Mtu mjinga sana anaweza kupata mafanikio makubwa katika maisha?

Mtu mjinga sana anaweza kupata mafanikio makubwa katika maisha?

Mtoa maada hajataja ujinga kwenye eneo Specific, Amejenga hoja kupitia neno ujinga kiujumla.

Ujinga ni kutokujua au kutokuwa na maarifa katika maeneo fulani.

Kama umefanikiwa katika eneo fulani inamaanisha ulipata maarifa kwenye eneo hilo ukaondoa ujinga then ukachukua hatua, ukafanikiwa.

Hayo matendo ya udhulumaji, uuaji na utapeli baada ya wewe kufanikiwa ni sahihi kabisa, si matendo ya kiungwana.

Mafanikio ya kweli ni kuuondoa ujinga huku ukitenda matendo ya busara katika jamii.
Kotokujua jambo au kuwa na maarifa hasa ya taaluma fulani sio ujinga. Ujinga unahusiana zaidi unavyo interact(unavyoingiliana) na jamii iliyokuzunguka pamoja na mazingira kwa ujumla.
 
Less intelligence, more success..

Kwa sababu intelligence inafanya analysis lakini pia ina purpose kubwa zaidi ya pesa.

Huu ndio uhalisia kwa sababu nchi zetu hizi hazina systems kali za watu wenye ubunifu au ugunduzi kuwa matajiri zaidi ya watu wanaoweza kuchukua risks, migodini, mashambani na kwenye uchuuzi.

Kwa hiyo kwa Tanzania hii naamini mtu ambaye ni less intelligent ambaye anaona pesa ndio end goal pekee pasipo kujifungamanisha na purpose au professional projections zozote.. Ana nafasi kubwa ya kutoboa
 
Hapana, unachanganya mambo. Kotokujua jambo fulani hasa linalohusiana na taaluma sio ujinga au kuwa mjinga, ni kwamba hujui tu hilo jambo.
Yaah! Huko kutokujua ndiyo maana ya Ujinga wenyewe.

Mfano mtu anayeishi na mtu mwenye HIV ila hajui kwamba ukimwi unasababishwa kwa Kutumia dodoki la kuogea ataendelea kuwa mjinga unless apate Elimu hiyo.

Ujinga hauingiii kwenye kitu ambacho hukifahamu kabisa wala huelewi kama kipo na huwezi fikiria kupata maarifa kukihusu, Ila kama upo nacho kila siku au unakiona kila siku ila huna maarifa sahihi kukihusu ndiyo ujinga wenyewe.

Tujikite kwenye maada zaidi mfano - Mtu anayefanya biashara ili mradi tu anafanya kazi bila kujua kutunza fedha ni Mjinga unless aamue kujifunza eneo hilo.
 
Less intelligence, more success..

Kwa sababu intelligence inafanya analysis lakini pia ina purpose kubwa zaidi ya pesa.

Huu ndio uhalisia kwa sababu nchi zetu hizi hazina systems kali za watu wenye ubunifu au ugunduzi kuwa matajiri zaidi ya watu wanaoweza kuchukua risks, migodini, mashambani na kwenye uchuuzi.

Kwa hiyo kwa Tanzania hii naamini mtu ambaye ni less intelligent ambaye anaona pesa ndio end goal pekee pasipo kujifungamanisha na purpose au professional projections zozote.. Ana nafasi kubwa ya kutoboa
Kama ni hivi mkuu ina maana kuwa intelligent sana katika nchi zetu hizi ni kama laana/mkosi fulani?!
 
Kama unakubali kua mleta mada hajataja ujinga kwenye eneo specific basi unatakiwa ukubaliane na ujinga utakaotajwa kwenye maeneo mengine pia,
Ndio tunarudi kule kule kua kila mtu ana ujinga wake,nobody is perfect.
Hii uko sahihi, Kila mtu ni mjinga kwenye eneo fulani mpaka pale utakapopata elimu kuhusiana na jambo hilo.

Ndiyo maana kuna Shule, Zisingekuwepo shule na Taasisi zingine za elimu tungekua wajinga sana.
 
