Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?

Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?

Kwahiyo wew ulitakaje, serikali yako iendelee kutesa upinzani na kuwavunja mikono.. Si bora uje ili hao police na serikali yako iogope kuwashika upinzani na ipambane na corana na ikiwezekana watu Wa ccm waupate huo ugonjwa ili waache kuwatesa na kuwavunja mikono wapinzani.. Tena na wewe ulivyo mnafiki uupate ili uache unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku zote kiboko kitabaki matakoni mwa mpumbavu. Ukitaka ujue, hiyo corona iingie, alafu uende magereza kutia upumbavu wako uone kiboko chake!
 
Pascal Mayalla,
P.
Umetikisa kibuyu kilichojaa nyongo na pilipili kuwa mvumilia nyongo itapikwapo harufu yake inaweza kumtapisha Anae uguza pia,
Hasira zetu hazichagui Neno bora wewe umeanzisha Mada ya kututapisha nyongo zetu acha tutapike tu.
 
1. Ni vibaya kumtakia mtu yeyote kupata ugonjwa wowote. Sembuse nchi nzima.

Hili kwangu halina mjadala.

Nakwenda mbali zaidi ya mtu, nasema kiumbe.

Ni vibaya kumtakia kiumbe yeyote kupata ugonjwa wowote.

Naenda mbali zaidi.

Badala ya ugonjwa, nasema mabaya.

Ni vibaya kumtakia kiumbe yeyote kupata mabaya yoyote.

Nimesoma Jainism. Wanaoikubali dini hii hawataki hata kumkanyaga sisimizi, waketembea hufagia mbele yao iki wasikanyage kiumbe na kukiua.

Nawaelewa sana.

2. Naweza kuelewa frustrations za mtu ambaye haipendi serikali iliyopo madarakani Tanzania mpaka akataka ugonjwa ufike Tanzania ili serikali iwe exposed ilivyoshindwa.

3. Mawili haya hayana contradiction.

4. Naweza kuwa simtakii mtu yeyote mabaya, sitaki ugonjwa wowote uweze kuwepo kwa kiumbe chochote, halafu, hapo hapo nikaelewa kwa nini kuna watu wanataka Corona ije Tanzania ili iwe moto utakaounguza machafu na kuanika mabaya.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Kwahiyo wew ulitakaje, serikali yako iendelee kutesa upinzani na kuwavunja mikono.. Si bora uje ili hao police na serikali yako iogope kuwashika upinzani na ipambane na corana na ikiwezekana watu Wa ccm waupate huo ugonjwa ili waache kuwatesa na kuwavunja mikono wapinzani.. Tena na wewe ulivyo mnafiki uupate ili uache unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio napata picha zaidi kuwa wenye akili nzuri hawawezi kuishi upinzani(chadema) watakaweza ni wale waliofyetuka akili na kupigwa segerea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo letu bado tuna imani za kishirikina sana. Tunafikiri kuwa eti kwakuwa kuna mtu kaposti kotona ije ndiyo atawezesha ije? Kwani Mungu ni mjinga sana mpaka atume ugonjwa unaoombwa na mjinga mmoja uletwe kwetu?

Coronavirus husambaa kwa njia za kisayansi zinazojulikana na kila mtu, na siyo kwa njia ya maombi, hasira, hisia, au chuki mtu alizonazo dhidi ya serikali au dhidi ya watu wengine.

Binafsi namwona mtoa posti kama mjinga anayepoteza muda wake tu. Kwa hiyo posti pekee Coronavirus hawezi kuingia nchini. Hata tungemwachia Jamiiforums aweke mamilioni ya posti za aina hiyo kwa miaka 100 bado kirusi cha Korona kakiwezi kuingia au kusambaa.

Nadhani kuna mambo mengine ni ya kupuuzia tu. Ukibahatika kukutana na mtu anayejaribu kuyachota maji ya bahari kwa kutumia ndoo akiamini kuwa kina kitapungua utabishana naye?

Niishie hapa, tuache imani za kishirikina.
 
