Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Kuna coz inaaitwa bee keeping[emoji28][emoji28] ipo UDSM
Wanachofundishwa ni sawa na elimu ya wazee wetu wazamani wasiyokuwa na elimu kabisa wa kimang'ati. Namtu anachukua elimu nadhalia miaka 3 mtoto aliyekulia masaki anayeogopa hata mende tatizo ni pale atakapo maliza kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Wala siyo la kushangaza wapo hadi wachoma chapati ,
Muhimu mkono kinywani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo rahisi kama unavyosema. Graduates wa course hizo ni wengi mno. Wengi wanahangaika mitaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni rahisi kama nilivyosema maana nimemaliza kozi tofauti na nimekua nazipata kazi hizo tu kwenye mashirika ya kimataifa...amini nakwambia..kutafuta na kupata kazi ni mbinu tofauti na ku graduate katika kozi husika
 
Matajiri wote ni waliopata ujasiri wa kujiajiri usishangae kesho na keshokutwa ana kampuni ya mitindo halafu wanao ndo maafisa masoko wake
 
Kushona cherehani wala sio tatizo,ila tatizo litaanza pale huyo mpwa wako atakapo amua kuweka mizizi kwenye cherehani pekee Hapo ndipo penye tatizo.

ila kama atashona cherehani kisha akajitanua na kuwaza vingine na vingine cherahani iwe kama mlango tu wa kuingilia basi nadhani mpwa wako chuo hakufika bahati mbaya.

nitashangaa sana kama december mwakani muda kama huu mpwa wako atakua pale pale kwenye kibaraza na cherehani yake,hapo nitasema mpwa wako kweli angetakiwa tu kuishia la saba.

ila kama mwakani Muda kama huu mpwa wako utamuona kaimarika,mtaji wa cherehani umesimama,yupo kwenye ofisi yake basi tambua mpwa wako elimu yake inamsaidia.

Siku zote naumia sana kuona mtu anafanya kazi ile ile miaka na miaka mpk wanambatza jina"fundi nguo" "mshonaji",nk kwakweli naumiaga sana,Mpwa wako kaamua kuja ktk ujasiriamali kamshauri akili isijifungie hapo kwenye chumba cha ushonaji nguo,mwambie asione kafika.

Mwakani akuonyeshe vibiashara vingine alivyovifungua kupitia cherehani hapo ndipo tutampa BIG thumb kweli kweli ila mwakan imefika yupo kibarazani katundka nguo kama yule wa darasa la 7 aaaaah we jua umekula hasara kwa huyo mpwa.
 
Afanye tu kazi kwa bidiiii fungu alilochagua ni jema sana kuliko kazi ya mshahara 800k per month,nakuhakikishia mpwa wako kama yupo seriouz atapoanza tu kufanya hiyo kazi kwa uaminifu miezi 6 tu,Htakua na mawazo tena ya kuajiriwa na kama akitaka kuajiriwa atakua na vigezo vyake vya mwajiri anaetaka kumuajiri ataevifikia ndio atamuajiri.

Nakuhakikishia hutokaa umuone anazunguka na Bahasha tena na Tena,ukimuona ana bahasha ujue n katoka kununua chipsi basi wamemuekea humo kwa kua sku hz hamna mifuko.

Ujasirimali tena fundi kushona ina pesa hiyo kazi jamani sema basi tu watu tunadharau dharau kazi,acha uone mabalaa ya huyo mpwa wako "Nakutahadharisha tu" usije ukamuita mchawi akitoboa maana nakuhakikishia anaenda kutoboa na anapenya kweli.
 
Hapa Mwanza kuna kondakta wa daladala, ana degree ya mambo ya usafirishaji kutoka NIT - Dar (Chuo cha Usafirishaji - DAR), tena sio kwamba ni gari la nyumbani kwao laa hasha!
 
Bado anafaida kubwa sana ya kusoma ,atatumia elimu yake kuongesa ufanisi wa katika kushona kwa kutafuta wateja wengi ,kupanua soko la huduma yake ,kutumia technologia kwenye kushona na mengine mengi .Huwezi kufanya haya kama huna elimu ,ni sawa yawezekana haya anaweza kufanya haya ila ni kwa kuchelewa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufikiri wa jamii, na wewe ukiwemo ndio shida, hakuna kazi za walioelimika na wasioelimika, shuleni huwa tunaenda kusoma ili kupanua mawazo yatakayo tusaidia katika kuendesha maisha yetu.

