Mtu mwenye akili timamu hawezi kula kumbikumbi

Mtu mwenye akili timamu hawezi kula kumbikumbi

Shule zifunguliwe tu kwa kweli
 
Zambia na DRC maeneo kama Lubumbashi wanakula ile midudu washa inakuwa kwenye miembe kipindi cha mvua...

Unakuta wamesonga bonge la ugali, na kwenye bakuli imejaa ile midude imekaushwa...
Yani yale madude nilikuwa sijui kama kuna mahala wanakula, nilipofika SA nilishangaa sana, basi itakuwa ukanda huo wote wanayala.
Halafu wanasema ni nzuri sana kwa waja wazito maana yanaongeza damu
 


Nenda Kigoma Ukajionee

Wanapotoka Watu Hukaa Juu Kichuguu Ama Eneo Wanapotoka Mchana Kutwa Kukamata
wenyewe Wanaita NswaA
 
Huyu mchaga baada ya kupakiliwa juzi na jana naye kaleta uzi anamalizia hasira kwa wahaya
 
Cha ajabu asiyekula kumbikumbi akiwa na upungufu wa damu atachangiwa damu na anayekula kumbikumbi.

Yule asiyekula kitimoto na kumuita mwenzake kafiri naye akiumwa upungufu wa damu naye ataongezewa damu na hao hao makafiri na wala kitimoto.
 
Mtoa uzi umeweka utata kwenye hoja yako ndo maana unashambuliwa vikali. Ungekuwa na hadidu rejea kwa nini unasema hivyo. Umekurupuka toka usingizini kuleta uzi.
 
Bora hata kumbi-kumbi,

Hapo kongwa kwa Ndungai watu wanarost viwavi jeshi na kuwatafuna na ugali.
 
Yani yale madude nilikuwa sijui kama kuna mahala wanakula, nilipofika SA nilishangaa sana, basi itakuwa ukanda huo wote wanayala.
Halafu wanasema ni nzuri sana kwa waja wazito maana yanaongeza damu

Doh! kweli tembea uone
 
Haiwezekani mtu na akili zako timamu ukala kumbi kumbi

Chakula chochote ni chimbuko la asili la jamii husika na kwa ujumla ni sehemu ya tamaduni za jamii husika.

Ukienda sehemu ukakuta wenzio wanatumia chakula cha aina fulani kama hali hiyo:
1: Haivunji sheria
2: Haivunji haki za binadamu
3: Haiwaweki kwenye hatari ya kiafya
4: ........
Wewe kaa kimya, jiunge ukiweza na ikikushinda chapa mwendo.
 
Back
Top Bottom