Ufikiri wa jamii, na wewe ukiwemo ndio shida, hakuna kazi za walioelimika na wasioelimika, shuleni huwa tunaenda kusoma ili kupanua mawazo yatakayo tusaidia katika kuendesha maisha yetu.
Sasa hizi degree tunasomea, mengi ni mambo ya utawala, ndipo unajikuta umesomea, utawala wa biashara, au maendeleo ya jamii, lakin, ni biashara gani unayoitawala? skills za hiyo biashara hauna, Au maendeleo ya jamii, je jamii inajihusisha na kazi zipi? hauna hiyo elimu.
Ni kweli kuna kashida kadogo kwenye mfumo wa elimu wetu, nao ni hako ka kuto incoroprate vocational training kwenye mafunzo yetu. Dogo kasoma, kaona anahitaji kujifunza cherehani, ili labda sasa aje atumie elimu yake ya chuo kikuu, kuendesha biashara ya cherehani, kwanza apatie mtaji,kisha ajikite huko. Wazo ambalo ni jema sana, na namuunga mkono 100%. Amini amini nakuambia, kwa moyo ambayo huyo dogo anaonesha, kuna kitu amekiona kwenye huo mchoro wake, na ndio manufaa ya elimu hayo. mwache aende, 5 years anaweza kuwa na story ya tofauti kuliko huyo fundi anaemfundisha? Je Haukusoma habari za mafundi vyerehani waliobahatika kutoka nchini mwetu hapa? Akina Speshoz, na Wengine, Kama Speshoz ni ana had masters kabisa, kaanza na kushona pia ila leo ana biashara kubwa ya fashion na sports. Sasa kwa nini kijana wa miaka 30, ndio anamikataba ya jezi kwa timu mbalimbali nchini, na ndo anaivalisha stars na Wasanii kama Diamondplatunuzm, anashina suti za harusi kwa bei karibu na mshahara wa miezi mitatu wa mwalimu mwenye degree? ni kwa sababu hakuwa fundi cherehani wa kawaida, nini kilimfanya asiwe fundi cherehani wa kawaida, ni Elimu yake ya masters. Na unajua ni kwa nini kwanini sio wote wenye elimu ya masters na hata wengine maprof hawaingizi mkwanja mrefu kama anaongiza yeye saivi? ni kwa sababu yeye nje ya Elimu yake ya mastars ana ujuzi, huo ujuzi ambao wewe unadhani dogo kapotea kuutafuta saivi. Ujuzi wa kushona.
So muache dogo afanye anachoona, na hayo ndiyo matumizi ya elimu.