Kotokujua jambo au kuwa na maarifa hasa ya taaluma fulani sio ujinga. Ujinga unahusiana zaidi unavyo interact(unavyoingiliana) na jamii iliyokuzunguka pamoja na mazingira kwa ujumla.
Je, usingeenda shule, ungekulia mazingira ambapo ni ngumu kupata Elimu kuhusiana na Maisha, Pesa na Mambo mengine uliyojifunza, Ungekua sio mjinga?

Unadhani kwanini msomi kama nyerere alisema Ujinga ni chanzo cha umasikini? na moja ya hatua kubwa iliyochukuliwa ni kutoa elimu kwa watu ili kuuondoa ujinga.
 
Hii uko sahihi, Kila mtu ni mjinga kwenye eneo fulani mpaka pale utakapopata elimu kuhusiana na jambo hilo.

Ndiyo maana kuna Shule, Zisingekuwepo shule na Taasisi zingine za elimu tungekua wajinga sana.
Kuna watu wanasoma mpaka chuo wanapata degree ila bado ni wajinga sana kuliko ambao hata hawajafika chuo kikuu.
 
Je, usingeenda shule, ungekulia mazingira ambapo ni ngumu kupata Elimu kuhusiana na Maisha, Pesa na Mambo mengine uliyojifunza, Ungekua sio mjinga?
Kuyaelewa maisha sio lazima kwenda shule tu, ujinga pia unachangiwa na genes pamoja na mazingira yanayokuzunguka na jinsi umepata exposure nyingi za nje.
 
Kuna watu wanasoma mpaka chuo wanapata degree ila bado ni wajinga sana kuliko ambao hata hawajafika chuo kikuu.
Si kweli, Mtu msomi yuko vizuri sana kwenye eneo alilolisomea mfano Daktari aliyekaa darasani miaka 6 huwezi kumuita mjinga kwenye taaluma yake hiyo.

Ila huyohuyo daktari ukimpeleka shambani au kwenye biashara atakuwa mjinga tu kwa muda fulani kisha atajifunza kuhusiana na hizo sekta na huo ujinga utaondoka.
 
Kuna watu wanasoma mpaka chuo wanapata degree ila bado ni wajinga sana kuliko ambao hata hawajafika chuo kikuu.
Na hapo ndio utaona utofauti wa education and intelligence,

Mwenye elimu ni yule ambaye amejifunza kutoka kwa wengine, ambapo mwenye akili anaweza kuchukua kile alichofundishwa na kukitumia kwa ubunifu,Mtu mwenye elimu anaweza kuwa na ujuzi na mambo mengi ya hakika, lakini mtu mwenye akili anaweza kuyatumia katika njia mpya ili kupata masuluhisho ya matatizo,

Elimu imefocus kwenye memorization But true intelligence lies in learning from experience,solving problems and apply knowledge,

So,elimu sio tu unaipata kwa kukaa darasani,kuna Formal education na Informal education.
 
Sheria namba mbili inajibu swali lako.

1735720679937.jpeg
 
Kama ni hivi mkuu ina maana kuwa intelligent sana katika nchi zetu hizi ni kama laana/mkosi fulani?!
Sana, kwanza utateseka sana kwa kuwa na ufahamu wa vitu vinavyoendelea nchini na kikubwa zaidi ile hali ya kutaka vitu viwe organized au fair kwako au hata kusimamia principles binafsi dhidi ya uchawa au unethical behaviours zinazofanya watu wafanikiwe, lazma uchelewe au ufe umaskini kwa sababu utatumika tu kutajirisha wengine..

Kwa hiyo kwa Tanzania ilivyo, intelligence ni muhimu lakini ni kitu extra sana kwa hiyo lazma mtu awe aggressive kiasi cha kufanya lolote linawezekana kufanikiwa.

Angalia tu kuanzia bungeni, utaliona hili kwa hiyo it's true, high intelligence kwa nchi zetu ni laana especially kama mtu huna back up nzuri ya familia.
 
