1. Ni vibaya kumtakia mtu yeyote kupata ugonjwa wowote. Sembuse nchi nzima.
Hili kwangu halina mjadala.
Nakwenda mbali zaidi ya mtu, nasema kiumbe.
Ni vibaya kumtakia kiumbe yeyote kupata ugonjwa wowote.
Naenda mbali zaidi.
Badala ya ugonjwa, nasema mabaya.
Ni vibaya kumtakia kiumbe yeyote kupata mabaya yoyote.
Nimesoma Jainism. Wanaoikubali dini hii hawataki hata kumkanyaga sisimizi, waketembea hufagia mbele yao iki wasikanyage kiumbe na kukiua.
Nawaelewa sana.
2. Naweza kuelewa frustrations za mtu ambaye haipendi serikali iliyopo madarakani Tanzania mpaka akataka ugonjwa ufike Tanzania ili serikali iwe exposed ilivyoshindwa.
3. Mawili haya hayana contradiction.
4. Naweza kuwa simtakii mtu yeyote mabaya, sitaki ugonjwa wowote uweze kuwepo kwa kiumbe chochote, halafu, hapo hapo nikaelewa kwa nini kuna watu wanataka Corona ije Tanzania ili iwe moto utakaounguza machafu na kuanika mabaya.
Sent from my typewriter using Tapatalk