KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Tatizo ni ku'define' "Janga la Kitaifa"Nasisitiza ule wito wangu wa siku zote kwenye hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", kwenye issues za kitaifa yakiwemo majanga mbalimbali, Watanzania tusimame pamoja kwa uzalendo, umoja, upendo na mshikamano na serikali yetu kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, regardless political affiliations zetu, sisi Watanzania lets pray and stand as one against Corona
Huu ndio mtizamo wangu na ukitaka ufafanuzi nitatafuta nafasi nifafanue.
Hii 'issue' ya uzalendo ndipo panapoanzia kuwekana usingizi.
Wengine huona 'uzalendo' kwa mtizamo wa manufaa kwao tu na sio lazima kwa manufaa ya taifa.
Niseme tu kiufupi - kuna unafiki mwingi unaoambatana na matumizi mabaya ya maneno haya: uzalendo; manufaa ya taifa, n.k.
Mimi nakataa unafiki. Kama unasimama na mama Tanzania, simama naye kweli kweli.
Ngoja niachie hapa.
Siungi mkono hoja yoyote inayoiombea Tanzania majanga kwa aina yoyote. Tutatafuta njia zetu wenyewe kuyaondoa yanayotusononesha mioyo yetu kwa njia zetu wenyewe.