Na hapo ndio utaona utofauti wa education and intelligence,

Mwenye elimu ni yule ambaye amejifunza kutoka kwa wengine, ambapo mwenye akili anaweza kuchukua kile alichofundishwa na kukitumia kwa ubunifu,Mtu mwenye elimu anaweza kuwa na ujuzi na mambo mengi ya hakika, lakini mtu mwenye akili anaweza kuyatumia katika njia mpya ili kupata masuluhisho ya matatizo,

Elimu imefocus kwenye memorization But true intelligence lies in learning from experience,solving problems and apply knowledge,

So,elimu sio tu unaipata kwa kukaa darasani,kuna Formal education na Informal education.
Exactly, kuna watu mitaani ukiongea nao unajua kabisa hiki ni kichwa lakini hakikupata supportive environment ya kuweka intelligence yake darasani. Na kuna wengine tu, kafika chuo kwa sababu alipata supportive environment

Na pia mkuu, mfumo wetu wa maisha ya Tanzania haujaweka segments mbalimbali ili watu wenye vipawa tofauti waweze kutumia intelligence yao to the maximum. Mfano

Kuna watu ni THINKERS, wanaweza kufikiria solutions na ideas kali sana Ila sio good implimentors, na kuna wengine ni implementors Ila sio good Thinkers.

Kwa wenzetu huwa wanawachukua hawa THINKERS na kuwapa best position kwa sababu wao huwa visionary Ila implementors huwekwa katika position za utendaji. Japo mtu akiwa ni thinker na implementors anakuwa katika position nzuri ya kufanikiwa

HUKU KWETU, tunaangalia nani anaweza kufanya nini, anaweza kuongea, anaweza kushawishi.. Na hata katika creative works wanaolipwa vizuri ni videographers au singers tofauti na watu waliotengeneza ideas.. Ndio maana tuna class ya juu ya implementors kiasi mambo yanafanyika lakini haichukui degree kuona tu kuwa nchi inaenda pasipo direction maana kila rais anakuja na lake..

But seriously, tunahitaji THINKERS ambao ni bigger brains kiasi cha kucheza na mifumo na mikataba maana ndio dunia ilipo. Japo kiuhalisia silioni hili kutokea

So kwa Tanzania hatuna mifumo mizuri ya kuhakikisha high intelligent people wanatoboa au kushika position za juu ambazo machawa wanazifikia kirahisi kwa kujua kula na vipofu
 
K
Mtu ambaye ana uelewa duni sana wa mambo mengi na ya msingi maisha, ambaye kiwango cha common sense kwake ni kidogo, uwezo mdogo wa fikra tunduizi.
Ngumu sana kukuelewa, maana hata hiyo common sense ni utata tu, au unamaanisha mtu ambaye hajui kusoma wala hesabu na akifundishwa hataelewa? Ambaye huyu atakuwa mlemavu wa akili

Ila kwa mtu wa kawaida ambaye akifundishwa kusoma na kuhesabu ataelewa, anaweza kupata mafanikio makubwa tu kutegemeana na fursa alizokutana nazo
Au anaweza kuwa na kipawa fulani, kama cha kuimba, mpira n.k
Au kaachiwa urithi na wazazi wake, au alikuwa wa kwanza kuwahi fursa ama kufanya jambo fulani,
 
Mtu ambaye ana uelewa duni sana wa mambo mengi na ya msingi maisha, ambaye kiwango cha common sense kwake ni kidogo, uwezo mdogo wa fikra tunduizi.
Kuna jamaa mmoja wa kutokea mkoani kigoma niliwahi kuconnect nae baada ya kukutana katika mambo ya biashara, hakuwa jamaa mwenye exposure ya mambo mengi sana kwani hata mkikaa mkimaliza stori za kibiashara hamuwezi kuwa na vitu vingine vya kuongea labda kwenye mpira ligi ya ndani pekee (kwa maana ni shabiki wa utopolo lialia).

Ila ni jamaa ambae hata kusoma hawezi ila anauwezo mkubwa sana wa kukariri mambo.

Kuifanya hii story iwe fupi ni kwamba huyu jamaa ni mtu ambae amefanikiwa katika mambo ya kibiashara.

Kwahiyo kupitia uzoefu huo, nafikiri mambo haya ya fedha yanaweza kumtembelea mtu yeyote ambae anazo akili timamu za kujiongoza bila kujali exposure aliyo nayo mtu.
 
Back
Top Bottom