Wala siyo la kushangaza wapo hadi wachoma chapati ,Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.
Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?
Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!
Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.
Tunakwama wapi?
Mkuu ni rahisi kama nilivyosema maana nimemaliza kozi tofauti na nimekua nazipata kazi hizo tu kwenye mashirika ya kimataifa...amini nakwambia..kutafuta na kupata kazi ni mbinu tofauti na ku graduate katika kozi husikaSiyo rahisi kama unavyosema. Graduates wa course hizo ni wengi mno. Wengi wanahangaika mitaani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Piga kazi mkuu, yupo mwingine ni mtu wangu sana. Huwa ananibeba mara nyingi sana. Amesoma International Relations hapo UDOM.Me nipo kitaa hapa napiga bodaboda na degree yangu, siri ya maisha aijuae Mungu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilijiongeza ufundi umeme maisha safi yanasonga!mimi na degree zangu mbili ni fundi seremala.
Umesoma course ganiWewe kweli ni mtoto. Watu wamemaliza vyuo mwaka 2013 na hawana ajira wewe unaongelea kuanza Chuo 2015!!!! Kama una ajira ni bahati tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Umemuelimisha vizuri. Hili ni tatizo la mindset za watanzania karibu wote, kuwa watu wanasoma ili wapate kazi nzuri zenye marupurupu na mishahara mikubwa. Ukimwongozea hapo tena na u-bosi basi anajiona yeye ni kila kitu. Jamani lengo la elimu siyo kuajiriwa. Lengo la elimu ni kupanua wigo wa kupambana na mazingira. Hapa JF mijadala ya kulaumu kuwa mtu amepoteza muda bure kwenye elimu ipo sana. Hii inaonyesha elimu yetu inavyowaandaa wahitimu wake. Kuna kipindi nilisoma member mmoja alikuwa analaumu kuwa Diamond mwanamuziki hajasoma lakini ana ''mkwanja'' kuliko maprofesa wa vyuo vikuu hivyo elimu haina maana yoyote! Just imagine mawazo fyongo kama haya tena yanatolewa na mtu mwenye elimu ya chuo! Bila kufumua mitaala ya elimu yetu na watu waende shule na vyuoni ili kuelimika na siyo kukariri kwa ajili ya kupasi mitihani kwa matarijio ya ajira nzuri hatutafanikiwa!Ufikiri wa jamii, na wewe ukiwemo ndio shida, hakuna kazi za walioelimika na wasioelimika, shuleni huwa tunaenda kusoma ili kupanua mawazo yatakayo tusaidia katika kuendesha maisha yetu.
Sasa hizi degree tunasomea, mengi ni mambo ya utawala, ndipo unajikuta umesomea, utawala wa biashara, au maendeleo ya jamii, lakin, ni biashara gani unayoitawala? skills za hiyo biashara hauna, Au maendeleo ya jamii, je jamii inajihusisha na kazi zipi? hauna hiyo elimu.
Ni kweli kuna kashida kadogo kwenye mfumo wa elimu wetu, nao ni hako ka kuto incoroprate vocational training kwenye mafunzo yetu. Dogo kasoma, kaona anahitaji kujifunza cherehani, ili labda sasa aje atumie elimu yake ya chuo kikuu, kuendesha biashara ya cherehani, kwanza apatie mtaji,kisha ajikite huko. Wazo ambalo ni jema sana, na namuunga mkono 100%. Amini amini nakuambia, kwa moyo ambayo huyo dogo anaonesha, kuna kitu amekiona kwenye huo mchoro wake, na ndio manufaa ya elimu hayo. mwache aende, 5 years anaweza kuwa na story ya tofauti kuliko huyo fundi anaemfundisha? Je Haukusoma habari za mafundi vyerehani waliobahatika kutoka nchini mwetu hapa? Akina Speshoz, na Wengine, Kama Speshoz ni ana had masters kabisa, kaanza na kushona pia ila leo ana biashara kubwa ya fashion na sports. Sasa kwa nini kijana wa miaka 30, ndio anamikataba ya jezi kwa timu mbalimbali nchini, na ndo anaivalisha stars na Wasanii kama Diamondplatunuzm, anashina suti za harusi kwa bei karibu na mshahara wa miezi mitatu wa mwalimu mwenye degree? ni kwa sababu hakuwa fundi cherehani wa kawaida, nini kilimfanya asiwe fundi cherehani wa kawaida, ni Elimu yake ya masters. Na unajua ni kwa nini kwanini sio wote wenye elimu ya masters na hata wengine maprof hawaingizi mkwanja mrefu kama anaongiza yeye saivi? ni kwa sababu yeye nje ya Elimu yake ya mastars ana ujuzi, huo ujuzi ambao wewe unadhani dogo kapotea kuutafuta saivi. Ujuzi wa kushona.
So muache dogo afanye anachoona, na hayo ndiyo matumizi ya elimu.
Kazi ya waliokosa elimu ndio kazi gani hizo ? kila kazi unayofanya ni lazima uwe na elimu nayo sasa umeipataje hiyo elimu utajua mwenyeweNimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.
Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?
Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!
Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.
Tunakwama wapi?
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.
Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?
Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!
Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.
Tunakwama wapi?
well saidDegree kitu gani? Wafundisheni watoto wenu wawe na skills nyingi.