Asante sana mkuu P, kwa bandiko lako litasaidia sana kufikisha ujumbe wa mariadhiano.Huenda shauri jipya kina Mh.Bulaa na Mdee zikafutwa.Watanzania juma zima habari za CDM, tuache tupishe elimu korona na maendeleo pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga,
Kusambaa kwa Corona kamwe hakutasababishwa mtu fulani kutaka au mtu fulani kutotaka. Corona na magonjwa mengine hutokeza kwa njia za kisayansi pekee.

Hapa naona mjadala mnaupeleka kwenye ushirikina zaidi.
 
Umehamisha magoli

Deal na la kuvunjwa mkono bila kuombew mabaya

Corona ina macho sasa itachagua nani cdm nani ccm?
Ije tu na ianze na wapuuzi kama nyie mnaoshangilia maovu kisa tu yanawapata watu mnaotofautiana nao itikadi.
 
Wawakilishi wangu ndiyo nguvu yangu. sasa hao wanapotezwa na Jiwe. hata Jiwe anapotza wapendwa wangu kama itakavyokuwa Corona, hawana tofauti na Jiwe
Kwanini sasa usipambane wewe mwenyewe na mbaya wako kuliko kutaka tukose wote hadi ambao hatuhusiki na kuwapoteza hao wawakilishi wako,hasa ukizingatia idadi kubwa ya wawakilishi wako wameamua wenyewe kuungana na mbaya wako.
 
Ndio napata picha zaidi kuwa wenye akili nzuri hawawezi kuishi upinzani(chadema) watakaweza ni wale waliofyetuka akili na kupigwa segerea

Sent using Jamii Forums mobile app

You need to think deeper, usilichukulie hili jambo juu juu, ni kwa nini watu wamefika huko? na huyo aliyesema hilo si lazima awe mwana chadema anaweza kuwa mtu mpenda haki asiye na chama lkn anagadhabishwa na matendo ya serikali.
 
pasco hujaacha tu tabia ya kuwachongea wanaotoa mawazo ambayo wewe huyapendi?.

inasemekana hata kabendera ulimchongea hivihivi, baadae yakaja kumkuta ya kumkuta.
Kwa hiyo ndio kusema hata huyu aliyeombea mabaya nchi ya Tanzazania atadakwa kama Eric! Basi P anatisha.
 
Kusambaa kwa Corona kamwe hakutasababishwa mtu fulani kutaka au mtu fulani kutotaka. Corona na magonjwa mengine hutokeza kwa njia za kisayansi pekee.

Hapa naona mjadala mnaupeleka kwenye ushirikina zaidi.

Una makosa mengi.

Lakini kwanza kabisa...

Kusambaa kwa Corona kunaweza kuongezwa na mtu kutaka, kisayansi.

China kuna watu wameambukizwa Corona, wanaenda kwenye lift, wanapaka mate yao kwenye buttons za lift.

Watu wanaokuja kwenye hizo lift na kushika buttons hizo wanaweza kuambukizwa.

Hiyo ni sayansi.

Ukikataa ukweli kwamba mtu anaweza kusambaza Corona kwa makusudi, unakataa sayansi.

Sasa wewe unakataa kwamba mtu anaweza kuamua kusambaza ugonjwa na kuusambaza?

Ukusema mtu hawezi kusambaza uginjwa kwa kutaka kama hivyo, wewe ndiye mshirikina.

Maana unapinga sayansi ya virology inayosema mtu anaweza kusambaza ugonjwa kwa makusudi.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Kwanini sasa usipambane wewe mwenyewe na mbaya wako kuliko kutaka tukose wote hadi ambao hatuhusiki na kuwapoteza hao wawakilishi wako,hasa ukizingatia idadi kubwa ya wawakilishi wako wameamua wenyewe kuungana na mbaya wako.
kama siyo wewe, wajukuu wako watakuta madhara ya huyu mtu. Tpambane na wewe uwemo pia...
 
Kiranga,
Hapa nadhani umehamisha magoli. Mtoa mada anasema kuna mtu anaombea ugonjwa uje. Kinyume cha sayansi. Hakuna mahali mtoa mada kasema kuwa kuna mtu anausambaza kwa makusudi ili awaambukize wengine.
 
Back
Top Bottom