioni mtu wa kukaa na wewe kwenye mahusiano hata masaa 48
Hakika
Kama alikuwa hataki mwenye mtoto kwanini akubali kuolewa ??
Yaani kumtesa mtoto namna hiyo ni ushetani,tena huyo mtoto amezaliwa kabla ya ndoa,heri angezaliwa baada ya ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mwanamke ni mtu mwenye dharau, majivuno sana, kifupi ni ana roho mbaya sana!!!
 
Kusoma tu nimepandwa na hasira imagine ndio ananiomba ushauri ana kwa ana nahisi kuna kitu nitakifanya
 
Yaani mtoto anafanana na baba yake halafu unamuchukua?

Mtoto kachukua sura ya baba yake na baba yake ni mbaya wa sura(nilivyoelewa mimi)

Dah!!nimejikutana napatwa na hasira niliposoma hapo kwenye kumupa chakula kingi ili ashindwe kukimaliza umupige...
kwanini sasa kaolewa na huyo Kaka Kama haipendi sura yake au ndo ameolewa sababu ya jioni ilifika jamn huyu dada mchawi siyo bure
 
Kwani sura ikiwa kwa baba kuna tatizo gani?
Wanawake wengine wamejaa gubu tu, akizaa wake mwenye sura hiyo atampeleka kwa ndugu?
Hii ndio inamfanya amchukie? Kwani mtu anajiumba.
Ni roho yake mbaya tu ndio inamsumbua. Aombe taraka aache mwenye mtoto amlee mwanae.
 
Kwani sura ya baba ina kasoro gani?
Kwa maana hiyo ht mme hampendi. Nina watoto wenye sura ya baba ila sijawahi kuwaza km hii ni tatizo kbs, nachukulia poa tu hlf ni wa kike. Na wa kiume kachukua sura yangu.

We dada hiyo ni roho mbaya tu inakusumbua.
 
Mimi ningemshauri ampende huyo binti la kama akishindwa basi yeye ndio aondoke kwa vile wahenga walisema "Ukipenda boga penda na ua lake" Huyo mume alomfata hapo ndio boga na huyo mtoto ndio ua lake.

Cc: Nahrene
 
Duuh! .hatari sana. Maskini hako katoto . Pamoja na kujipendekeza na kutamani ku-win moyo wa mama wa kambo bado haitoshi.
Ilibidi ukutane na toto likorofi kweli kweli yani ili akufunze adabu.
Poor girl, Mungu amfunulie mumeo aone your wicked heart.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atafte namna Mambo ya kuchoshana siwezi wangu tu hapo ukute ananisumbua sembuse wa mwingine, nimeshuhudia kwa ndugu walivoteseka na watoto wa kambo walivokuwa wakubwa wakawageuka kwa kweli niliapa silei mtoto wa mtu Bora Nika adopt yatima huko asiye na ndugu
Na wewe pia una roho mbaya tu kwa haya majibu yako.
 
KILA NIKIMUONA MTOTO WA MUME WANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA!

Kaka naomba tu unisaidie maana najikuta nashindwa haya maisha. Mimi nimeolewa ndoa yangu ina miezi minne sasa. Wakati nakutana na huyu mchumba wangu aliniambia kabisa kuwa ana mtoto ambaye amezaa na mwanamke mwingine, alishaachana na mwanamke na kaolewa hivyo yeye anaishi na mtoto wake kwani hataki mtoto wake kulelewa na Baba wa kambo.

Basi mimi sikua na shida, nilikua naenda kwake, namuona mtoto lakini wakati huo hata sikuona kuwa ni tatizo kwakua nilikua bado sijaolewa. Lakini Kaka baada ya kuingia kwenye ndoa, kuanza sasa kuishi na yule mtoto ndiyo sijui naonaje, mpaka nahisi kuchanganyikiwa. Katoto ni kakike, lakini ana sura ya Baba yake, yaani sijui nikuambieje Kaka, sio kwaba ni mtoto mabya, siwezi kusema hivyo lakini hatuendani naye kabisa.

Rafiki zangu wakija kunisalimia inabidi niseme tu ni mtoto wa ndugu yake na mume wangu lakini si mtoto wa mume wangu. Mtoto ana miaka mitano, ana akili, kachangamfu anajua kila kazi na ananiheshimu. Yaani kangekua katoto kazuri ningekapenda balaa kwani kana heshima sijui nikuambieje Kaka, lakini shida nashindwa, nikimuangalia wakati mwingine najiikuta na hasira tu nampiga hata bila sababu.

Hali hiyo inaniumiza kwani mwisho kanakuja kuniomba msamaha wakati hata hana kosa. Yaani kuna vitu vingine najikuta nagomba mpaka basi, nakua tu na chuki na mtoto. Wakati mwingine namfanyia visa tu ili kumpiga, mfano juzi nilimuwekea chakula kingi makusudi ili aache kula, basia liacha nikajikuta nampiga kuwa anachezea chakula basi nikamlazimisha kula na kweli alikula lakini alishindwa hata kunyanyuka yaani anapepesukapepesuka ila alimaliza na kuosha vyomboa akaosha.