Sasa hizi degree tunasomea, mengi ni mambo ya utawala, ndipo unajikuta umesomea, utawala wa biashara, au maendeleo ya jamii, lakin, ni biashara gani unayoitawala? skills za hiyo biashara hauna, Au maendeleo ya jamii, je jamii inajihusisha na kazi zipi? hauna hiyo elimu.

Ni kweli kuna kashida kadogo kwenye mfumo wa elimu wetu, nao ni hako ka kuto incoroprate vocational training kwenye mafunzo yetu. Dogo kasoma, kaona anahitaji kujifunza cherehani, ili labda sasa aje atumie elimu yake ya chuo kikuu, kuendesha biashara ya cherehani, kwanza apatie mtaji,kisha ajikite huko. Wazo ambalo ni jema sana, na namuunga mkono 100%. Amini amini nakuambia, kwa moyo ambayo huyo dogo anaonesha, kuna kitu amekiona kwenye huo mchoro wake, na ndio manufaa ya elimu hayo. mwache aende, 5 years anaweza kuwa na story ya tofauti kuliko huyo fundi anaemfundisha? Je Haukusoma habari za mafundi vyerehani waliobahatika kutoka nchini mwetu hapa? Akina Speshoz, na Wengine, Kama Speshoz ni ana had masters kabisa, kaanza na kushona pia ila leo ana biashara kubwa ya fashion na sports. Sasa kwa nini kijana wa miaka 30, ndio anamikataba ya jezi kwa timu mbalimbali nchini, na ndo anaivalisha stars na Wasanii kama Diamondplatunuzm, anashina suti za harusi kwa bei karibu na mshahara wa miezi mitatu wa mwalimu mwenye degree? ni kwa sababu hakuwa fundi cherehani wa kawaida, nini kilimfanya asiwe fundi cherehani wa kawaida, ni Elimu yake ya masters. Na unajua ni kwa nini kwanini sio wote wenye elimu ya masters na hata wengine maprof hawaingizi mkwanja mrefu kama anaongiza yeye saivi? ni kwa sababu yeye nje ya Elimu yake ya mastars ana ujuzi, huo ujuzi ambao wewe unadhani dogo kapotea kuutafuta saivi. Ujuzi wa kushona.

So muache dogo afanye anachoona, na hayo ndiyo matumizi ya elimu.
Umemuelimisha vizuri. Hili ni tatizo la mindset za watanzania karibu wote, kuwa watu wanasoma ili wapate kazi nzuri zenye marupurupu na mishahara mikubwa. Ukimwongozea hapo tena na u-bosi basi anajiona yeye ni kila kitu. Jamani lengo la elimu siyo kuajiriwa. Lengo la elimu ni kupanua wigo wa kupambana na mazingira. Hapa JF mijadala ya kulaumu kuwa mtu amepoteza muda bure kwenye elimu ipo sana. Hii inaonyesha elimu yetu inavyowaandaa wahitimu wake. Kuna kipindi nilisoma member mmoja alikuwa analaumu kuwa Diamond mwanamuziki hajasoma lakini ana ''mkwanja'' kuliko maprofesa wa vyuo vikuu hivyo elimu haina maana yoyote! Just imagine mawazo fyongo kama haya tena yanatolewa na mtu mwenye elimu ya chuo! Bila kufumua mitaala ya elimu yetu na watu waende shule na vyuoni ili kuelimika na siyo kukariri kwa ajili ya kupasi mitihani kwa matarijio ya ajira nzuri hatutafanikiwa!
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Kazi ya waliokosa elimu ndio kazi gani hizo ? kila kazi unayofanya ni lazima uwe na elimu nayo sasa umeipataje hiyo elimu utajua mwenyewe
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?

Nina dogo anauza Mitumba kigamboni huko kwenye minada.
 
Atafanya hiyo lkn baadaye atapata kiwanda usicheze na mtu shule
 
Mm naona hakuna alichokosea....kuwa fundi Nguo wakati una degree sio tatizo...uzuri degree yake inauhusiano wa karibu na kazi hiyo....kwa kuwa yeye amesoma basi kazi zake zinatakiwa ziwe zenye ubora zaidi ili kuakisi elimu yake ya degree....na akijipanga vizuri mbeleni anaweza kuja kuwa na viwanda vya nguo na akaajiri watu wengine...tuwe kama wahindi...wahindi wengi utawaona vyuoni lakini wakiisha maliza tu...hawaendi kuajiriwa bali kujiajir i. Kumbuka pia kuna group kubwa la wasomi walioajiriwa -na huko kwenye ajira mambo hayaendi sawa hivyo wanatafuta namna ya kutoka wajiajiri lakini mazingira yanawabana...muache mtoto ajiajiri- kuajiriwa ni utumwa.
 
Back
Top Bottom