Nilijisikia vibaya kwani sikupata faida yoyote, hali hii inanifanya nakua na kisirani, nakua mtu wa hasira hata kwa mume wangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, nataka kuongea na mume wangu amuondoe huyu mtoto ampeleke kwa Bibi yake. Mume wangu wazazi wake wamefariki lakini ana ndugu wengine, kuna Baba mdogo wake na wengine tu ambao wana uwezo.

Sio kama si mtaki moja kwa moja lakini aondoke tu ili niwe sawa maana nahisi naweza kumuua huyu mtoto. Shida ni kwamba mume wangu anampenda sana mtoto na kwakua yeye alilelewa na ndugu baada ya wazazi wake kufariki basi anasema kuwa mwanae hawezi kulelea na mtu mwingine yoyote na aliniambia kabla hata hatujaanza mahusiano, nisaidie kaka nifanye nini maana nahisi kuchanganyikiwa.

Je kama ni wewe ndio unaombwa ushauri kama huu, utamjibu nini, utamuacha salama kweli?
Dah sema kinakachomtokea hatasahau
 
Na wewe pia una roho mbaya tu kwa haya majibu yako.
Ni heri niwe nayo haiwezekani uzae hovyo bila mpango then uje u force mtu akulelee uzinzi wako, Tena uzae hovyo wewe si ndo una roho mbaya hujali huyo mtoto.
Kabla ya kuita watu roho mbaya wewe Ni mjinga unaleta kiumbe duniani ambacho hakikukuomba ukilete then uanze kuhangaisha mtoto na mama tofauti ka si uchawi Nini.
 
Ndio maana Mimi hupenda mtoto alelewe na mamake atleast afikishe umri wa kujitambua ka fourtenn hivi ndo aende kwingine, Sasa wanaume mnazaa hovyo mnategemea Mana mwingine ampende mwanao huo ni ukichaa mkubwa, acheni kutesa watoto, kikawaida binadamu wenye upendo wa kweli wameisha, na hata ukiwa na upendo huwezi linganisha na upendo wa mtoto wako tumboni lazima tu ubague, I prefer kila mtu alelee mtoto had awe mkubwa, kila mtu ashinde mechi nyumbani kwake.
N roho mbaya tu zinawasumbua
 
Hurumianeni mlio ardhini na alie mbinguni atawahurumia kwani n mwingi wa huruma!!

MTU hana baya analokufanyia roho mbaya ya nini???

uchawi sio lazima ushike tunguli ndo funzo ambalo tunatakiwa tulipate sisi ambao hatujaoa,kuna wanawake sio wachawii ila roho zao zinaweza kufanya wakaingia katika uchawii [emoji19][emoji19]

Wanaume tufanyeni uhuni wote ila katika kuoa tuwe very selective kwajili ya afya ya familia!!
 
Ni heri niwe nayo haiwezekani uzae hovyo bila mpango then uje u force mtu akulelee uzinzi wako, Tena uzae hovyo wewe si ndo una roho mbaya hujali huyo mtoto.
Kabla ya kuita watu roho mbaya wewe Ni mjinga unaleta kiumbe duniani ambacho hakikukuomba ukilete then uanze kuhangaisha mtoto na mama tofauti ka si uchawi Nini.
Bado nakazia hiyo ni roho mbaya.

Wewe kwa style yako hiyo hata housegirl huwezi kuishi nae wala mtu baki yoyote zaidi ya ndugu uliozaliwa nao tumbo moja.

Watu wa hivi wanakaa na housegirl hata sita kwa mwaka mmoja kila wanakushindwa sbb ya toho mbaya.
 
Bora niwe na hyo roho mbaya kuliko unafiki, wewe unazaa na kuja kumtesa mtoto ambaye hakuomba umzae Ila ilikuwa tu starehe zako, yet unataka ku force ulewewe mtoto wako huo si ukenge mtupu, kila mtu abebe msalaba wako.
Mimi huwa si entertain ujinga wa aina yoyote si kwa ndugu au mtu Baki nasimamia kitu kilicho sahihi, by the way hamna mtu anayeshindwa kukaa na Mimi maana huwa si force Mambo.
NB. Narudia Tena acheni ukenge wa kuzaa hovyo Kama hamuwezi kuendelea na watu mliozaa nao, Mambo ya kutesa watoto kwa kuwayumbisha kisa lack of self control kwangu hayana nafasi. Kabla ya kuzaa hovyo fikirieni hao watoto wenu na mikaganyiko wakulelewa na watu Baki.
 
Back
Top Bottom